Tuesday, April 11, 2023

Askofu Makundi wa IGMT aunga mkono juhudi za Tanzania kupinga mapenzi ya jinsia moja

 

Askofu mteule wa Kanisa la ITINERANT GOSPEL MINISTRIES (IGMT) Joshua Makundi

Watanzania wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, katika mapambano dhidi ya mmomonyoko wa maadili katika jamii. 

Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste Miracle Gospel Church  Tanzania (KMGCT) Askofu Dk. Godluck Manga katika ibada maalum ya Pasaka iliyoenda sambamba na tukio la kusimikwa kwa Askofu wa Makanisa ya ITINERANT GOSPEL MINISTRIES TANZANIA  (IGMT) Joshua Makundi, iliyofanyika kijiji cha Mambo Komakundi wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. 

Askofu Dk. Manga alisema ni jukumu la Wazazi na Walezi kushirikiana katika kuwakuza watoto kuwq na maadili yanayotakiwa kama vitabu vya dini vinavyoelekeza. 

"Inashangaza kuona kuwa licha ya kuwepo kwa elimu mema na mabaya lakini bado vitendo viovu vikiendelea kutendeka kwenye jamii,"alisema Askofu Manga. 

Dk. Manga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Maridhiano na Amani Tanzania,  alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan  kwa hatua yake ya kusimamia haki ya Mungu kwa kupinga ndoa ya jinsia moja na wao kama viongozi wa dini wataendelea kumuunga mkono katika hilo kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wote anapoliongoza taifa. 

Alisema ndoa ya jinsia moja sio mpango wa Mungu, hata maandiko matakatifu ya Biblia na Quran  inakataza vitendo hivyo, na kumpongeza Rais Samia, viongozi wa serikali, Wabunge na Wananchi kupinga jambo hilo ndani ya nchi ya Tanzania kwani sio maadili ya Mwafrika. 

"Kila mafanikio yana msingi wake na moja wapo ya msingi wa amani tuliyonayo sasa ni mafanikio ya ya Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa sehemu kubwa ya kuhamasisha amani ya nchi yetu, ameifungua kwa kuleta maridhiano ya kitaifa ndani ya taifa letu,"alisema Askofu Manga. 

Askofu wa Kanisa la Free Pentecostal Fellowship in Kenya (FPFK) Stephen Ojwang, alisema daraja jipya la uaskofu ambalo amelipata Askofu Joshua Makundi anatakiwa kwenda kuwa muajibikati katika kuihubiri injili kwa watu wote. 

Katika mahubiri yake Askofu Ojwang alisema huduma ya uaskofu ni kuendelea kutangaza Habari Njema ya  Wokovu wa Yesu Kristo na kwamba anatakiwa kwenda kuitenda kwa uaminifu. 

Kwa upande wake Askofu mteule wa Kanisa la ITINERANT GOSPEL MINISTRIES (IGMT) Joshua Makundi, alisema ameupokea uaskofu huo kwa moyo na kuahidi kufikisha neno la Mungu mbali huku akiomba waumini kumuombea katika kazi hiyo ya utume. 

Aidha  Kiongozi huyo Mkuu wa Makanisa ya (IGM)  Tanzania Askofu  Makundi alisema kama kanisa hilo haliko tayari kuunga mkono ndoa ya jinsia moja.kwani jambo hilo sio mpango wa Mungu. 

Askofu Joshua Makundi alisimikwa Jumapili ya Aprili 9,2023 kuwa Askofu wa Makanisa ya  ITINERANT GOSPEL MINISTRIES TANZANIA (IGMT) ambapo alikabidhiwa vitendea kazi kama Kiti, Fimbo ya kiuchungaji, Biblia, Katiba na Muongozo.










0 Comments:

Post a Comment