Thursday, April 13, 2023

Mfumo wa Mageuzi ya Kimfumo na Usimamizi unavyoinufaisha KCBL

Meneja Mkuu wa (KCBL) Godfrey Ng’ura, akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu mageuzi ya kimfumo na usimamizi unavyoinufaisha benki hiyo kuelekea kuwa Benki ya Taifa ya Ushirika ifikapo Juni 2023 (Picha zote na Johnson  Jabir/JAIZMELA Blog)


Benki ya Ushirika  Kilimanjaro (KCBL) imepitia mageuzi ya kimfumo na usimamizi ambao ifikapo Juni mwaka huu itakuwa Benki ya Taifa ya Ushirika. 

Akizungumza jana katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Meneja Mkuu wa (KCBL) Godfrey Ng’ura, alisema kCBL ni benki pekee iliyosalia hapa nchini ikitoa huduma kwa zaidi ya miaka 20 ambapo mageuzi ya kimfumo na usimamizi yataifanya kuwa Benki ya Taifa ya Ushirika. 

Benki ya KCBL  inashirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika TCDC, benki ya CRDB,  SCCULT, TFC na Vyama vya Ushirika kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika kupitia Benki ya KCBL  kwa kufanya mageuzi ya kimfumo na kiuendeshaji ndani ya KCBL  ili kuunda benki mpya ya Taifa ya Ushirika,"alisena Ng'ura. 

Meneja huyo alisema licha ya kupitia changamoto lukuki, lakini mwaka 2022 ameifanya KCBL kupata ongezeko la faida kwa mwaka wa pili mfululizo. 

"Tusingeweza bila ninyi wanahabari, moja wapo ya mafanikio haya ni kuongezeka kwa mtaji wa wanahisa hadi kufikia bilioni 4.4 kutoka bilioni 2.7 mwaka 2021. 

Aliongeza "Kumekuwa na ongezeko la zaidi ya akaunti elfu nane (8,000) na zimefanya miamala kwa mwaka 2022 kutoka elfu 15 za nwaka 2021 hadi kufikia elfu 21. 

Aidha Meneja alisema KCBL imepanua wigo wake wa huduma na kuanzisha bidhaa mpya za kubadili fedha za kigeni, mikopo kwa Wakandarasi, Wajasiriamali na vikundi vya akina mama na vijana. 

"Kwa mwaka 2022, tumeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma zetu kwa njia ya kidigitali kupitia KCBL,  Visa, ATM na Wakala, miundombinu hii imewapa fursa wateja wetu kupata huduma popote nchini,"aliongeza. 

Ng'ura aliongeza kuwa KCBL ilizindua mfumo mkuu mama wa kibenki bora na wa kisasa uitwao BR. Net ambao umekuwa ukiboresha huduma kwa wateja wake. 

Akizungumza kwa niaba ya wakulima na wanahisa wa benki ya KCBL  Gabriel Ollomi, alisema ukosefu wa weledi ndio uliochelewesha KCBL kuwa benki ya Taifa ya Ushirika. 

Kwa upande wake Mrajis wa Vyama vya Ushirika na mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, alisema dhamira ya Serikali ni kutumia mfumo wa ushirika katika kuwewezesha wananchi kiuchumi na kuchangia ipasavyo katika ustawi wao na wa Taifa kwa ujumla. 

"Kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha Ushirika unahamasishwa miongoni mwa watanzania na kusimamiwa kwa mujibu wa sheria ili kuwalinda na kuwanufaisha Wanaushirika," alisema Dk. Ndiege. 

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo na Biashara Frank Wilson akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Kilimanjaro Jackline Senzige 


Wafanyakazi wa KCBL katika picha ya pamoja mnamo Aprili 13, 2023 katika ukmbi wa mikutano wa Kili Wonders Hotel mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro



Imetayarishwa na Johnson Jabir, April 13, 2023

 





0 Comments:

Post a Comment