Ukistaajabu ya Musa, basi ujue ya Firauni yapo, ndivyo
unavyoiweza kusema baada ya tukio la kustaajabisha na kusikitisha baada ya
kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Matindigani Manispaa ya Moshi
Mkoani Kilimanjaro kufanya mapenzi na mama yake mzazi.
Sakata hilo ambalo limetokea siku za hivi karibuni katika
kata hiyo ya Pasua limeshuhudia mtafaruku miongoni mwa wakazi wa eneo hilo na
maeneo ya jirani huku kijana huyo wa kiume akikana kufanya vitendo hivyo na
mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 59.
Taarifa za kuhusika na vitendo hizo zilipatikana baada ya
mdogo wa kijana huyo wa kiume kuwakuta chumbani wakifanya vitendo hivyo ndipo
alipoamua kutoa taarifa kwa majirani kwa ajili ya msaada zaidi.
Hata hivyo kijana huyo wa kiume alisema kiuhalisi huingia
chumbani kwa mama yake lakini suala la
kufanya mapenzi na mama yake mzazi sio kweli
“Mara kadhaa nimekuwa nikifika chumbani kwa mama yangu, huwa
ninapendelea wakati wa kunywa pombe zangu ninaketi pembezoni mwa kitanda cha
mama yangu kasha ninaondoka zangu…tuhuma hizi ni za kusingiziwa,” alisema kijana huyo wa kiume.
Kijana huyo aliongeza kuwa siku ya tukio aliingia chumbani
mwa mama yake mzazi akiwa amelewa na alianza kunywa pombe nyingine na hatimaye
aliondoka.
Mama mzazi anayetuhumiwa kufanya vitendo hivyo alikana
kuhusika na kudai kuwa sio za kweli.
“Sijawahi kufanya kitendo hicho na mtoto wangu wala kumvulia
nguo, wala kumshuhudia kwa macho yangu mwenyewe akiwa kifuani kwangu,
ninapofanya kazi zangu nikimaliza huwa ninakwenda kunywa pombe, kisha narudi
zangu kulala…sijawahi kumkuta kifuani kwangu kwa macho yangu kabisa kwa kweli,”
alisema Mama mzazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Matindigani Amos
Pmachi na Diwani wa kata ya Pasua Pastori Minja walisema ulevi kupita kiasi
umekuwa ukichangia mmonyoko wa maadili na ndio sababu matukio kama hayo
huonekana kuwa ya kawaida.
“Suala la ulevi kupita kiasi linachangia kiasi kikubwa
vitendo vya ukatili.Sisi kama viongozi tunalikemea kwa nguvu zote lisiweze
kutokea tena katika jamii. Kwa ni ni tukio la aibu sana ,” waliongeza
Msaidizi wa masuala ya kisheria mjini Moshi Immaculata
Mwigane alisema wanatakiwa kusimamia maadili na malezi huku akitaka familia
zimrejee Mwenyezi Mungu.
“Mtoto huyu alipelekwa shule na kaka yake katika katika masuala ya ufundi wa magari lakini mama yake alimkatalia na kutaka aendelee kuishi nyumbani”, alisema Mwigane.
0 Comments:
Post a Comment