"Shule ni mahali pa kujifunza, hatutaki kubadili wazo hili, Haifai shule iwe kiwanda au shamba. Lakini lazima shule iwe kiwanda au shamba. Lakini ni lazima tuone kuwa kazi katika kiwanda cha shule au katika shamba la shule ni jambo la kawaida katika shughuli za kujifunza kuishi."
Tuesday, January 31, 2023
Mwalimu Nyerere: Shule ni Kiwanda au Shamba
Saturday, January 28, 2023
Simba fans trust new appointed CEO Imani Kajula
Imani Kajula, new CEO of Simba SC |
Trust is of utmost importance and an integral part of happy and fulfilling relationships, for both professional as well as personal relationships.
Without trust, relationships are like a life without oxygen. You will feel suffocated and fail to maintain because one or both parties feel insecure or let down.
Lincoln Davenport Chafee is an American politician. He
was mayor of Warwick, Rhode Island, from 1993 to 1999, a United States Senator
from 1999 to 2007, and the 74th Governor of Rhode Island from 2011 to 2015.
Chafee said, “Trust is built with consistency.”
UWT Moshi vijijini yajitayarisha kujenga Chuo cha Ushonaji
Hayo yalisemwa Januari 27,2023 na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rwaichi Kaale kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa Baraza la Jumuiya hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa chama hicho Wilayani humo.
Akizungumzia mpango kazi wa miaka mia Tano 2022-2027 Kaale amesema Jumuiya hiyo inakusudia kuwa na miradi ya kitegauchumi ili kuiwezesha Jumuiya hiyo kujiendeleza pasipo kutegemea wafadhili.
Kaale aliità ja miradi hiyo ni pamoja na Chuo cha ushonaji, kuanzisha kikundi cha mapishi, kuwa na mgahawa wa chakula na vinywaji pamoja na vyombo vya usafri kama vile bajaji.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa UWT Moshi Vijijini aliwaomba Wajumbe wa Baraza hilo kuvunja makundi na kuwataka kufanya kazi kwa pamoja ili kuendelea kuijenga Jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Moshi Vijijini Shakila Singano, alisema katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM Jumuiya hiyo imeshiriki upandaji wa miti pamoja na kuwasajili wanachama wapya 500 kwa mfumo wa Kieletroniki ambapo matarajio ni kusajili wanachama 3,000 kwa mwaka 2023.
Akifungua kikao hicho Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu amesema Serikali ya awamu ya sita imeipatia Wilaya hiyo kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mbili ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama.
Baadhi ya Wajumbe wa
Baraza la UWT Moshi Vijijini Gladness Mbwambo na Arapita Lyimo, wamesema
uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi ndani ya Jumuiya hiyo itaiwezesha UWT
kuondokana na utegemezi sambamba na kuwasaidia vijana wa kike kujiepusha na
ndoa za utotoni.
Polisi, DC Mwaipaya wafanya usafi kituo cha Afya Mwirange-Mwanga
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Watumishi wa kituo cha afya Mwirange, Januari 28,2023 wameshiriki zoezi la usafi wa mazingira katika baadhi ya maeneo yanayozunguka kituo hicho cha afya ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina yao na wananchi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Akizungumza mara baada ya zoezi la usafi Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Wilaya ya Mwanga (SSP) Hendry Nguvumali alisema, jeshi la polisi nchini lina kawaida ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
SSP Nguvumali alisema askari polisi wilaya ya Mwanga wameamua kuungana na wafanyakazi wa kituo cha afya Mwirange, ili kufanya usafi, lengo likiwa ni kuwa karibu na jamii pamoja na kutoa elimu kwa jamii itakayo lenga usalama wa Raia na mali zao, katika kuzuia na kupambana na uhalifu.
Akishiriki zoezi la usafi Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya alisema serikali wilayani humo imeungana na jeshi hilo katika kufanya usafi katika eneo ambalo linatoa huduma za afya kwa wananchi.
Mwaipaya alisema maeneo ya kutolea huduma za afya yanapokuwa na mazingira salama yanasaidia kuepusha kuwepo kwa maambukizi mbalimbali ya magonjwa yasiyakuambukiza kwa wananchi wanaofika katika kupata huduma za kimatibabu.
Alisema wilaya ya Mwanga inazo kata 20 na kati ya hizo kata 16 zote zina polisi jamii na kwamba uwepo wa askari hao, umesaidia kupunguza changamoto za wananchi hao kusafiri kwenda katika kituo kikuu kupeleka mashauri mbalimbali.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mwirange Dkt. Yosya Foya, alisema kwenye kituo hicho wagonjwa wengi wanaofika kwa ajili ya kupatiwa matibabu wengi wao wanasumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu, kuharisha na malaria.
Akizungumza Dkt. Afath Mohamed na Dkt. Joyce Kangero, walisema changamoto ya maradhi ambayo wakazi wa wilaya ya Mwanga wamekuwa wakiugua na kuletwac katika kituo hicho cha afya yanaweza kuzuilika endapo watazingatia zaidi elimu ya afya ambayo imekuwa ikitolewa na wataalamu hao wa afya.
Zoezi la usafi wa mazingira hufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa
kila mwezi ambapo Januari 28 mwaka huu Jeshi la Polis8i Mwanga kwa kusirikiana
na uongozi wa serikali ya wilaya na uongozi wa kituo cha afya Mwirange
wameshiriki kufanya usafi katika kituo hicho.
Tuesday, January 24, 2023
PICHA: Namna Chifu Mwariko alivyopumzishwa katika makaburi ya Manyema mjini Moshi
CHIFU ATHUMAN Omary MWARIKO “Mhelamwa” :Huyu ni yule aliomba noti ya Tanzania ichapishwe picha ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli, pia ndiye huyu aliomba mlima Kilimanjaro ufunikwe pazia, ndiye huyu aliandaa kinyago na kumpelekea Rais wa Urusi Vladmir Putin kwa ajili ya kufanikisha Kombe la Dunia 2018.
Chifu Mwariko is no more
Chifu Athuman Mwariko enzi za uhai wake |
Mwili wa marehemu Chifu Mwariko ukiwa katika jeneza kuelekea makaburini Manyema, Moshi Mjini |
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa ya Kilimanjaro Cultural Heritage Centre ya mkoani Kilimanjaro, Chifu Athuman Omari Mwariko amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Taarifa za familia ya Chifu Mwariko zinasema alifariki dunia
alfajiri ya Januari 22,2023 nyumbani kwake Maili Sita, na kuzikwa Jumatatu ya Januari 23,2023; saa 12 jioni.
Familia yake ilisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na
ugonjwa wa moyo ambapo siku chache kabla ya kifo chake alidai kuishiwa nguvu
hadi umauti ukamkuta.
Chifu Mwariko aliwahi kufanya kazi na Hayati baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere pia Malkia Elizabeth II wa Uingereza.
Mwishoni mwa mwaka 2022 alimkabidhi Kifimbo Chifu Frank Marealle,
mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) na Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo.
TAARIFA ZILIZOPITA ZA CHIFU MWARIKO
BONYEZA LINKI HIZI
https://jaizmelanews.blogspot.com/2020/07/wizara-ya-fedha-yashauriwa-kuchapisha.html
https://jaizmelanews.blogspot.com/2020/11/mhelamwana-amkabidhi-kifimbo-mbunge.html
https://jaizmelanews.blogspot.com/2021/08/chifu-mwariko-ataka-chanjo-ya-uviko-19.html
https://jaizmelanews.blogspot.com/2022/06/kilimanjaro-cultural-heritage-centre.html
https://jaizmelanews.blogspot.com/2022/07/wasanii-wa-kilimanjaro-waishio-dar.html
https://jaizmelanews.blogspot.com/2022/10/chifu-marealle-akabidhi-madaraka-aonya.html
https://www.youtube.com/watch?v=8REybEtLY-4
https://www.facebook.com/johnson.jabir.735/videos/294583529107769
UVCCM Moshi Mjini yapanda miche 3,000
UVCCM Moshi Mjini wakiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge katika zoezi la upandaji wa miti kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. |
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Moshi Mjini umewataka Vijana wa Jumuiya hiyo kusimamia misingi ya jumuiya hiyo kwani ndiyo nguzo kuu ya chama inayozalisha viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.
Akizungumza katika zoezi la upandaji miti ya matunda
katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo kata ya Kiusa Januari 24,2022 Mwenyekiti
wa jumuiya hiyo Sadath Sudi Ndibalema alisema UVCCM ni nguzo kuu inayopaswa
kuzingatiwa katika mustakabali wa taifa hivyo vijana walioko ndani ya chama
kuhakikisha kwamba wanaendelea kusimamia misingi hiyo.
Chama cha Mapinduzi kuliundwa Februari 5,1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.
Azma ya zoezi la uoteshaji wa miche ya miti katika shule
hiyo, Ndibalema alisema lengo ni kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi sambamba na wanafunzi kupata lishe ya wanafunzi hao.
Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge Hellena John alisema,
shule hiyo ilikuwa na uhitaji mkubwa wa miche ya miti ya matunda na kuipongeza
Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwakuweza kuwapatia miche hiyo.
Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge Bi. Hellen John |
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Moshi mjini Arafati Mbiruka alisema Jumuiya hiyo ya Vijana wameamua kuotesha miti ya matunda katika shule ya msingi Mwenge ili kuboresha mazingira ya shule hiyo sanjari na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kupata matunda lishe ili kuboresha afya zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kiusa, Khalid Shekoloa aliishukuru Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa UVCCM Manispaa ya Moshi kwa kuwezakupanda miti ya matunda katika shule hiyo kwani itakwenda kusaidia utatuzi wa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi sanjari na kuwaomba wanafunzi wa shule hiyo kuendelea kuitunza
Aidha Shekoloa amewataka kupanda miti kwa wingi itakayosaidia utunzaji wa mazingira ili kwenda sambamba na mpango wa Serikali wa upandaji miti ili kuzuia athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Sadath Ndibalema, mwenyekiti wa UVCCM Moshi Mjini |
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Moshi Mjini
kutoka kundi la Vijana Ashiraf Baraka
Malya, walisema bado kuna changamoto ya uelewa kwa jamii juu ya upandaji wa
miti na utunzaji wa mazingira.
“Upandaji miti ulioendeshwa na UVCCM Wilaya ya Moshi
Mjini katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM, itakwenda kuboresha
mazingira ya shule huku akitoa wito kwa wanafunzi hao kuitunzana kuilinda ili
kuwana mazingira yaliyo salama,”alisema Malya.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge mjini Moshi wakiwa na miche ya miti |
Zoezi la upandaji wa miti ni ikiwa ni maandalizi ya
kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM. Chama cha Mapinduzi kuliundwa Februari
5,1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union
(TANU) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.
Wednesday, January 11, 2023
UVCCM Moshi Mjini yamjia juu Juma Raibu
Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Moshi Mjini umemjia juu aliyetimuliwa Umeya wa
Manispaa Juma Raibu kuacha kukikosoa chama chake hadharani hususani katika
mitandao ya kijamii na badala yake kupeleka changamoto hizo kwa kufuata
utaratibu wa chama.
Akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya CCM
wilaya ya Moshi Mjini, Mwenyekiti wa Sadath
Sudi Ndibalemwa, alisema wako baadhi ya watu wachache ambao ni wana chama,
baada ya kushindwa kuchaguliwa kwenye nafasi walizokuwa wameziomba kwenye
chaguzi zilizomalizika hivi karibuni ndani ya chama hicho, wameunda kikundi cha
kuanza kukichafua chama na viongozi wake
kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Licha ya Ndibalemwa kutomtaja
moja kwa moja Juma Raibu lakini mitandao ya kijamii ya aliyekuwa Meya wa
Manispaa hiyo na Diwani wa kataya Bomambuzi
ameonyesha ukosoaji mkubwa wa chama hususani baada ya Mwenyekiti wa CCM Taifa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kutangaza kuanza kwa
mikutano ya hadhara kwa vyama vyote vya siasa nchini baada ya kuzuiwa enzi za
utawala wa Dkt.John Pombe Magufuli.
Sadath Sudi Ndibalemwa,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya wa Moshi Mjini
Katika akaunti ya Juma Raibu katika Instagram mnamo Januari 9,2023 aliandika, “Nemesikitishwa sana na baadhi viongozi wa chama changu mkoa na wachache wilaya na baadhi ya wanachama, kulaumu kuhusu Mh Rais Samia Kuruhusu mikutano ya hadhara, hakika huu ni udhaifu mkubwa sana na nikukimbia majukumu walioomba kwa Kuzoea kulala usingizi hakuna ushindi bila jasho…”
Juma Raibu anayefahamika kama ‘Man
of the People’ yaani mtu wa Watu aliongeza katika utoaji wake wa maoni katika Instagram
kuwa, “Twendeni kwa wananchi kusema yanayofanywa na CCM yetu na sio kuogopa
mikutano tujipime kwa nguvu zetu Na sio kubebwa " hongera Mama Samia…tukutane
Kazini”
Katika kuunga mkono juhudi zake
Juma Raibu, wafuasi wake nao wameendelea kutoa maoni yao huku wakimtaka kukaza
kamba zaidi
“Hao viongozi wa CCM
wanaolalamika kwa nini mama karuhusu mikutano ingekuwa bora wangejiondoa kwenye
nafasi zao, wawapishe watu wanaoweza kukisemea Chama. Viongozi dizaini hiyo ni
wale waliozoea : " MSEREREKO " !!!!., Wana haja gani ya kuwa kwenye
nafasi zao? waache uvivu walishazoea kulala usingizi. waamke...”alisema mfuasi
aliyejitambulisha kwa jinala Job Faustine.
Viongozi wengine wa CCM waliojibu
hoja za Juma Raibu ni Mrindoko Mwidadi ambaye ni Mwenyekiti wa Juumuiya ya Wazazi
Tanzania mkoa wa Kilimanjaro alisema, “Viongozi gani wa Mkoa na Wilaya kwani
tupo Mkoani?? pima maneno ya kuandika na kusema kwani ukiambiwa uthibitishe
hili usije sema unaonewa!”
Kwa upande wake Mjumbe wa
Halmashauri Kuu CCM (W) Moshi Mjini, Issa Bulilo alisema, “Hii sio sawa mkuu
Viongozi wa Chama ngazi ya Mkoa na Wilaya wamelalamika wapi kufuatia Mh Rais
kuruhusu mikutano??
Mnamo Januari 3,2023 Rais Samia
aliruhusu mikutano ya vyama vya siasa baada ya marufuku ya miaka zaidi ya 6
iliyowekwa na mtangulizi wake, hayati John Magufuli.