Tuesday, December 20, 2016

‘Rushwa ya ngono sasa basi’

NA JEMAH MAKAMBA
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Chalinze Anthony Nyange (aliyesimama) akizungumza katika semina hiyo

JAMII imetakiwa kuungana na taasisi zisizo za kiserikali katika vita dhidi ya rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi ili kuiweka nchi katika nafasi nzuri kimaendeleo.
Akizungumza katika semina ya uwezeshaji iliyofanyika Miono wilayani Chalinze, Pwani hivi karibuni Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo Anthony Nyange alisema rushwa ya ngono imesababisha madhara makubwa katika jamii.
“Rushwa ya Ngono imekuwa sugu nchini kutokana ugumu uliopo katika kumgundua mhusika, bila nguvu ya jamii pamoja na NGO’s hizi vita hii itakuwa ngumu kuikabili na itawatafuna watoto wetu hususani wa kike,” alisema Nyange.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa na na Shirika la Maendeleo ya Wajasiriamali Miono (SHIMAWAMI) kwa msaada wa Women Fund Tanzania (WFT), Nyange aliweka bayana kuwa taasisi zinazoendesha harakati mbalimbali za kimaendeleo ni muhimu kwani zinaikumbusha serikali ulazima wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Nyange alisisitiza kuwa umaridadi umekuwa ukitumiwa na wengi kutenda maovu kutokana na uvivu miongoni mwa wanawake, tamaa, ukosefu wa sifa kwenye ajira na uwezo wa kifedha.

Hata hivyo Nyange aliwakumbusha washiriki akali wa 65 wa SHIMAWAMI kuwa utafiti  umeonyesha wanawake na wasichana wengi wamekuwa wakikosa sifa katika maeneo ya kazi lakini wameendelea na kazi kutokana na mahusiano ya kimapenzi na mabosi wao.








0 Comments:

Post a Comment