NA
MWANDISHI WETU
John Guninita |
Katika mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa wilaya hiyo Bernard Mwakyembe walihudhuria Mbunge wa Viti Maalum jimbo la Temeke Lucy Magereri, Afisa Kanda ya Pwani kwa tiketi ya chama hicho Christopher Mbusule Shiru
Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo Chang’ombe jijini Dar es Salaam kiongozi huyo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema mapato na matumizi katika chama ni sehemu nyeti ambayo isipowekewa utaratibu mzuri huibua migogoro isiyo na sababu.
Aidha Guninita alisisitiza serikali ya Rais John Magufuli (JPM), imejaa woga, kiburi na majivuno yasiyo na msingi wowote katika maendeleo ya nchi hii.
“Mimi ni mwanasiasa wa siku nyingi…viburi, majibu ya hovyo hovyo, hiyo ndiyo CCM ya sasa. Rais ni kama mpiga ngoma anapiga mwenyewe na kutaka kucheza mwenyewe… Haiwezekani,” alisema Guninita.
Pia aliongeza tatizo kubwa la watanzania namba moja ni maji na kwamba Rais anaogopa kukosolewa juu ya hilo.
“Rais mzuri ni yule anayewaruhusu wananchi wake wamkosoe, sio yule anayefanya tathmini kwa mwaka mmoja…hatujaona mabadiliko kwa Magufuli,” alisema Guninita.
Kwa upande wake Magereri alisema Operesheni Amsha Chama inakuja na itaendeshwa nchi nzima kuelekea 2020 na kuongeza kadi mpya za kielektroniki kwa wanachama zitaanza kupatikana mwaka ujao.
Aidha Afisa wa Kanda ya Pwani aliwataka wanachama wasitishike na vitisho vya serikali iliyopo sasa isipokuwa sauti ya pamoja itatwatoa katika konga hilo.
Pia aliwataka wanasheria wa chama kupita katika kata na kuwaeleza na kutolea ufafanuzi wa katiba ya chama chao ili kuongeza na kukuza uelewa wa mwongozo huo hali itakayoondoa sintofahamu.
Kata 13 za wilaya ya Temeke zilihudhuria mkutano huo hivyo kutimiza akidi kwa mujibu wa Sura ya sita (6.2), ya katiba ya chama hicho
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lucy Magereri akizungumza jambo katika
Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
|
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lucy Magereri akizungumza jambo katika
Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
|
0 Comments:
Post a Comment