Wednesday, December 28, 2016

Dk. Guydon Makulila na salamu za Mwaka Mpya 2017

ZIMEBAKI siku chache kumaliza majuma 52 ya mwaka 2016. Katika mwaka huu kuna mengi yametokea ya kuudhi, kuhuzunisha na kufurahisha. Licha ya changamoto zote bado kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitambua kuwa hayo yote ni maisha.
Dk. Guydon Makulila

Kwani maisha ni mchanganyiko wa vipindi vyote vya kila siku katika maisha ya binadamu. Inapokuwa siku zote ni furaha tu hayo sio maisha, ikiwa ni kulia tu bila kingine hayo sio maisha.
Jaizmelaleo imepata bahati ya kuzungumza na Dk. Guydon Makulila ambaye ni mtaalamu wa mtaalam wa kutoa dawa za usingizi katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya kuhusu masuala mbalimbali.
Dk. Makulila (kushoto) akiwa na wahandisi kutoka Kasmedics Ltd baada ya kufunga mashine ijulikanayo kwa jina la Universal Anaestjeaia (UAM), katika kuhakikisha wagonjwa wa upasuaji wanapata huduma bora na ya usalama.
Miongoni mwa mambo aliyoyasema ni kuhusu matarajio yake mwaka 2017 katika medani yake ya utabibu.
“Matarajio yangu kwa mwaka 2017 ni kuongeza ufanisi katika kazi yangu ili wagonjwa wote ninaowahudumia wapate kurudi katika hali yao ya kawaida,” alisema Dk. Makulila
Aidha Dk. Makulila alifunga kwa kuiasa jamii ya Watanzania ambao baadhi yao wamekuwa na tabia ya kujinunulia dawa pasipo kupimwa.
“Pia naiasa jamii kuwa na hali ya kuwahi katika vituo vya tiba ili kupata matibabu ya uhakika na sio kujitibia wenyewe kama ilivyo kwa sasa wananchi wengi wanaojinunulia dawa katika maduka ya madawa pasipo kupimwa,” alihitimisha Dk. Makulila.
Kwa ufupi Dk. Makulila ni baba wa watoto watatu (Kefa, Samweli na Guydon) na mke mmoja mwenye uzoefu wa kimataifa katika fani ya udaktari ambapo amekuwa akichukua kozi na mazoezi mbalimbali ya kuongeza ufanisi wake ndani na nje ya nchi.
Familia ya Dk. Makulila



0 Comments:

Post a Comment