Mangi Gilbert Shangali anayetarajiwa kusimikwa Desemba 14, 2024 katika kijiji cha Wari, wilayni Hai mkoani Kilimanjaro. (Picha Na. MAKTABA)
Desemba 14, 2024 itakuwa siku nyingine muhimu katika Historia ya Wenyeji wa Machame wilyani Hai mkoani Kilimanjaro ambako kutashuhudiwa hafla ya kumsimika Mangi wa 52 wa Wamachame Gilbert Shangali.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Clement Andrea Shangali, aliyasema hayo Desemba 9,2024 mjini Moshi, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuwa Chifu Frank Marealle ataambatana na machifu wengine, kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, mkuu wa Wilaya ya Moshi James Kaji, pamoja na Viongozi wa madhehebu ya kidini.
Aidha alisema, maandalizi ya kumsimika yameshakamilika na kwamba tukio hilo litaanza majira ya saa tatu asubuhi, huku akitoa wito kwa wananchi kuhudhuria kwa wingi kushuhudia tukio la kusimikwa kwa Mangi mpya wa Machame.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ukoo Dk. Harold Shangali, alisema kuteuliwa kwa Gilbert Shangali, kuwa Mangi wa WanaMachame, anayo nafasi kuwa ya kuhakikisha kwamba anakwenda kusimamia maadili ambayo kwa kiasi kikubwa yameporomoka katika jamii.
Aidha alisema machifu wana mchango mkubwa katika kulinda maadili na kutatua changamoto za kimaadili katika jamii licha ya kuwa yanashughulikiwa katika ngazi ya Serikali.
Naye Katibu wa Umoja wa Machifu mkoa wa Kilimanjaro Joseph Mselle, alisema Afrika ilikuwa na mfumo wake wa utawala, uliokuwa unarithishwa kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Akizungumzia tawala za jadi katika nchi ya Tanzania Mselle, alisema ni alama ya mfumo wa kiuongozi kwa Waafrika kabla ya ukoloni kitu ambacho ndicho kilikuwa ni kielelezo cha kutambulisha tamaduni zetu.
Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) Frank Mareallle, anatahahudhuria tukio la kusimikwa kwa Mangi mkuu wa Machame Gilbert Shangali, litakalofanyika, kijiji cha Machame Wari, Wilaya ya Hai mkoani humo.
0 Comments:
Post a Comment