Kanisa la Africa Mission Evangelism (AMEC) limemsimika rasmi
Paul Assey kuwa mchungaji wa Usharika wa Kileo, jimbo la Kilimanjaro katika
hafla iliyofanyika katika usharika wa Kileo wilayani Mwanga.
Hafla hiyo ya kumsimika Mchungaji Assey ilifanywa na Askofu
Mkuu wa AMEC Tanzania Baltazar Kaaya ilienda sambamba na Ibada ya Jumapili na
Uimbaji kutoka kwaya ya Mtiini Mungu
AMEC-Ulshoro ya Arusha.
Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Mchungaji Wilson Kawiche alikuwa
miongoni mwa watumishi wa Mungu walioongoza ibada hiyo ambayo iliwaleta pamoja
Wakristo wa madhehebu hayo nchini
Hafla hiyo ilianza kwa utaratibu wa kanisa, kuwasimika
watumishi wake ambapo Wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo, walimzunguka
Mchungaji Assey na kuanza kusoma Neno la Mungu mmoja baada ya mwingine.
Hatua iliyofuata ilikuwa ni kukiri kwa kinywa chake, kiapo
cha kulitumikia Kanisa la Mungu kwa uaminifu wote hata ukamilifu wa dahali.
Mchungaji Assey na viongozi wakuu wa Kanisa hilo akiwamo Askofu
Mkuu wa AMEC Tanzania Baltazar Kaaya walisaini kiapo hicho muhimu tayari kwa
kuanza rasmi kazi ya Mungu katika Parokia ya Kileo.
Awali akizungumza kabla ya hafla ya kumwingiza kazini
Mchungaji Assey, Mchungaji Judah kutoka Amec Arusha alisema ni furaha kuu ku
Katika ibada hiyo Mchungaji Judah alipata nafasi ya kutoa
neon la Mungu kwa waliohudhuria ibada hiyo wakiwamo ndugu jamaa na marafiki.
Aidha ujumbe kutoka Kanisa la Furaha Tanzania ukiongozwa na
Askofu Jones Mollah ulitolewa katika ibada hiyo
Katika hafla hiyo ulienda sanjari na kuwarudisha hemani mwa
Bwana waumini walioamua kurudi tena kumtumikia Mungu katika kanisa hilo.
Nasaha zilitolewa kwa waliorudi hemani mwaka Bwana huku
wakisisitizwa kuvumilia hila za Shetani za kutaka kuwarudisha nyuma.
Aidha Mkuu wa Jimbo la Arusha Mchungaji Elidaima Mushi alitoa
nasaha kwa Mama Mchungaji Assey namna ya kumtunza Mchungaji Assey ili aweze
kuifanya kazi ya Mungu kwa ukamilifu wote,
Ndugu, Jamaa na Marafiki walipata fursa ya kutoa shukrani zao
kwa tukio hilo muhimu katika maisha yao, ambapo Kaka wa Mchungaji Assey alitoa
shukrani za dhati kwa niaba ya kundi hilo.
Kuwasimika wachungaji kuanza kazi ya Mungu ni kitendo cha
kanisa kumtambulisha na kumwezesha mchungaji kuingia katika jukumu rasmi la
kuongoza na kutunza kundi la waumini. Hii ni hatua muhimu katika huduma ya
kiroho ambapo mchungaji anapewa mamlaka
na wajibu wa kuhubiri Neno la Mungu, kuongoza ibada, kufanya huduma za kiroho
kama vile ubatizo, ndoa na mazishi na
pia kutunza na kulinda mwanzo wa Imani ya waumini.
AMEC inaundwa na takribani makusanyiko 100 ya Wakristo wa
Kilutheri katika eneo la Kaskazini mwa Tanzania. Limesambaa zaidi katika eneo
la chini ya Mlima Meru mkoani Arusha na sasa linaendelea kuongezeka kuzunguka
Mlima Kilimanjaro na tambarare kuelekea Upareni.
Credit to: Jabir Johnson, +255 693 710 200 jabirjohnson2020@gmail.com
0 Comments:
Post a Comment