Mnamo mwaka 2022,aliyewahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania 2000, Rashida Wanjara na wenzake 13 waliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuwasamehe huku wakiahidi kubadili tabia zao ndani ya miaka miwili.
Washtakiwa wengine walikuwa ni Masha Ngubi maarufu Masha love, Zena Abdallah maarufu kwa jina la Jike shupa, Rhodie Webb, Hawa Anthony, Lydia Mlelwa, Malkia Hashim, Latifa Idd, Mariam Bakari, Hadija Said, Mariam Idd, Nasra Kondo, Irene John na Joyce Matulanga
Wanjara na wenzake hao walikamatwa na Polisi na kufikishwa mahakamani kwa kufanya vitendo vya udhalilishaji hadharani ikiwa pamoja na kucheza ngoma za kigodoro, kibao kata na kutumia chupa na tunda aina la tango kuingiza sehemu za siri.
Juni 8, 2022; Washtakiwa hao akiwamo Masha Love walifikia uamuzi huo, baada ya Jamhuri kuwasilisha maombi mahakamani hapo ya kuwataka washtakiwa hao waahidi kuwa watabadilika na kuwa na tabia njema.
Akitoa uamuzi wa maombi hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo aliwataka washtakiwa hao kutokufanya makosa yoyote ya kimaadili kwa kipindi cha miaka miwili yaani mpaka mwaka 2024 na watatakiwa kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jina Kanda (ZCO ).
“Kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh. 5 milioni na pia wawe na nidhamu na tabia njema katika jamii," alisema Tarimo
Sasa basi tarehe 25 Novemba 2024; Masha Love akiwa na Moseiyobo ambaye ni mpenzi wake walijisalimisha kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) kutokana na msako dhidi ya watu wenye ushawishi katika mitandao ya kijamii wanaozalisha maudhui yasiyokuwa na maadili mema ya Kitanzania.
Masha alifika ofisini kwa Waziri akiwa na Mwenza wake, Moses Iyobo, kwa ajili ya kujibu tuhuma za maudhui yanayokiuka maadili ya Kitanzania anayopakia kwenye mitandao yake ya kijamii.
Baada ya mazungumzo marefu katika kikao hicho na Waziri Dkt. Gwajima, Mashalove amekiri makosa yake na kuomba radhi na kuahidi kuacha mara moja na kuendelea kuboresha kazi zake kwa mujibu wa Sheria.
Aidha Dkt. Gwajima alimuonya Mashalove na kumtaka kutokurudia tena kuzalisha maudhui yanayokinzana na maadili ya kitanzania na badala yake azingatie Sheria na miongozo ya kutumia mitandao ya kijamii kwani, kinyume na hapo anakuwa anautweza utu wa mwanamke na pia kukwaza wengine
“Hata kama unajipatia kipato kwa njia ya mitandao ya kijamii na isiwe kwa maudhui yanayoenda Kinyume na Maadili ya Nchi na Jamii zetu, Masha uwe Balozi wa kukemea haya” alisema Dkt. Gwajima.
Naye Mashalove alimuahidi Dkt. Gwajima kutoa ushirikiano na kusema atakuwa Balozi mwema katika kubadilisha wengine, na yeye binafsi ameshabadilika sana tangu alipopewa onyo la kwanza na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ila wapo watu wanaopakia kazi zake za zamani na kumchonganisha na Serikali.
Waziri Gwajima, alimpongeza Mashalove kwa kukata shauri kubadilika na kuzingatia kulinda maadili kwenye kazi zake.
Aidha, Waziri Dkt. Gwajima alitoa wito kwa wananchi kuwatia moyo watumiaji wa mitandao wanaokata shauri kubadilika na kuunga mkono kulinda maadili na ameahidi kuandaa na kuratibu semina ya wanawake wenye wafuasi wengi na ushawishi Mitandaoni
Jambo la kuzingatia katika sakata hili la Masha Love; Kutunza maadili ya Mtanzania kuna faida nyingi, kwa sababu maadili ni msingi wa utamaduni, umoja, na maendeleo ya jamii.
Kunaimarisha Umoja na Mshikamano,Kuheshimu Haki na Heshima kwa Wengine, Kukuza Uadilifu na Haki, Kukuza Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii, Kuongeza Matarajio ya Kesho Bora, Kujenga Heshima ya Taifa Kimataifa, Kuimarisha Familia na Jamii, Kupunguza Uhalifu na Uasi.
Kwa ujumla, kutunza maadili ya Mtanzania ni muhimu katika kujenga jamii yenye umoja, maendeleo, na mafanikio, huku pia ikilinda na kukuza tamaduni na desturi nzuri za taifa letu.
Credit to: Jabir Johnson; jabirjohnson2020@gmail.com; +255 693 710 200
0 Comments:
Post a Comment