Monday, December 9, 2024

Mangi Gilbert Gilead Shangali ni nani?

Chifu mteule Gilbert Gilead Shangali ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa Mangi (Gilead Abdiel Shangali) na ni Mjukuu wa Mwitori Abdeil Shangali na ni Kitukuu cha  Mangi Shangali Ndeserua

Chifu mteule Gilbert Shangali, alizaliwa Machame mwaka 1973,baadaye alijiunga na masomo ya shule ya msingi  Machame kuanzia mwaka 1980 hadi 1987.  Shule ya sekondari (O-Level) Mwaka 1988 hadi 1992,na shule ya sekondari ya Siha (A-Level) mwaka   1993 hadi 1995.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari ,alijiunga na Chuo cha Oshwal  Nairobi nchini Kenya, kuanzia mwaka 1996 hadi 1999. Ambapo alihitimu masomo yake na kuwa na Taaluma ya Uongozi na Utawala.

0 Comments:

Post a Comment