Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Friday, July 19, 2024

New Lumumba Food Restaurant yazinduliwa mjini Moshi

 

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Zephania Sumaye akikata utepe katika uzinduzi wa New Lumumba Food Restaurant kwenye hafla iliyofanyika mjini Moshi mnamo Julai 19, 2024 katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Moshi Mjini; kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Moshi Mjini Frida Kaaya, Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Faraj Swai na Mkurugenzi wa mgahawa huo Athuman Ally Mfutu. (Picha na JAIZMELA/credited to: Jabir Johnson)

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za ujasiriamali, ikiwemo kuwapatia fursa za kiuchumi hatua ambayo inadhihirisha ukuaji wa uchumi.

Hatua muhimu ya uzinduzi wa New Lumumba Restaurant, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro chini ya mkurugenzi wake Athuman Ally Mfutu inadhihirisha namna CCM kinavyotoa fursa kwa vijana wake waliopo ndani ya chama hicho kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwamo biashara.

New Lumumba Restaurant imeanza kwa kasi mpya baada ya uzinduzi wake wa nguvu ambao umetiwa chachu na viongozi wa chama hicho na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Zephania Sumaye amekata utepe wa kuacha kwa utoaji wa huduma ya chakula na vinywaji wa mgahawa huo.

Akizungumza na wageni waalikwa wa hafla hiyo fupi mnamo Julai 19, 2024 katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Moshi Mjini DC Sumaye Mkuu amesema nia njema ya taifa kwa ujumla katika suala la maendeleondio chachu kubwa ya kuruhusu uwekezaji wa ndani pale wanapokidhi vigezo.

“CCM kwa nia njema kabisa yenye kuleta maendeleo ya nchi na watu wake imetoa fursa za uwekezaji kupitia chama hicho, ni vyema watu wakachangamkia fursa hizo ili waweze kukuza vipato vyao na hata kipato cha taifa kupitia kodi mbalimbali”, alisema DC Sumaye.


Aidha Mkuu huyo wa Wilaya, alimpongeza Mwekezaji aliyefungua Mgahawa huo Athuman Ally Mfutu, ambapo amesema Serikali itaendelea kushirikiana naye pamoja na wawekezaji wengine katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana Wilayani humo.


Akiongea katika hafla hiyo Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Moshi Stuwart Nathael, amesema uwekezaji huo utasaidia kukuza uchumi wa Manispaa ya Moshi kupitia njia mbalimbali kutokana na kukua kwa mzunguko wa fedha.


 “Tatizo kubwa katika nchi yetu ni ukosefu wa ajira, inapotokea kijana anaamua kuwa Mwekezaji Serikali itamuunga mkono kwa kuwa atachangia kukua kwa uchumi”, amesema Nathael.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Mjini Faraji Swai, amesema chama Wilayani humo, kitaendelea kushirikiana na Wawekezaji mbalimbali ili kuongeza fursa za uwekezaji Wilayani Moshi.


“Moja wapo ya yale yaliyomo ndani ya ilani ya CCM ni kwa serikali kutengeneza fursa za ajira; hili ndilo lililopelekea uongozi wa CCM wilaya kuja na wazo la kutafuta mwekezaji ambaye uwekezaji wake pia umebadilisha madhari ya ofisi kuwa nzuri”, amesema.


Awali akizungumza Mkurugenzi wa New Lumumba Food Restaurant Athuman Ally, amekishukuru Chama kwa kumpa ushirikiano katika uwekezaji alioufanya, ambapo amesema umetoa ajira kwa zaidi ya 15 wengi wao wakiwa ni vijana.



















 

Unafahamu kuwa Kiti unachokalia ofisini kinaongeza morali ya kufanya kazi?


Shirika la AJISO limetekeleza mradi wa Uraia Wetu unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Foundation for Civil Society (FCS) mnamo Julai 17, 2024 baada ya kuendesha Mdahalo uliojumuisha wakurugenzi wa mashirika ya Kanda ya Kaskazini na Viongozi wa serikali kutoka Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara uliokuwa na malengo ya kuimarisha ushirikiano  katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo na kuimarisha utawala bora.

 

Thursday, July 18, 2024

Kutumia Takwimu zisizo sahihi ni kosa kisheria

 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu inathamini maoni yako kuhusu bidhaa na huduma za kitakwimu na zisizo za takwimu inazozitoa. Maoni yako yatashughulikiwa kwa usiri wa hali ya juu na kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa pekee. Tafadhali toa maoni yako kupitia simu, barua pepe, sanduku la maoni, tovuti au kwa kutembelea Makao Mkuu ya NBS na Ofisi zetu za Takwimu za Mikoa zinazopatikana katika kila makao makuu ya mkoa.












Changamoto ya Maji Yamu Makaa yazua tafrani

 


Yapi ni maji safi na salamaMaji safi na salama ni maji yasiyokuwa na uchafu, yasiyo na harufu mbaya na yasiyo na vidudu. Maji safi na salama huleta afya njema na maji yasiyo safi na salama huleta madhara kwa binadamu kama vile kuhara na kuhara damu.












Monday, July 15, 2024

Jaribio la Donald Trump lina maana gani katika siasa za Marekani?

 

Jumamosi ya Julai 14, 2024 nchini Marekani haikuwa siku njema kwa Rais wa zamani wa Taifa hilo Donald Trump baada ya jaribio ;la kutaka kumwua kushindikana. Risasi moja ilijeruhi sikio la kiongozi huyo alipokuwa jimboni Pennsylvania. 

Je, ni Rais pekee wa Marekani kunusurika kuuawa tangu enzi za ABRAHAM LINCOLN mnamo Aprili 14, 1865...Jibu ni la hasha! Wengine hao ni kina nani?

Friday, July 12, 2024

Irmegolik ni nini?

 

Wamaasai ni kabila linalotambulika kama mashujaa wa kuua Simba ili uonekane kidume cha mbegu. 

Kabila ambalo kabla ya kujigeuza kuwa walinzi na wasusi mjini kila mtu alikuwa akiowagopa kutokana na tabia zao za kutembea na fimbo pamoja na sime kiunoni, sana sana Kwa viana wao wa kimorani. 

Sijawahi sikia au kusoma popote pale kama waliwahi kupambana wakati wa ukoloni kama ilivyo kwa baadhi ya makabila mengine mfano, wahehe na Chifu mkwawa wao. 

Hili kabila la Wamasai kuna historia yeyote kweli inayowahusu ya wakati wa ukoloni kama ipo naomba niambiwe ili niwajue vyema.