Wafanyabiashara wa Matunda katika soko la Korongoni. |
Wakala wa Vipimo mkoa wa Kilimanjaro (WMA) imeaonywa wafanayabiashara wanaokiuka sheria ya vipimo wakati wanaponunua mazao kutoka kwa wakulima.
Hayo yamejiri katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo
duniani ambayo mwaka huu inaenda sanjari na kauli mbiu isemayo, “Umuhimu wa
Vipimo katika kuwezesha mifumo ya usafirishaji chakula duniani.”
Akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Korongoni lililopo Manispaa ya Moshi mkoani humo Meneja
wa Vipimo mkoani Kilimanjaro Salum Masinde amesema, Sasa hivi kuna
mabadiliko ya tabianchi, ishu ya kivipimo katika usafirishaji wa chakula
duniani ni muhimu sana, ndiyo maana dunia yote leo inaenda na kauli mbiu hiyo.”
Aidha
Masinde amesema kuadhimisha siku hiyo katika Soko la Korongoni kumekuja kutokana
na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kukiuka sheria za vipimo huku wakiwalaghai
“Kwa wafanyabiashara
wa matunda ya parachichi, yanayosafirishwa kutoka Moshi kuelekea Tanga na Dar
es salaam yanayotoka kwa wakulima kuletwa hapa sokoni, lazima kuwe na usawa wa
kibiashara na haki kwa wakulima, wakulima wasije wakanunuliwa lumbesa kwa kufisiliwa
kuwa gunia ni zaidi ya kilo 100,” amesema Masinde.
Masinde amesema
wanaiadhimisha siku hii kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wakulima wote wa
mkoa wa Kilimanjaro kutokana wengine kukosa elimu ya masuala ya vipimo.
“Kuna wengi wafanyabiashara
ndiyo mara yao ya kwanza kuleta mizigo sokoni labda hawakuwa na elimu hiyo huko
nyuma leo wamepata nafasi ya kupata elimu ya ufungashaji mazao na tafsili ya
gunia ni kitu gani ili kumlinda mkulima na kuwalinda wafanyabiashara wanaonunua
mazo kutoka kwa mkulima,” ameongeza Meneja huyo.
Afisa vipimo
mwandamizi mkoa wa Kilimanjaro, Meshack Edward ameongeza kuwa watu wanazidi
kuongezeka duniani huku mabadiliko ya hali ya tabianchi yakizidi, hivyo Wakala
wa vipimo wametoa elimu hiyi kwa wafabnyabiashara wa vyakula vilivyo katika
vipimo sahihi ili kuweza kuwa na akiba ya chakula .
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Soko la Parachichi Korongoni Athuman
Mkony ameushukuru uongozi wa
Wakala wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro, kwa kuadhimishia siku hiyo katika soko la
Parachichi Korongoni kwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo, ili kuweza
kushirikiana na wakala hao bila kupata changamoto yoyote wawapo barabarani.
“Sisi wafanyabiashara
wa Parachichi tunashukuru kwa kupatiwa elimu hiyo na kuendelea kuwaelimisha
wenzetu ambao hawakuwepo katika elimu hiyo.
Mfanyabiashara wa
parachichi Hilda Moshi na Ally Mmbwambo; wamesema baadhi ya wafanyabiashara
wa zao la parachichi walikuwa hawana uelewa na masuala ya vipimo kutokana na
zao hilo kuwa jipya lakini baada ya kupata elimu hiyo watakuwa mabalozi wazuri
katika utumiaji wa vipimo .
Pia Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa matunda Mkoa wa Kilimanjaro Cosmas
Mushi amesisitiza kuwa wafanyabiashara
wengi wa matunda walikuwa wakiifanya bila ya vipimo, kwa elimu ambayo imetolewa
na wakala wa vipimo itasaidia na kuwaomba wazidi kuendelea kutoa elimu zaidi
kwa wafanyabiashara wa matunda.
Mei 20, 1875 mataifa
17 ulimwenguni, yalikutana na kukubaliana ufanano wa kivipimo uwepo duniani ili
biashara iweze kufanyika.
0 Comments:
Post a Comment