Ubunifu mara nyingi huchukuliwa kuwa ni matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika, hivi ndivyo unavyoweza kusema kwa Halmashauri ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Halmashauri hiyo iliyopo mikononi mwa Mkurugenzi Mtendaji Mwajuma Nasombe imefanikiwa kununua gari la kusambaza madini ya ujenzi (mchanga) ikiwa ni ubunifu baada ya kukusanya asilimia 50 ya mapato kutokana na ukusanyaji wa mchanga.
Akizungumza katika uzinduzi wa gari hilo uliofanyika tarehe 19 Mei 2023 wilayani hapo Nasombe amesema, “Halmashauri ya mwanga asilimia 50 ya mapato yake ya ndani yanatokana na ukusanyaji wa madini ya ujenzi (mchanga) ili kuyaongezea thamani tumeona kununua gari la mchabga ambalo litatumika kusambaza mchanga huo kwenye halmashari za mkoa wa Kilimanjaro ili kuongeza mapato.”
Nasombe ameongeza kuwa gari hilo wamelinunua kwa pesa zilizopatikana kwa mapato ya ndani pasipo kuitegemea serikali kuu kiasi cha shilingi mil.177
“Halmashauri ilikuwa ikitegemea.zaidi ushuru wa mchanga lakini kwa sasa hatutaki tena kutegemea kukusanya ushuru pekee. Tunatarajia kwa siku gari hili litakuwa na uwezo wa kuingiza sio chini ya Sh milioni 1 kwa siku,” amesema Nasombe
Katika hafla hilo kumehudhuriwa watu mbalimbali akiwamo Mbunge Joseph Tadayo ambaye amewapongeza watalaamu wa halmashauri hiyo kwa kuwa wabunifu katika kuongeza vyanzo vya mapato.
“Ameshauri kuwepo na usimamizi wa mradi huo ili chombo hicho kiweze kudumu kwa kipindi kirefu, kuwepo pia na utunzaji wa gari hilo na lisitumike vinginevyo,” amesema Tadayo
Aidha Mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga Salehe-Mkwizu amesema, “ Unapokuwa na mapato mazuri utoaji wa huduma kwa jamii unakuwa mzuri, utaweza kutoa huduma bora kwenye afya, elimu, barabara, kulipa mishahara kwa watumishi.”
Mkwizu amesisitiza kama baraza walianza na ujenzi wa kiwanda cha kufyatua tofali ambazo zinatumika kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake Diwani wa Mgagao Longoviro Kipuyo; amempongeza Mkurugenzi kwa kuwa na ubunifu mkubwa jambo ambalo limefanikisha Halmashauri ya Mwanga kuweza kujiendesha pasipo kutegemea serikali kuu
“ Ded amekuwa mchapakazi, mbunifu amefanikisha wilaya ya mwanga kusonga mbele katika ukusanyaji mapato na mradi huo wa gari utakwenda kuongeza mapato ya halmashauri,” amesema Kipuyo.
Diwani wa Ngujini Theresia Msuya; amesema Gari litakwenda kuongeza mapato ya halmashauri litatumika kwenye kupeleka vifaa vya ujenzi kwenye kata hususani zilizoko milimani
“Tutapunguza gharama ambazo kata
zilikuwa zinapata changamoto ya kusafirisha vifaa kupeleka vijijini,” amesema
Diwani Theresia.
0 Comments:
Post a Comment