Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Wednesday, May 31, 2017

Zitto atoa ya moyoni kifo cha Ndesamburo

Philemon Ndesamburo, enzi za uhai wake
“Salaam zangu za rambirambi Kwa dada yangu mpenzi Lucy Owenya Kwa kupotelewa na baba mzazi Mzee Philemon Kiwelu Ndesamburo. Ni msiba mkubwa Kwa watu wa Kilimanjaro na hasa Moshi Mjini ambapo Mzee Ndesa Pesa alikuwa mwakilishi wake Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka 2015. Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu kingine chochote. Ni msiba mkubwa Kwa wanachama wa CHADEMA ambacho alikuwa Mwenyekiti wake Wa Mkoa tangu Chama kimeanzishwa mpaka mauti yalipomkuta. Huwezi kutaja maendeleo ya CHADEMA kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la Mzee Ndesamburo. Nimepata bahati ya kufanya naye kazi Kwa karibu, naweza kutamka bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda Chama chake Kwa dhati Kabisa. Ni msiba mkubwa Kwa Watanzania. Mzee Ndesamburo alitumia uwezo wake Wa kifedha na kiakili kuimarisha mfumo wa Vyama vingi nchini kwetu. Mchango wake katika kupigania Demokrasia nchini ni wa kupigiwa mfano na Kwa Kweli wengi wetu Leo tunafaidi matunda ya Vyama vingi Kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Mzee Ndesamburo na wenzake walio hai na waliotangulia mbele ya haki walifanya. Mzee Ndesamburo amechangia Sana ukuaji wa sekta ya utalii nchini. Kupitia kampuni zake za Keys Hotels ameweza kuchangia Sana ukuaji wa sekta ya Utalii nchini kwetu. Bungeni alikuwa mstari wa mbele kutaka uhifadhi wa mlima Kilimanjaro kutokana na tishio la theluji kuondoka katika uhai wetu ( in our life time). Kwa hakika Vyuo Vikuu vyetu vya Umma vingekuwa vinatenda haki Mzee Huyu angepewa Shahada ya Uzamivu ya Heshima Kwa mchango wake katika Maendeleo ya sekta ya Utalii nchini kwetu. Nawapa pole Sana watoto, wajukuu na vitukuu vya Mzee Ndesamburo. Mzee wetu aliishi maisha yake na ameacha ‘ legacy ‘ yake. Najua maumivu yenu lakini tupo wengi tunaoumia nanyi. Mungu awavushe kwenye mtihani huu mkubwa. Muwe wamoja na mshikamane. Poleni Sana ndugu zangu wa CHADEMA Kwa kupotelewa na Kiongozi wenu na Kiongozi wetu pia. Poleni Sana wana Moshi Mjini na wana Kilimanjaro wote. Poleni Sana Watanzania. Pumzika Kwa Amani Philemon Kiwelu Ndesamburo. Hiyo ni njia yetu sote. Amina”
Zitto Kabwe

Monday, May 29, 2017

Kufuturisha kwapigwa marufuku Zanzibar

Futari ya Mfungo wa Ramadhani

Serikali  ya  Mapinduzi  ya  Zanzibar  imepiga  marufuku  kuftarisha  katika  kipindi  hiki  cha  mwezi  mtukufu  wa  Ramadhan  pamoja  na uuzwaji  wa  vyakula  kiholela   hususani  vilivyopikwa  ikiwamo  juisi  isipokuwa  wa  maeneo  yaliyoruhusiwa  kisheria.

Marufuku hiyo imekuja visiwani humo ili kukabiliana na maradhi ya kipindupindu baada ya kutokea kwa visa 23 vya wagonjwa wa maradhi hayo hali ilisababisha kufunguliwa kwa kambi maalum katika Hospitali ya Chumbuni kwa wagonjwa wenye vimelea hivyo.

Akitoa  taarifa  hiyo  kwa  waandishi  wa  habari  Kaimu  Waziri  wa  Afya  Riziki  Pembe  Juma  amesema  kuwa  ugonjwa  wa  kipindupindu hususani  Unguja  umerejea  hivyo kuna haja ya kuweka mazingira ya usafi ili kuepuka maradhi hayo ikiwamo kuacha kufuturisha na kuongeza kuwa maeneo yanayoongoza kwa visa vya kipindupindu ni Mtoni Kidatu na Chumbuni.


Aidha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mikakati ya kukabiliana na maradhi hayo ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi juu ya maradhi hayo.

Monday, May 22, 2017

Vituko vya Machinjioni: Vingunguti

Wanunuzi wawili wa nyama ambao majina yao hayakufahamika mara moja katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam wakirushiana makonde katika eneo lenye kinyesi cha ng’ombe na mbuzi baada ya kutofautiana katika uchaguaji wa nyama huku mmojawapo akiwaamulia wasiendelee kupigana. 
Wengi wanafahamu kuwa siku njema huonekana asubuhi. Wataalamu wa Saikolojia wanaamini kuwa siku njema huanza siku ya nyuma yaani jana. Ikiwa na maana kuwa ili siku iwe njema maandalizi yake huanza jana na kesho yako ni kwasababu ya leo ulivyoiandaa. Iwe kwa jambo zuri au baya yote hayo ni kutokana na maandalizi yako siku ya nyuma. Kama inavyoonekana picha kituko hiki kilitokea katika machinjio ya mifugo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam saa 3 asubuhi ya Mei 21, 2017  pale wanunuzi wawili ambao majina yao hayakufahamika mara moja waliposhindwa kuelewana na kupeana songombingo la hatari lililowatoa udenda hata kusukumiana kwenye uchafu wa machinjioni hapo.




Bata wana tabia gani?

Bata dume wa kufugwa nchini Tanzania akiwa amesimamia mguu mmoja, ikiwa ni sehemu yake ya starehe.

Mwili wote wa bata kwa ujumla ni mrefu na mpana, na bata wengi kwa wastani wana shingo fupi lakini shingo la bata bukini na bata-maji ni ndefu.

Umbo la mwili la mabata kwa kiasi fulani hutofautiana na hawa kwa kuwa kidogo wa duara kidogo. Miguu yenye magamba ni yenye nguvu na iliyokuwa vizuri, na kwa kawaida, na hurushwa nyuma kabisa ya mwili, hivyo zaidi hasa kwenye spishi za majini.

Mbawa zake ni zenye nguvu na kwa ujumla ni ndogo na zilizochongoka, na kupaa kwa bata kunahitaji mapigo ya haraka bila ya kupumzika, hivyo kuhitaji misuli yenye nguvu sana. Hata hivyo spishi tatu za bata aina ya steamer hawawezi kuruka kabisa.

Spishi nyingi za bata hushindwa kuruka vizuri kipindi cha kupukutisha manyoya ya zamani na kuotesha mapya; hutafuta mazingira salama yenye chakula kingi wakati huo. Hivyo basi kipindi hiki hufuata baada ya kipindi cha kuhama.

Ndege hawa wana rangi mbalimbali. Spishi kubwa hutafuta chakula aghalabu ardhini au kwa maji machache. Spishi ndogo nyingine hula mimea ya maji na huzamia kichwa chao tu, nyingine huzamia kabisa ili kukamata samaki, wanyamakombe au mimea ya maji, lakini spishi kadhaa hutafuta chakula ardhini.

Hujenga matago yao ardhini, juu ya mwamba, ndani ya shimo la miti au ndani ya pango la sungura, mhanga.

Manyoya ya spishi kadhaa hupendwa sana kama kijazo cha mito, mifarishi, mafuko ya kulalia na makoti. Spishi nyingi za mabata hutumika kama chakula.

CHANZO: Wikipedia/Jabir Johnson
Bata jike wa kufugwa nchini Tanzania akiwa katika malisho yake
Muonekano wa shingo ya bata na eneo la kichwa cha bata wa kufugwa wa Tanzania
Bata dume wa kufugwa nchini Tanzania akiwa amesimamia mguu mmoja, ikiwa ni sehemu yake ya starehe. Bata huyo alisimama kwa zaidi ya dakika 15. Bata huyo alipigwa picha hii Mei 21, 2017 katika mtaa wa Mbuyuni, Makumbusho jijini Dar es Salaam.



Mtoto wa miaka 12 auawa, anyofolewa viungo

Ramani ya Mkoa wa Singida

MTOTO wa kike mwenye miaka 12 ameuawa mkoani Singida baada ya kunyongwa kwa kamba ya ngozi na watu wasiojulikana, kisha mwili wake kunyofolewa baadhi ya viungo na kutoweka navyo kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni imani za ushirikina.

Mtoto huyo Dorcas Meshack mkazi wa Kijiji cha Matongo Wilaya ya Ikungi aliondoka nyumbani kwao juzi majira ya saa sita mchana na kuaga kuwa anakwenda kuvuna mahindi kwenye shamba lililopo umbali wa mita 70 lakini hakurejea tena hadi mwili wake ulipookotwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi Isaya Mbughi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi unaendelea.


Hata hivyo Mrakibu Mwandamizi Mbughi ameitaka jamii mkoani humo kuweka utaratibu wa ulinzi dhidi ya watoto na kutoa taarifa kwa mtu yeyote au kundi lolote linalojihusisha na vitendo hivyo.

Leo ni siku ya Wabaha'I

Alama ya Wabaha'I
Jumuiya ya Wa-Bahai waishio Dar es Salaam leo inaungana na jumuiya nyingine za madhehebu hayo kote ulimwenguni kwa ajili ya kusherehekea Tangazo la Bab.
Bahá'u'lláh_(Mírzá_Ḥusayn-`Alí_Núrí) mwaka 1868
Katika taarifa yake Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Baraza la Kiroho la Wabaha’I wa Dar es Salaam Qudsiyeh Roy amesema tangazo la Bab ni mojawapo ya siku takatifu tisa kwa mujibu wa imani yao ambapo siku ya maadhimisho, Wabaha’I hawapaswi kwenda kazini ama Shuleni.

Roy amesisitiza kuwa kuwa imani yao inajitegemea, isiyopaswa kuunganishwa na imani nyingine kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiilinganisha na dini nyingi kubwa hususani Uislamu.

Ibada fupi, usomaji wa maandiko matakatifu, burudani ya nyimbo, mazungumzo na chakula vitafanyika katika maadhimisho hayo.

Licha ya kusherehekea siku hii, wafuasi hao wa Bahaullah watakuwa wakitimiza miaka 174 tangu kuzaliwa kwa Imani ya Baha’I, mnamo Mei 22, 1844 Bab alikamatwa, kupigwa na kufungwa hatimaye aliuawa Julai 9, 1850 hadharani katika uwanja wa Tabriz nchini Iran.

Wabaha’I wanaamini kuwa wadhihirishaji wote wa Mungu ni pamoja na Ibrahimu, Krishna, Musa, Zoroasta, Budhaa, Yesu, Muhammad, Bab na Bahaullah ambao ni waelimishaji watukufu.

Friday, May 12, 2017

Raila kufanya mkutano Mei 14 katika ngome ya Jubilee

Raila Odinga akifanya maombi Jerusalem hivi karibuni.
Mgombea urais kwa tiketi ya Muungano wa Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga anatarajiwa kuongoza maelfu ya watu katika mkutano mkubwa wa kwanza akiwa na viongozi wa muungano huo kwenye ngome za chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Hayo yanajiri baada ya kumaliza safari yake ya kuhiji mjini Yerusalemu ambako Odinga alifanya maombi katika mji huo mtakatifu kabla ya kuanza Kampeni za kuwani kiti hicho Agosti 8 mwaka huu.

Odinga anatarajiwa kurudi nchini humo na kufanya mkutano huo Jumapili ya Mei 14 mwaka huu huko Nakuru katika viwanja vya Afraha. NASA inaamini kwa kufanya mkutano katika eneo hilo tayari wameshapata kura milioni 10.

Mratibu wa mkutano huo Boni Khalwale amesema jana kuwa viongozi watano Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Isaac Ruto, Moses Wetangula na Raila wakitarajiwa kuhudhuria katika ngome hiyo imara ya Jubilee.

Akiwa nchini Israel, Raila alizuru ukingo wa Magharibi.

Tuesday, May 9, 2017

NEC yapiga hatua elimu kwa njia ya Redio

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wananchi walioko kwenye halmashauri mbalimbali nchini, kuitumia vyema fursa ya utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia redio kwenye halmashauri zao ili kuondoa manung’uniko kwenye chaguzi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani wakati akizungumzia mpango wa kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima ulioanza kutekelezwa jana katika mikoa kumi nchini.

Amesema kupitia mpango huo wananchi wanaosikiliza redio za kijamii kwenye halmashauri nchini, watapata fursa ya kujifunza elimu ya mpiga kura na kuelewa masuala yote muhimu yanayohusu mfumo mzima wa kupiga kura.

Utekelezaji wa mpango huo umegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza limeanza kutoa elimu hiyo elimu hiyo kwenye mikoa ya Kagera,Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya na Dodoma.

Mikoa mingine itakayojumuishwa kwenye kundi hilo ni Ruvuma, Mara, Pwani na Mtwara ambapo elimu hiyo itatolewa hadi Mei 20 mwaka huu.

Kundi la pili linatarajiwa kutoa elimu hiyo kuanzia Mei 24 hadi Juni 7 mwaka huu katika mikoa ya Geita, Tanga, Singida, Shinyanga, Lindi, Arusha, Tabora, Kigoma, Iringa, Manyara, Rukwa, Katavi, Songwe, Njombe na Simiyu.


Thursday, May 4, 2017

Mizoga ya Tembo yapungua Selous Game Reserve

Mzoga wa tembo baada ya kuuliwa na majangili
MAUAJI ya tembo katika Mbuga ya Selous yamepungua kutoka mizoga 184 hadi 84.
Hayo yanajiri wakati ambapo tembo wawili kuuawa na wananchi hivi karibuni huku mmoja aking’olewa meno yake katika kijiji cha Wenje Tarafa ya Nalasi wilayani humo.
Akizungumza katika kikao cha Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Kaimu Mkurugenzi wa Operesheni ya kuuzuia Ujangili dhidi ya wanyama Pori Robert Mande  amesema takwimu hizo zinaonyesha kuwa ukubwa wa tatizo hilo umepungua kutokana na jitihada za kupambana na majangili.
Mande amesema mizoga ya tembo imepungua kutokana na wafanyabiashara wakubwa wa pembe za ndovu kukamatwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Tunduru Juma Homera amewataka watu wanaomiliki Silaha Kiholela kuzisalimisha kwenye ofisi za vijiji na vituo vya Polisi
Homera amebainisha kuwa wananchi wanaoishi karibu na mipaka ya nchi jirani ya Msumbiji wanapata silaha hizo kwa kubadilishana na chakula.
Kutokana na tukio hilo watuhumiwa 8 wa ujangili wamekamatwa

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la  PAMS Foundation linalojishughulisha na Mapambano dhidi ya Ujangili Maximillan Janes  amesema shirika limetoa ndege mbili ambazo zinatumika kulinda wanyama wasiingie katika makazi ya watu pia kufuatilia mienendo ya watu wanaojihusisha na ujangili.

Tuesday, May 2, 2017

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017

NA MWANDISHI WETU
Wanataaluma na Wadau wa Habari nchini, hii leo wamekutana katika Kongamano la kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili tasnia hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017.
Kitaifa Maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza ambapo kilele chake ni kesho huku mgeni rasmi anakitarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli.
Miongoni mwa wachangia mada kwenye kongamano hilo ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji, Mtaalamu wa masuala ya teknolojia nchini, Innocent Mungy, Mwanasheria na Mwanataaluma ya Habari, James Marenga, na Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), Ernest Sungura.

 
Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji

Eminem ashtaki Chama Tawala cha New Zealand

WELLINGTON, NEW ZEALAND
Chama tawala cha New Zealand kimesema hakitajibu chochote baada mwanamuziki mashuhuri wa Marekani Eminem kukipandisha chama hicho kortini.
Eminem
Msemaji wa chama hicho Steven Joyce amesema kwa sasa wanasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu shtaka hilo.
Jana mwanasheria wa Eminem  Garry Williams aliiambia mahakama Kuu mjini Wellington kuwa chama tawala cha New Zealand kilitumia wimbo wake ambao kwenye tangazo la kampeni bila idhini ya msanii.
Rapa huyo amesema wimbo uliotumiwa katika tangazo la chama cha National Party mwaka 2014 ulikuwa makala ambayo haikuwa imeidhinishwa ya wimbo wake wa Lose Yourself.
Lakini mawakili wa chama hicho wanasema wimbo uliotumiwa haukuwa wa Lose Yourself, bali ni wimbo ufahamikao kama Eminem-esque ambao waliununua kupitia soko la jumla la muziki mtandaoni.
Katika kesi hiyo iliyoanza jana na kutarajiwa kuchukua takribani siku sita, nyimbo zote mbili zilichezwa katika ukumbi wa mahakama.
Wakili wa Eight Mile Style, kampuni inayomuwakilisha mwanamuziki huyo, amesema wimbo wa Lose Yourself ulikuwa na kipekee na bila shaka ni fahari ya kazi za sanaa za Eminem.
Tangazo hilo la mwaka 2014 lilikuwa na picha za wapiga makasia na sauti nyuma yake ikiwahimiza watu kudumisha "timu ambayo inafanya kazi" na kurejesha National Party madarakani katika uchaguzi uliokuwa unakaribia.
Wimbo uliotumiwa, Eminem-esque, unakaribiana sana na Lose Yourself, ambayo ulitumiwa katika filamu ya Eminem ya 8 Mile ambayo ilitolewa 2002.


Monday, May 1, 2017

Mei Mosi 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili Aprili 30, 2017.
Leo ni siku ya wafanyakazi duniani kitaifa inaadhimishwa mkoani Kilimanjaro.
Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Kauli mbiu ya mwaka huu, “ Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki, Maslahi na Heshima kwa Wafanyakazi.”