Friday, March 1, 2024

Rais wa Awamu ya Pili Tanzania afariki dunia, Kuzikwa Machi 1, 2024 Zanzibar

 

Aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 98.

 

Rais wa awamu ya sita wa Tanzania  Samia Suluhu alitangaza kifo chake kuwa kilitokea Alhamisi jioni yapata saa 5.30 usiku.

 

Suluhu alitangaza kuwa rais huyo wa zamani alifariki kutokana na saratani.

 

Mwinyi alikuwa Rais wa Tanzania kati ya 1985 hadi 1995.

 

Mwinyi alichukua nafasi kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 

Rais Suluhu ametangaza kipindi cha siku 7 cha maombolezo ambapo bendera zitapandishwa nusu mlingoti.

 

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, natuma salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na wananchi wa Tanzania kwa msiba huu mkubwa," alisema.

 

Rais Suluhu alitangaza kuwa Mwinyi atazikwa Machi 1, 2024 huko Uganja Nyanda za Juu Zanzibar.

0 Comments:

Post a Comment