Mjukuu
wa Mangi Meli Mandara, Isaria Meli ameiomba serikali ya Tanzania iingie
rasmi katika mpango kazi wa kuyafanya Masalia ya Mangi Meli kuwa
vivutio vya Utalii nchini ili kuepusha upotevu wa Kumbukumbu muhimu za
kihistoria za kiongozi huyo wa kijadi.
Hayo yanajiri wakati
ambapo Old Moshi inaadhimisha miaka 122 tangu kuuawa kikatili kwa Mangi
Meli kwa kunyongwa kwenye mtu mbele ya umati wa watu kisha kupigwa
risasi na wakoloni wa Kijerumani huko Tsuduni, Old Moshi mkoani
Kilimanjaro mnamo mwaka 1900
Akizungumza na vyombo vya habari
Isaria Meli Mandara amesema wakati umefika kwa serikali kuingilia kati
suala hilo na kuliweka kwenye mpango rasmi wa kuvifanya kuwa vivutio vya
Utalii ili kuendelea kutunza Kumbukumbu ya Kihistoria ya Wachagga wa
Old Moshi.
Mjukuu huyo wa Mangi Meli mwenye umri wa miaka 92
amesema umri wake umekwenda anahitaji kuona masalia hayo yanakuwa na
faida kwao na kwa watanzania.
Kwa upande wake mwanaharakati wa
masuala ya historia Mnyaka Sururu Mboro mwenye umri wa miaka 76
anasema juhudi za pamoja kama nchi zitawaamsha wakoloni hao kurudisha
Masalia ya Jamii mbalimbali za Tanzania ambazo masalia yao yapo nje ya
nchi.
Mnyaka Sururu Mboro ambaye alianza harakati hizo tangu
mwaka 1977 za kutaka masalia ya Mangi Meli kurudi nchini amesema Bado
ana matumaini ya kurudi nchini na kufanyiwa maziko ya Mashujaa hao kila
jamii kwa namna yao.
Mnamo Machi 2 kila mwaka Jamii ya Watu wa
Old Moshi huadhimisha Kumbukumbu hiyo kwa madhumuni ya kuendelea
kupambana masuala hayo kurudi katika Ardhi Yao ili historia yao iendelee
kutunza na Kukumbukwa kizazi hata kizazi.
0 Comments:
Post a Comment