Monday, March 4, 2024

Pandashuka rekodi za Kili Marathon na Ongezeko la Joto

 

Augostino Sulle akimaliza kilometa 42 katika Kili Marathon 2024 akitumia saa 02:21:06

 

Mbio za Kimataifa za Kili Marathon mwaka 2024 zilifanyika katika mji wa kipekee wa Moshi mkoani Kilimanjaro ambako ndiko chanzo cha mbio hizo kuanza kufanyika mnamo mwaka 2003.

 

Katika makala ya 22 ya Kili Marathon kulishuhudiwa mtanzania Augostino Sulle kilomita 42.2 kwa wanaume akitumia saa 02:21:06, akimpita Mkenya Abraham Kipkosegei Too kwa sekunde 68 ambapo Kipkosegei alitumia saa 02:22:02 na kushika nafasi ya pili, huku Mkenya mwingine Elisha Kimutai akibanana vilivyo na Kipkosegei akizidiwa kwa sekunde tano aliyetumia saa 02:22:07 hivyo kushikilia nafasi ya tatu.

 

Sulle anakuwa bingwa mwaka 2024 baada ya miaka miwili alipolitwaa taji hilo mnamo mwaka 2021 akitumia saa 02:17:58 mbele ya  Michael Kishiba Sanga (02:19:15) na Charles Sulle (02:29:39).

 

Kwa upande wa wanawake, Mtanzania Natalia Sulle alishinda mbio hizo akitumia  saa 02:51:23 akiwa mbele ya mtanzania mwingine kwa sekunde 24 na kushinda mbio hizo; Nafasi ya Pili ilikamatwa na Neema Sanka aliyetumia saa  02:51:47, huku Vailet Kidasi akishinda nafasi ya tatu baada ya kukimbia kwa saa 03:01:03 na hivyo kukamilisha ushindi wa Watanzania kwa nafasi zote tatu za kwanza kwa kilomita 42.2 kwa wanawake.

 

Katika mbio hizo maarufu nchini na nje ya nchi ya Tanzania kufanyika rekodi mbalimbali zimekuwa zikiwekwa tangu kuanzishwa kwake huku nyingine zikiwa bado hazijafikiwa kutokana na sababu mbalimbali.

 

Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitoa changamoto ya nguvu kwa wanariadha wenyeji wa Tanzania hatua mabayo imewafanya Watanzania kujitahidi kupambana katika mbio pekee nchini zenye hadhi ya Kimataifa.

 

Shirika la Utabiri wa Hali ya hewa Duniani (WMO) linasema Tangu miaka ya 1980 kila muongo umekuwa wa joto kali kuliko uliotangulia na kwamba mwenendo huu unatarajiwa kuendelea kwa sababu ya ongezeko la joto hewani linalotokana na gesi ya viwandani.

 

Kwa mujibu wa wastani wa seti za takwimu zilizokusanywa na kutumiwa kutoa tathimini hii kiwango cha joto cha kimataifa kwa mwaka 2019 kilikuwa nyuzi joto 1.1°C zaidi ya kiwango cha wastani kilichokuwa katika ya miaka 1850-1900, ambacho ndio kilitumika kuelezea wastani wa kiwango cha joto katika nyakati za kabla ya mapinduzi ya viwanda.

 

Mji wa Moshi umeshuhudiwa kuwa na joto kali kuliko ilivyozoeleka zaidi ya nyuzijoto 21 kipimo cha Celcius hatua ambayo imepunguza kasi ya wanariadha wengi walitamani kuweka rekodi kwenye mbio hizo mwaka huu.

 

Baadhi vya vyanzo vilirekodi joto kufikia nyuzijoto 31 kipimo cha Celcius, hatua mbayo imewafanya wanariadha kupambana na hali hiyo ukilinganisha na miaka mingine ambayo wanariadha walikimbia katika halia ya kawaida ya joto.

 

Rekodi za mwaka huu zimekuwa mbaya ukilinganisha na Kili Marathon za mwaka 2020, 2021, 2022 na 2023. Ambapo kwa wanaume muda walianza ni saa mbili na dakika 21 ikiwa ni chini kwa dakika nne mwaka 2020 na 2023, dakika sita mnamo maka ya Kili Marathon 2022 na dakika tano mnamo mwaka 2021 kwa washindi wa kwanza wanaume.

 

REKODI ZA KILI MARATHON KUTOKA MWAKA 2020-2024 KWA BAADHI YA WANARIADHA

2024

Augostino Paul Sulle (02:21:06)

Abraham Kipkosegei Too (02:22:02)

Elisha Kimutai (02:22:07)

Charles Boay Sulle (02:22:42)

………

Natalia Elisante Sulle (02:51:23)

Neema Sanka (02:51:47)

Sarah Kiptoo (03:01:41)

 

2023

Kenneth Kiprop Omulo (02:18:05)

Abraham Kipkosgei Too (02:18:30)

Paul Damian  (02:22:56)

…..

Sara Ramadhan (03:02:36 )

 

2022

Alphonce Felix Simbu (02:16:30)

Arnold Kiptaoi (02:17:04)

James Tallam (02:17:42)

 

…..

Shelmith Muriuki (02:41:05)

Flavious Teresa Kwamboka (02:57:21)

Angel John (03:06:12)

 

2021

Augostino Paul Sulle (02:17:58)

Michael Kishiba Sanga (02:19:15)

Charles Sulle (02:29:39)

…..

Jackline Sakilu (02:45:20)

Catherine Lange (02:59:06)

 

2020

Cosmas Muteti (02:18:16)

David Kipkorir Ruthoh (02:18:41)

 Phillip Kangogo (02:19:19)

 

 

 

0 Comments:

Post a Comment