Timu ya Taifa ya Morocco iliiweka Afrika katika ramani ya Dunia baada ya kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia 2022, ikitolewa na Ufaransa.
Hata hivyo
iliambulia nafasi ya nne, ikizidiwa na Croatia iliyoshika nafasi ya tatu.
Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.
Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.
Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.
JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.
Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.
Timu ya Taifa ya Morocco iliiweka Afrika katika ramani ya Dunia baada ya kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia 2022, ikitolewa na Ufaransa.
Hata hivyo
iliambulia nafasi ya nne, ikizidiwa na Croatia iliyoshika nafasi ya tatu.
Romero alicheza
dakika zote 120 katika fainali dhidi ya Ufaransa wakilitwaa kwa mikwaju ya
penati. Romero alikuwa kiungomuhimu katika kulitwaa kombe hilo akiwa na La Albiceleste.
Tunaposema
MERRY CHRISTMAS Maana yake ni FURAHA YA KUSANYIKO LA WAKRISTO.
Kwa hiyo
hakuna mahusiano baina ya Christmas na kuzaliwa kwake Yesu Kristo Desemba 25.
katika hili wala tusimung'unye maneno.
Nyakati
zile Dola ya Rumi ilipokuwa ikitawala dunia walikuwa wana miungu yao ambayo
iliabudiwa kila siku na Desemba 25 kila mwaka walifanya sherehe ya kuitukuza
miungu yao hiyo.
MAJINA
YA SIKU NA MIUNGU ILIYOABUDIWA
>Jumatatu (Monday) - inatokana na moon day, kwa wapagani wa nyakati zile ilimaanisha siku ya kumwabudu mungu moon (mwezi).
>Jumanne (Tuesday) – inatokana na tiw’s day, kwa wapagani wa nyakati zile ilimaanisha ni siku ya mungu Tiw.
>Jumatano (Wednesday) – inatokana na wedn day au woden day, kwa wapagani ilimaanisha siku ya mungu wedn au woden.
>Alhamisi (Thursday) - inatokana na ,,thor day,, kwa wapagani ilikuwa ni siku ya kumwabudu mungu thor.
mungu frig au freia.
>Jumamosi (Saturday) – inatokana na Saturn day (siku ya sayari zohari), kwa wapagani
ilikuwa ni siku ya kumwabudu mungu wa Kirumi aitwaye ,,Saturn,, yaani kwa Kiswahili
sayari ya zohari.
>Jumapili (Sunday) –ilitokana na sun day (siku ya jua), kwa wapagani waKirumi ilikuwa ni
siku ya kumwabudu mungu sun (jua).
Kwa ujumla, Siku zote za juma, Warumi walizipa majina ya miungu yao, kwa sababu hao
kwa kipindi hicho ndiyo walikuwa watawala dunia kwa wakati huo.
Katika
miungu yote iliyotajwa hapo juu, mungu mkuu alikuwa ni mungu jua (sun) wao
walimuita ni mungu asiye shindwa.
Hata
baada ya utawala wa Dola ya Kirumi kuvunjika na nchi kuanza kujitawala bado watu
kutoka mataifa mbalimbali waliendelea kuikumbuka miungu hiyo kila ifikapo
Desemba 25 kila mwaka, na wengine walifunga safari kwena Mjini Rome Italia
kushereheke sikukuu hizo za miungu ambazo hazikufahamika kwa jina la CHRISTMAS.
Hata
warumi wenyewe waliposherehekea sikukuu hizo hawakuziona kuwa ni SIKUKUU ZA
KIPAGANI maana walijiona wako sahihi (njia ya mtu ni njema machoni pake
mwenyewe).
Miaka ilivyozidikuendelea mbele ndipo baadhi ya watu waliopata kuifahamu kweli wakatambua hawakuwa sahihi kuendelea kuitumikia miungu ya kirumi wakati yupo Mungu muumba wa mbingu na nchi. Na hapo ndipo CHRISTMAS ilipoanzishwa.
Lengo
kuu la kuianzisha sikukuu ya christmas lilikuwa ni kuvunja nguvu au kufuta
kabisa zile sherehe za kuiabudu au kuitukuza miungu ya kirumi kila Desemba 25
ya kila mwaka na ndio maana hata Christmas ilipoanzishwa ikapangwa katika
tarehe sawa na sikuku ile ya kuiabudu miungu ya rumi.
Katika sherehe za Christmas watu walikuwa wakipokea zawadi kama vile nguo na vyakula nk, lakini katika zile sherehe za miungu ya ya warumi watu walikuwa wakiitolea zawadi ile miungu waliyoiabudu na huo ndio mwanzo wa Father Christmas.
Hali hiyo iliwafanya watu kuanza kuyaendea makusanyiko yaliyopewa jina la Christmas na kusahau kuindea ile miungu yao kwa kuwa christmas ilitumika kwa matendo mema na ya faraja.
Katika sherehe za Christmas watu walifundishwa matendo mema kwa kuwasaidia wahitaji kwa kuwapelekea zawadi kwa kunukuu maandiko kwamba hata Yesu Kristo alipozaliwa watu walipeleka zawadi zao.
Hapo ndipo Christmas ilipoanza kuhusishwa na KUZALIWA KWA YESU KRISTO jambo ambalo ni kinyume na uhalisia wa maana ya jina au neno CHRISTMAS.
Neno Christmas halipatikani popote katika biblia hata ukisoma kitabu cha MWANZO mpaka UFUNUO WA YOHANA huwezi kuliona neno Christmas.
Pia huwezi kuizungumzia Christmas kwa maana ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo huku ukiwa umeshika Biblia mkononi kwa kuwa hakuna andiko litakalo kusapoti hoja zako.
Kuamini
CHRISTMAS ni kuzaliwa kwa Yesu Kristo huku ni kuamini kusiko sahihi.
KUZALIWA KWA YESU KRISTO.
Biblia imekaa kimya kabisa kuhusiana na tarehe na mwezi na hata mwaka aliozaliwa Yesu Kristo, hata Yesu mwenyewe hakuwahi kuwaambia mitume na manabii wa nyakati zake kuhusiana na tarehe halisi ambayo yeye alizaliwa, na hata wanafunzi wake hawakuwahi kudadisi dadisi kuhusu jambo hilo.
Hata kama mitume na manabii wa nyakati za Yesu wangepata kufahamu tarehe halisi aliyozaliwa Bwana Yesu, kuifahamu tarehe hiyo kusingeweza kuwa na msaada wowote katika maisha yao ya kiroho.
Mtu yeyote anapokombolewa vitani baada yakuwa ameshikiliwa mateka kwa muda mlefu, atakachokifurahia mtu huyo ni tendo la kukombolewa kwake pomoja na jina la komandoo aliyemuokoa ili apate kushukuru kwa ujasiri wake, maana tarehe ya kuzaliwa kwa komandoo huyo wala hainamsaada kwake hata kama ataifahamu.
LUKA 1:31, imeandikwa Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume, na jina lake utamwita jina lake Yesu.
Huu ni ujumbe wa Malaika Gabrieli kwenda kwa Marimu na ilikuwa ni mwezi wa sita (6).
Ujumbe unasema UTACHUKUA MIMBA, sio unachukua mimba.
Maana kama ujumbe ungesema UNACHUKUA MIMBA, nayo ilikuwa ni mwezi wa sita, basi Yesu alifaa azaliwe mwezi wa tatu (sio wa kumi na mbili) hii ni kulingana na muda uaotakikana kwa mwanadamu kubeba mimba mpaka kuzaa mwana.
Kwahiyo kwasababu ujumbe wa Malaika ulisema Tazama utachukua Mimba, hivyo haikuwekwa wazi kwamba hiyo mimba mariamu aliipata mwezi wa ngapi, maana ujumbe ni UTACHUKUA MIMBA na sio unachukua mimba.
Hakuna
mtume wala nabii yeyote aliyewahi kuikumbuka au kusherehekea siku ya kuzaliwa
kwake Yesu Kristo, hata Yesu mwenyewe hakuwahi kuagiza hayo.
MAFANIKIO YA KUANZISHWA KWA CHRISTMAS.
Kama
nilivyosema hapo awali kwamba, lengo la kuanzishwa kwa Christmas lilikuwa ni
kuvunja na kuondoa kabisa zile sikukuu za kuabudu miungu ya kipagani ya kirumi,
kwa kuianzisha christmas katika tarehe ileile ambayo wapagani wa kirumi
waliitumia kuiabudu miungu yao, ndiomaana leo hii sherehe za kuiabudu miungu ya
kirumi imebaki kuwa ni historia tu badala yake kila mtu anaifahamu Christmas
kama ndio siku ya kuzaliwa Yesu Kristo (japo si kweli)
ACP Simon Maigwa |
Mwishoni mwa miaka ya 1970, mjasiriamali na mgunduzi wa mfumo wa simu za kiganjani nchini Marekani Martin Cooper alisema, “Tulijua kuwa watu hawapendi kuzungumza ndani ya magari, au nyumba; au maofisini wanataka kuzungumza na watu wengine…Tulichokuwa tukiaminini kwamba namba ya simu inatakiwa kuwa ya mtu binafsi badala ya kuwepo eneo fulani.”
Majaribio ya Cooper na wagunduzi wengine yameifanya dunia kwa sasa kuwa ya kipekee, mtu aweza kuwasiliana binafsi na mtu mwingine na wakazungumza ajenda zao za binafsi kwa wakati wowote.
Hivyo ndivyo wadau wa maendeleo mkoani Kilimanjaro (KDF) walivyoona fursa kupitia kampuni ya simu nchini Vodacom kwa namna gani wanaweza kurahisisha mawasiliano miongoni mwa Maofisa wa Jeshi la Polisi hivyo kuifanya kazi ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuwa nyepesi.
Ilianzia hapa pale KDF ilipofanya makubaliano na Vodacom na kukubaliana nao kuwapa Polisi na wafanyakazi wote wa Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro namba za Vodacom ili waweze kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe bure.
Hatua hiyo inawafanya maofisa wa Polisi kupunguza gharama za mawasiliano miongoni mwao, kupitia mfumo wa Closed User Group (CUG) ambapo mfumo huo ni maalum kwa maofisa hao pekee.
Tukio hilo la makabidhiano ya laini za simu limefanyika Desemba 19,2022 mjini Moshi katika ukumbi wa mikutano wa Kili Wonders.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro( ACP) Simon Maigwa amesema zoezi hili litaimarisha mawasiliano baina Askari na Askari katika utendaji wa kazi za Askari za kila siku.
“Niwapongeze sana KDF
kwa kuleta wazo hili ambalo limehusisha Kampuni ya Vodacom PLC,Chief Premium
Beer, na Jeshi la Polisi.Ni hatua kubwa kwakweli na hili itarahisisha utendaji
kazi kwa Askari wetu,Gharama hazitakuwepo hivyo mawasiliano yatafanyika kwa
urahisi na kazi zetu pia zitaenda ukizingatia pia mawasiliano ni muhimu sana
katika kazi zetu hizi,” amesema ACP Maigwa.
Aidha mjumbe wa KDF Rashid Tenga amesema zoezi hilo ni endelevu na halitadumu katika msimu huu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
“Tutatoa Dk 300 za muda wa maongezi kwa shilingi Elfu mbili pekee mwezi mzima kwa askari wetu na zoezi hili ni endelevu, Iwapo kutakuwa na uhitaji zaidi wa huduma hii katika msimu wa sikukuu n.k tutaona namna ya kufanya,Hata hivyo tutaangalia pia uwezekano wa sekta nyingine kupatiwa huduma hii.,”
“Tumeanza na wenzetu wa
Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro na lengo kubwa ni kuhakikisha tunarahisisha
mawasiliano na kufanya utendaji kazi wao kuwa rahisi zaidi.,mafanikio tutakayo
yapata ndio yatasababisha tuangalie namna ya kuingia pia katika mikoa mingine,”
ameongeza Tenga.
Hafla hiyo ilihudhuriwa
na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Kilimanjaro akiwamo Mkuu wa Wilaya ya
Moshi Mjini Abbas Kayanda.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Abbas Kayanda
Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto imeanza kuchukua hatua za kuwalinda Watumishi
wake dhidi ya magonjwa ambukizi kwa kuwapatia chanjo ya Homa ya Ini na kuwapima
magonjwa mengine ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao wakiwa kazini.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dkt.
Leonard Subi, wakati wa uzinduzi wa upimaji wa afya kwa watumishi wa hospitali
hiyo uliofanyika hospitalini hapo.
Alisema ugonjwa huo umekuwa tishio katika siku za hivi
karibuni ambapo amesema pamoja na tishio hilo jambo jema ni kuwa unatibika pale
unapogundulika mapema.
“Mara nyingi tumekuwa wakitoa huduma za afya kwa watu wa nje
ambapo kwa mwaka 2021 takribani watu
13,000 tuliwafikia katika maeneo
mbalimbali ya nchini kwa kutumia gari letu maalumu kwa ajili ya kuwapima, kuwachunguza
afya zao zikiwemo zile zinazotolewa kwa njia ya usafiri (mobile services),”alisema
Dk.. Subi.
Alisema takribani asilimia 26 ya waliopimwa walikutwa na
changamoto ya shinikizo la damu, asilimia tisa kisukari ikiwa ni sehemu tu ya
matokeo ya huduma ya upimaji waliofanyiwa watu kipindi hicho.
Akizungumza kuhusu zoezi hilo la upimaji wa afya kwa
wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk. Subi amesema limelenga kuhakikisha ya kuwa
watumishi hao wako salama mahala pa kazi wakati wakiendelea kutoa huduma zao
kwa watu wengine.
Aidha Dk. Subi alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha
wanajenga tabia ya kupima afya zao kwa kushirikisha familia zao pamoja na
wengine wote wanaoishi nao ili kuepuka kupata maradhi ambayo yaambukiza.
Kuhusu ugonjwa wa COVID-19, Dk. Subi amesema pamoja na
juhudi kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Serikali katika
kukabiliana nao bado ugonjwa huo uko hivyo ni vyema watu wakaendelea kuchukua
tahadhari kama inavyoelekezwa na wataalam wa afya.
Kwa upande wake Katibu wa Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi
Kibong’oto Rose Shawa, alisema zoezi
hilo ni la hiyari na kutoa wito kwa watumishi wote kushiriki ili kujua hali zao
za kiafya na pia kujenga mazingira ya uhakika wa afya zao pale wanapoendelea
kuhudumia watu wengine.
Bi. Rose alisema zoezi hili sio la kwanza kufanyika
hospitalini hapo kwani mazoezi kama hayo
yameshawahi kufanyika mwaka 2015 hadi
mwaka 2022 kwa watumishi kuchunguza afya na kupatiwa chanjo ya homa ya ini.
Mratibu wa shughuli za afya ya Jamii hospitali ya Kibong’oto
Dk. Alexander Mbuya, alisema zoezi la upimaji na chanjo ya homa ya ini ni suala
muhimu sana kwa wafanyakazi wa hospitali ya Kiobong’oto.
Wakizungumza kwa
niaba ya watumishi wenzao wa afya katika
hospitali hiyo Afisa Mazingira Asharose Muttasingwa na Afisa Muuguzi
Msaidizi kitengo cha Afya ya Jamii
Eulogy Tukay walimpongeza Mkurugenzi wa
hospitali hiyo kwa kuja na wazo la watumishi wenzake kuona umuhimu wa kupima afya zao.
Zoezi la upimaji wa afya kwa Watumishi wa Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto lilianzihswa mwaka wa 2015 wakati huo kukiwa na watumishi 264 ambapo 256 kati yao walipima afya zao.
Kaimu Meneja wa Posta Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro Veronica Magoto (kulia) akimkabidi mhudumu wa afya kituo cha kulelea wazee Njoro Bi. Maria Hatari Massawe
Vijana wameshauriwa kujitolea na kuwatunza wazee katika maeneo yao ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa maendeleo yao na taifa.
Kaimu meneja wa Posta Mkoa
wa Kilimanjaro Veronica Magoto ameyasema hayo jana wakati wakikabidhi misaada
mbalimbali ya kijamii kwenye kituo cha kulelea wazee wasiojiweza kilichoko
Njoro Manispaa ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
Siku ya Posta Duniani.
Magoto alisema kuwa jukumu
la kuwatunza na kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii pia ina nafasi
yake katika kuwatunza wazee hasa Vijana huku akisema kuwa Serikali imejitaidi
sana kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za afya na
kuwatunza wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali
ya wazee nchini.
Akizungumza kwa niaba ya
mkuu wa kituo cha wazee Derick Lugina,
Mhudumu wa afya Maria Hatari Massawe, amelishukuru Shirika la Posta
Kilimanjaro kwa misaada hiyo ambapo amesema ni msaada mkubwa huku akiziiomba na
taasisi nyingine kuwa na moyo wa kutoa kwa watu wenye uhitaji kama ambavyo
wamefanya Posta.
“Kambi yetu ina wazee 17
hadi sasa wanaolelewa katika kituo hiki, hivyo Shirika la Posta Kilimanjaro
mmefanya jambo kubwa sana ambalo limegusa maisha ya watu wengi ambao hawana
msaada na hili linasisitizwa hadi kwenye vitabu vya dini,”alisema.
Awali akisoma risala ya
maadhimisho ya siku ya Posta Duniani Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania Mkoa wa
Kilimanjaro Mwanamkuu Mussa, amesema
wametoa misaada hiyo kwenye kituo cha kulele a wazee wasiojiweza cha
Njoro kilichoko Manispaa ya moshi ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii
kuadhimisha siku ya posta duniani.
“Misaada tuliyookabidhiwa
kwa wazee wasiojiweza wanaoishi kwenye kambi ya wazee ya Njoro iliyoko Manispaa
ya Moshi inayomilikiwa na Serikali kuu
ni mchele, sukari, sabuni za kufulia, kuogea na kudekia pamoja na
pampers kwa ajili ya kuwasitiri wazee,”alisema Mwanamkuu.
Wakizungumza kwa niaba ya
wazee wenzao wanaolelewa katika kituo hicho James Joseph na Katarina Batazari
wameushukuru uongozi wa Shirika la Posta
kwa moyo wao wa kuwajali wazee na kuweza kuja kuwaona.
“Naomba utufikishie
shukurani zetu kwa Meneja wa Posta mkoa wa Kilimanjaro kwa kutujali wazee hasa
kwa kutatua changamoto zetu zinazotukabili, kwani tupo wazee ambao
tumetelekezwa na watoto wentu…lakini kumbe tuna watoto wanaoweza kuja na
kututembea na kutupatia zawadi kama hizi,” alisema mzee Joseph.
Bi. Katarina Batazari akipokea msaada wa sabuni ya maji kutoka kwa mfanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania mkoa wa Kilimanjaro Emmanuel Assey (kulia) akimkabidhi mhudumu wa afya kituo cha kulelea wazee Njoro Bi. Maria Hatari Massawe, mfuko wa sukari, ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya Posta Duniani.
Chifu Marealle (kushoto) akipokea zawadi ya kifimbo cha uchifu kutoka kwa Chifu Omary Mwariko 'Mhelamwana' walipokutana Marangu, Moshi mnamo mwezi Agosti 2022. (Picha: Maktaba) |
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi uenyekiti wa UMT aliodumu nao kwa takribani miaka 13,
huko Marangu, Moshi mkoani Kilimanjaro; Chifu Marealle amesema matumizi ya
fedha yamekuwa changamoto kubwa kwa taasisi nyingi nchini.
“Fedha
zitumike kwa lengo lililokusudiwa la kuendeleza shughuli za umoja, msitumie
fedha hovyo, fedha kidogo inayopatikana itumike kuendeleza umoja huo,” amesema
Chifu Marealle
Aidha
Chifu Marealle amesema suala la matumizi ya fedha linapaswa kutiliwa mkazo ili kuepusha
mgongano wa kimaslahi unaoweza kufanywa endapo hakutafnyika uchaguzi wa
viongozi sahihi kuongoza UMT.
“Changamoto;
wako baadhi ya wanachama walitaka kuuvuruga umoja huo lakini aliweza kusimama
imara na kuweza kufanikiwa kuwaunganisha na kuwa wamoja,” ameongeza Chifu
Marealle.
Chifu
Marealle amesema kwa miaka yote alioongoza umoja huo amejifunza mambo mengi
kutoka kwa machifu huku akisisitiza kuwa ameachia kiti hicho kwa hiari ili Kujenga
tabia ya kuachiana madaraka.
“Watu
tujenge umoja wa kukabidhi madaraka tusiwe ving'ang'anizi na huu utaratibu
niliamua kuujenga ili pasitokee mtu yeyote kutaka kuvuruga,” amesisitiza.
Katika
miaka 13 yake ya uongozi ameweza kuwaunganisha, mshikamano, amehamasisha kila
chifu kuweza kusimamia maadili, elimu afya kusimamia Mila na desturi na
mazingira.
Chifu Marealle akisoma hotuba yake wakati wa kukabidhi madaraka kwa hiari mnamo Oktoba 8, 2022 |
Hiki ni kisa cha kweli kilichomkuta kijana James mkazi wa mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro…Nani alimsaliti kijana huyu mwenye umri wa miaka 37 afike hapo alipofikia? ANKO TUNUNU anaanza katika sehemu ya kwanza ya makala haya…
Tulipokuwa shuleni tulikuwa tukifundishwa
methali, vitendawili, misemo na mambo kadha wa kadha. Katika kipengele cha
methali miongoni mwao ilikuwa ni “Hujafa, Hujaumbika”.
Maana yake halishi ni kwamba mwili wa binadamu
unaweza kubadilika kimaumbile wakati wowote angali akiwa hai.
Hivyo basi haifai kwa sababu yoyote ile
kumcheka, kumdhihaki au kumkejeli mtu ambaye ana ulemavu wa kiungo mwilini
mwake.
Aliyekufa ndio amekamilika, safari yake
imefika mwisho. Mfuatiliji wa makala haya utakubaliana name na methali hii kwa
asilimia mia moja, utapofuatilia kisa hiki cha kweli kilichompata kijana
anayefahamika kwa jina la James Severin Mushi (37) mkazi wa Moshi katika mkoa
wa Kilimanjaro.
Watu wengi hupewa sifa na heshima
wanazostahili wakishakufa.
Wakati wa uhai wao watu huwachukulia
"poa", hawautambui au kuuthamini mchango wao mpaka wakishakufa na
pengo lao kuonekana.
Watu wachache sana katika historia
walifanikiwa "kuumbika" angali wakiwa hai.
Kwa haraka watu wanaokuja kichwani ni kama
Nelson Mandela, Michael Jackson, Steven Hawkings, Muhammad Ali na wengineo.
Wapo pia wenye bahati zaidi ambao wanapewa
tuzo za heshima sana au kupendwa na mamilioni ya watu angali wakiwa hai kama
Barak Obama, Pele, Beyonce na kadhalika.
Kisa hiki cha kweli cha kijana James kinaanzia
katika kivuko cha waenda kwa miguu cha Karanga-Magereza mjini Moshi mnamo
Aprili 2003 majira ya saa 11 jioni wakati akitoka shule.
Wakati huo alikuwa akisomea katika shule ya
Ufundi ya Moshi masuala ya ufundi bomba (Plumbing).
James anasema, “Nakumbuka ilikuwa siku ya
Ijumaa mida ya saa 11 jioni katika kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Karanga
nikiwa na baiskeli basi lilinigonga.”
Muathirika huyo ambaye kwa sasa hana miguu
yake ya asili, alijikuta akiwa katika Hospitali ya KCMC iliyopo mjini Moshi
akiwa kwenye vitanda vya hospitali hiyo huku maumivu makali yakiendelea katika
mwili wake.
James anasema machozi yalizidi kutoka baada ya
kugundua kuwa maumivu makali sio pekee yamesababishwa na ajali kama ajali bali
ni baada ya taa ya mwili (macho) kuangaza katika mwili wake na kujikuta hana
miguu yote miwili.
“Baada ya kupelekwa hospitalini na kufika huko
miguu ilikuwa haina uwezo tena wa kutibika isipokuwa kukatwa…machozi yalinitoka
sikujua la kufanya,” anasimulia James.
ITAENDELEA…
Rais wa nne wa Kenya Uhuru Kenyatta amekabidhi madaraka kwa amani kwa Rais wa Tano wa taifa hilo William Ruto katika tukio lililofanyika katika Uwanja wa Moi-Kasarani jijini Nairobi.
Rais Ruto
ameapa kuitumikia Jamhuri ya Kenya kwa moyo mkunjufu na uaminifu mkubwa pasipo
kuwa na upendeleo wala ushawishi ili kulijenga taifa hilo.
Sambamba na
hilo Makamu wa Rais Gachagua naye amekula kiapo cha utii cha kulitumikia taifa
la Kenya.
Marais 20 wa
barani Afrika wamehudhuria sherehe hizo akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) na Mfalme Mswati III wa Eswatini.
Chama cha mchezo wa ngumi, Kanda ya Kaskazini (KBA),umepania
kuurejesha mchezo huo baada ya kipindi kirefu kupotea kutokana na
vijana wengi kutokujitokeza kushiriki pambano hilo.
Katibu wa mchezo wa Ngumi mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Taifa wa
maandalizi Ngumi Frank Francis, amesema hayo jana wakati wa uzinduzi wa mchezo
wa ngumi uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mawenzi mjini
Moshi mkoani Kilimanjaro
Amesema kutokana changamoto mbalimbali za kiutendaji kutoka kwa
baadhi ya viongozi wa mchezo huo, zilipelekea kupoteza ya sifa yake Kitaifa na
Kimataifa na kudidimiza maendeleo yake hapa nchini.
Francia ametumia fursa hiyo ya kuwataka vijana kujitokeza kwa
wingi kushiriki mchezo huo wa ngumi ambapo kwa sasa chama hicho kimeamua
kurejesha heshima ya mikoa hiyo ya Kanda ya Kaskazini.
“Ngumi ni miongoni mwa michezo ambayo imeitangaza na kuipa
heshima nchi yetu ya Tanzania duniani, kutokana na mabondia wake kuonyesha
uwezo mkubwa na kushinda katika mapambano mbalimbali ya Kimataifa,”amesema.
Amesema mchezo wa ngumi Kanda ya Kaskazini kwa kipindi kirefu
ulipotea baada ya vijana wengi kutojitokeza kushiriki pambano hilo na hivyo
wameamua kufufua na kuinua mchezo wa ngumi katika Kanda ya Kaskazini ili vijana
wengi waweze kushiriki mchezo huo.
Aidha ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau wa mchezo wa
ngumi kuwasaidia vijana walioonesha nia ya kucheza mchezo huo kupata
viwanja vya kufanyia mazoezi ya ngumi sanjari na kuwapatia vifaa vya mchezo
huo.
Naye Bondia mstaafu mkoa wa Kilimanjaro Emmanuel Mushi amesema
wameandaa pambano hilo la ngumi kimkoa ili kukuza vipaji vilivyopo ili
kuwasaidia vijana waweze kupata ajira
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa Chama cha Ngumi
Mkoa wa Kilimanjaro (KBA), Malonga Kitika amesema ukosefu wa viwanja vya mchezo
wa ngumi pamoja na upungufu wa vifaa vya mchezo huo, umekuwa chanzo kikubwa cha
vijana wengi kurudi nyuma kushiriki mchezo wa ngumi na kutoa wito kwa taasisi
za umma na binafsi kuwapatia maeneo yao ili waweze kufanyia mazoezi ya mchezo
huo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bomang’ombe Wilaya ya Hai Evod
Njau, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo, amewashauri madiwani
kuhakikisha kila kata wanayoiongoza kuhamasisha vijana chini ya umri mdogo
kuanza kushiriki mchezo wa ngumi ili taifa liweze kupata wachezaji bora ambao
wataweza kushindana na kuweza kuleta medani za mchezo huo.
Mchezo wa ngumi
ni miongoni mwa michezo inayofahamika na kupendwa na watu wengi duniani, kama
ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa miguu, mchezo huu umekuwa ni
chanzo cha ajira na hivyo kujipatia umaarufu mkubwa ambapo vijana wengi
wanajiunga kwa lengo la kujipatia kipato.
Mchezo wa ngumi
nchini Tanzania ulianza kufahamika katika miaka ya 1950 ambapo miaka ya 1970
mabondia wake walianza kufahamika katika mashindando mbalimbali ya Kimataifa.
Medali ya kwanza
ya Kimataifa ililetwa na Titus Simba mwaka 1974 katika michezo ya Jumuiya ya
Madola iliyofanyika nchini Uingereza na mwaka 1998 bondia mwingine Michael
Yombayomba aliiletea Tanzania medali nyingine katika mashindano hayo ya Jumuiya
ya Madola yaliyofanyika nchini Malaysia.
Afisa Uhusiano wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi kuhusu maboresho yaliyofanyika tangu mwaka 2019 hadi sasa |
Uwekezaji wa bilioni 429.1 kwa ajili ya uboreshaji
wa bandari ya Tanga umeanza kuzaa matunda baada ya mkandarasi kukabidhi ujenzi
wa wa gati wenye urefu wa mita 200 ambao utaruhusu bandari hiyo kongwe kuhudumia
meli zisizozidi mita 200 gatini kwa wakati mmoja.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliamua kutenga kiasi hicho cha fedha ili kutekeleza mradi mkubwa na wa kimkakati katika bandari ya Tanga ambao unatekelezwa kwa awamu mbili.
Nchi
jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimeanza
kutumia bandari ya Tanga kupitishia mizigo yake kutokana na maboresho ya
bandari hiyo yanayoendelea ya upanuzi wa bandari hiyo, huku nchi nyingi zaidi
zikitarajiwa kutumia bandari hiyo.
Rwanda imeanza kutumia bandari hiyo kupitishia malighafi inayotumika kutengenezea saruji huku nchi ya Burundi ikipitisha mzigo wa mafuta kupitia bandari hiyo.
Mnamo mwanzoni mwa Agosti mwaka huu mkandarasi
ambaye ni kampuni ya China Harbour Engineering (CHEC) Limited alikabidhi
kipande cha urefu wa mita 200 hivyo kufanya uboreshaji wa bandari hiyo kufikia asilimia 61.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi Afisa Uhusiano wa Bandari ya Tanga
Peter Milanzi amesema mradi huo uliwekwa katika awamu mbili za utekelezaji
ambapo awamu ya kwanza ilijikita katika uchimbaji wa kina cha maji kwenye
mlango wa kuingilia meli na shemu ya
kugeuzia meli kutoka mita tatu hadi mita 13.
“Aidha licha ya uchimbaji huo, ununuzi wa mitambo ya
bandari (operational equipment) kwa gharama ya shilingi 172.3 bilioni
ulifanyika,” amesema.
Awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi umegharimu
shilingi 256.8 bilioni na utadumu kwa miezi 22 ulioanza Septemba 5, 2020 na
unatarajiwa kumalizika Novemba 28, 2022.
“Awamu ya pili unahusisha ujenzi wa gati mbili zenye
urefu wa mita 450 na kuongeza kuchimba kina cha maji kutoka mita tatu hadi 13
wakati wa maji kupwa
Bandari
ya Tanga ni ya namna gani?
Bandari ya Tanga ni bandari kongwe iliyojengwa
katika Pwani ya Afrika Mashariki na kuanza kufanya kazi mwaka 1891 wakati wa
utawala wa Wajerumani katika ardhi ya Afrika Mashariki.
Bandari ya Tanga ni ya pili kwa ukubwa katika
kuhudumia shehena baada ya bandari ya Dar es Salaam. Bandari ya Tanga ina uwezo wa kuhudumia
shehena ya jumla ya tani 750,000 kwa mwaka ikijumuisha mzigo mchanganyiko,
shehena ya mafuta pamoja na shehena ya makasha kwa mwaka
Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imeweza kuvuka lengo
kwa kuhudumia jumla ya Tabi 870,000, hata hivyo hayo ni matokeo ya awali mara
baaada ya uwekezaji mkubwa wa uboreshaji wa bandari ya Tanga tangu mwaka 2019.
Tangu kujengwa kwake, bandari ya Tanga ilikuwa
inahudumia shehena katika kina kirefu cha maji eneo la umbali wa mita 1700 kutoka
gatini kwasababu ya changamoto ya kina kifupi cha maji eneo la gati ambapo kina
cha maji kilikuwa mita tatu hali iliyofanya meli zishindwe kufika kwenye gati.
Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliamua kutenga kiasi cha shilingi
429.1 bilioni ili kutekeleza mradi mkubwa na wa kimkakati katika bandari ya Tanga ambao unatekelezwa
kwa awamu mbili.
TPA
imejipanga vipi na bandari kavu ya Arumeru?
Kuhusu
ujenzi wa Bandari kavu katika eneo la Malula wilayani Arumeru, ujumbe huo wa
bandari ya Tanga umesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
imetenga bajeti ya fedha ya kufanya upembuzi yakinifu katika mwaka huu wa fedha
2022/23.
Ujumbe
wa kueleza uboreshaji uliofanyika katika bandari ya Tanga uliongozwa na Afisa Uhusiano Peter Milanzi, Afisa Masoko
Mkuu Rose Tandiko na Mhandisi wa Bandari hiyo,Hamis Kipalo.
Mikoa
ya Arusha na Kilimanjaro imekuwa wanufaika na ziara hiyo ya taarifa ya maboresho
ya bandari ya Tanga tangu mwaka 2019.
Afisa Masoko Mkuu wa Bandari ya Tanga Rose Tandiko akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matunda yaliyoanza kupatikana baada ya uwekezaji wa shilingi 429.1 bilioni bandari hapo. Mhandisi wa Bandari ya Tanga Hamisi Kapilo
Hecton Chuwa, mwandishi wa Daily News akiuliza swali kwa ujumbe wa TPA Bandari ya Tanga uliofika mjini Moshi kuzungumza na waandishi wa habari. |
Bahati M. Nyakiraria, Mwenyekiti wa Kilimanjaro Press Club (MECKI) akizungumza na ujumbe wa Bandari ya Tanga