Tuesday, December 20, 2022

MAKTABA YA JAIZMELA: Ifahamu Christmas

 

Tunaposema MERRY CHRISTMAS Maana yake ni FURAHA YA KUSANYIKO LA WAKRISTO.

Kwa hiyo hakuna mahusiano baina ya Christmas na kuzaliwa kwake Yesu Kristo Desemba 25. katika hili wala tusimung'unye maneno.

Nyakati zile Dola ya Rumi ilipokuwa ikitawala dunia walikuwa wana miungu yao ambayo iliabudiwa kila siku na Desemba 25 kila mwaka walifanya sherehe ya kuitukuza miungu yao hiyo.

MAJINA YA SIKU NA MIUNGU ILIYOABUDIWA

>Jumatatu (Monday) inatokana na moon day, kwa wapagani wa nyakati zile ilimaanisha siku ya kumwabudu mungu moon (mwezi).

>Jumanne (Tuesday) – inatokana na tiw’s day, kwa wapagani wa nyakati zile ilimaanisha ni siku ya mungu Tiw.

>Jumatano (Wednesday) – inatokana na wedn day au woden day, kwa wapagani ilimaanisha siku ya mungu wedn au woden.  

>Alhamisi (Thursday) - inatokana na ,,thor day,, kwa wapagani ilikuwa ni siku ya kumwabudu mungu thor.

 >Ijumaa (Friday) - inatokana na ,,frig day au freia day,, kwa wapagani ilikuwa ni siku ya

mungu frig au freia.  

>Jumamosi (Saturday) – inatokana na Saturn day (siku ya sayari zohari), kwa wapagani

ilikuwa ni siku ya kumwabudu mungu wa Kirumi aitwaye ,,Saturn,, yaani kwa Kiswahili

sayari ya zohari. 

>Jumapili (Sunday) –ilitokana na sun day (siku ya jua), kwa wapagani waKirumi ilikuwa ni

siku ya kumwabudu mungu sun (jua).


Kwa ujumla, Siku zote za juma, Warumi walizipa majina ya miungu yao, kwa sababu hao

kwa kipindi hicho ndiyo walikuwa watawala dunia kwa wakati huo. 

Katika miungu yote iliyotajwa hapo juu, mungu mkuu alikuwa ni mungu jua (sun) wao walimuita ni mungu asiye shindwa.

Hata baada ya utawala wa Dola ya Kirumi kuvunjika na nchi kuanza kujitawala bado watu kutoka mataifa mbalimbali waliendelea kuikumbuka miungu hiyo kila ifikapo Desemba 25 kila mwaka, na wengine walifunga safari kwena Mjini Rome Italia kushereheke sikukuu hizo za miungu ambazo hazikufahamika kwa jina la CHRISTMAS.

Hata warumi wenyewe waliposherehekea sikukuu hizo hawakuziona kuwa ni SIKUKUU ZA KIPAGANI maana walijiona wako sahihi (njia ya mtu ni njema machoni pake mwenyewe).

 CHRISTMAS.

Miaka ilivyozidikuendelea mbele ndipo baadhi ya watu waliopata kuifahamu kweli wakatambua hawakuwa sahihi kuendelea kuitumikia miungu ya kirumi wakati yupo Mungu muumba wa mbingu na nchi. Na hapo ndipo CHRISTMAS ilipoanzishwa. 

Lengo kuu la kuianzisha sikukuu ya christmas lilikuwa ni kuvunja nguvu au kufuta kabisa zile sherehe za kuiabudu au kuitukuza miungu ya kirumi kila Desemba 25 ya kila mwaka na ndio maana hata Christmas ilipoanzishwa ikapangwa katika tarehe sawa na sikuku ile ya kuiabudu miungu ya rumi.

Katika sherehe za Christmas watu walikuwa wakipokea zawadi kama vile nguo na vyakula nk, lakini katika zile sherehe za miungu ya ya warumi watu walikuwa wakiitolea zawadi ile miungu waliyoiabudu na huo ndio mwanzo wa Father Christmas. 

Hali hiyo iliwafanya watu kuanza kuyaendea makusanyiko yaliyopewa jina la Christmas na kusahau kuindea ile miungu yao kwa kuwa christmas ilitumika kwa matendo mema na ya faraja. 

Katika sherehe za Christmas watu walifundishwa matendo mema kwa kuwasaidia wahitaji kwa kuwapelekea zawadi kwa kunukuu maandiko kwamba hata Yesu Kristo alipozaliwa watu walipeleka zawadi zao. 

Hapo ndipo Christmas ilipoanza kuhusishwa na KUZALIWA KWA YESU KRISTO jambo ambalo ni kinyume na uhalisia wa maana ya jina au neno CHRISTMAS. 

Neno Christmas halipatikani popote katika biblia hata ukisoma kitabu cha MWANZO mpaka UFUNUO WA YOHANA huwezi kuliona neno Christmas. 

Pia huwezi kuizungumzia Christmas kwa maana ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo huku ukiwa umeshika Biblia mkononi kwa kuwa hakuna andiko litakalo kusapoti hoja zako. 

Kuamini CHRISTMAS ni kuzaliwa kwa Yesu Kristo huku ni kuamini kusiko sahihi.

 

KUZALIWA KWA YESU KRISTO. 

Biblia imekaa kimya kabisa kuhusiana na tarehe na mwezi na hata mwaka aliozaliwa Yesu Kristo, hata Yesu mwenyewe hakuwahi kuwaambia mitume na manabii wa nyakati zake kuhusiana na tarehe halisi ambayo yeye alizaliwa, na hata wanafunzi wake hawakuwahi kudadisi dadisi kuhusu jambo hilo. 

Hata kama mitume na manabii wa nyakati za Yesu wangepata kufahamu tarehe halisi aliyozaliwa Bwana Yesu, kuifahamu tarehe hiyo kusingeweza kuwa na msaada wowote katika maisha yao ya kiroho. 

Mtu yeyote anapokombolewa vitani baada yakuwa ameshikiliwa mateka kwa muda mlefu, atakachokifurahia mtu huyo ni tendo la kukombolewa kwake pomoja na jina la komandoo aliyemuokoa ili apate kushukuru kwa ujasiri wake, maana tarehe ya kuzaliwa kwa komandoo huyo wala hainamsaada kwake hata kama ataifahamu. 

LUKA 1:31, imeandikwa Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume, na jina lake utamwita jina lake Yesu. 

Huu ni ujumbe wa Malaika Gabrieli kwenda kwa Marimu na ilikuwa ni mwezi wa sita (6). 

Ujumbe unasema UTACHUKUA MIMBA, sio unachukua mimba. 

Maana kama ujumbe ungesema UNACHUKUA MIMBA, nayo ilikuwa ni mwezi wa sita, basi Yesu alifaa azaliwe mwezi wa tatu (sio wa kumi na mbili) hii ni kulingana na muda uaotakikana kwa mwanadamu kubeba mimba mpaka kuzaa mwana. 

Kwahiyo kwasababu ujumbe wa Malaika ulisema Tazama utachukua Mimba, hivyo haikuwekwa wazi kwamba hiyo mimba mariamu aliipata mwezi wa ngapi, maana ujumbe ni UTACHUKUA MIMBA na sio unachukua mimba. 

Hakuna mtume wala nabii yeyote aliyewahi kuikumbuka au kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo, hata Yesu mwenyewe hakuwahi kuagiza hayo.

MAFANIKIO YA KUANZISHWA KWA CHRISTMAS. 

Kama nilivyosema hapo awali kwamba, lengo la kuanzishwa kwa Christmas lilikuwa ni kuvunja na kuondoa kabisa zile sikukuu za kuabudu miungu ya kipagani ya kirumi, kwa kuianzisha christmas katika tarehe ileile ambayo wapagani wa kirumi waliitumia kuiabudu miungu yao, ndiomaana leo hii sherehe za kuiabudu miungu ya kirumi imebaki kuwa ni historia tu badala yake kila mtu anaifahamu Christmas kama ndio siku ya kuzaliwa Yesu Kristo (japo si kweli)

0 Comments:

Post a Comment