Tuesday, December 20, 2022

KDF yarahisisha mawasiliano Jeshi la Polisi


ACP Simon Maigwa 

Mwishoni mwa miaka ya 1970, mjasiriamali na mgunduzi wa mfumo wa simu za kiganjani nchini Marekani Martin Cooper alisema, “Tulijua kuwa watu hawapendi kuzungumza ndani ya magari, au  nyumba; au maofisini wanataka kuzungumza na watu wengine…Tulichokuwa tukiaminini kwamba namba ya simu inatakiwa kuwa ya mtu binafsi badala ya kuwepo eneo fulani.” 

Majaribio ya Cooper na wagunduzi wengine yameifanya dunia kwa sasa kuwa ya kipekee, mtu aweza kuwasiliana binafsi na mtu mwingine na wakazungumza ajenda zao za binafsi kwa wakati wowote. 

Hivyo ndivyo wadau wa maendeleo mkoani Kilimanjaro (KDF)  walivyoona fursa kupitia kampuni ya simu nchini Vodacom kwa namna gani wanaweza kurahisisha mawasiliano miongoni mwa Maofisa wa Jeshi la Polisi hivyo kuifanya kazi ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuwa nyepesi. 

Ilianzia hapa pale KDF ilipofanya makubaliano na Vodacom na kukubaliana nao kuwapa Polisi na wafanyakazi wote wa Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro namba za Vodacom ili waweze kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe bure. 

Hatua hiyo inawafanya maofisa wa Polisi kupunguza gharama za mawasiliano miongoni mwao, kupitia mfumo wa Closed User Group (CUG) ambapo mfumo huo ni maalum kwa maofisa hao pekee. 

Tukio hilo la makabidhiano ya laini za simu limefanyika Desemba 19,2022 mjini Moshi katika ukumbi wa mikutano wa Kili Wonders. 

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro( ACP) Simon Maigwa amesema zoezi hili litaimarisha mawasiliano baina Askari na Askari katika utendaji wa kazi za Askari za kila siku. 

“Niwapongeze sana KDF kwa kuleta wazo hili ambalo limehusisha Kampuni ya Vodacom PLC,Chief Premium Beer, na Jeshi la Polisi.Ni hatua kubwa kwakweli na hili itarahisisha utendaji kazi kwa Askari wetu,Gharama hazitakuwepo hivyo mawasiliano yatafanyika kwa urahisi na kazi zetu pia zitaenda ukizingatia pia mawasiliano ni muhimu sana katika kazi zetu hizi,”    amesema  ACP Maigwa.

Aidha mjumbe wa KDF Rashid Tenga amesema zoezi hilo ni endelevu na halitadumu katika msimu huu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka. 

“Tutatoa Dk 300 za muda wa maongezi kwa shilingi Elfu mbili pekee mwezi mzima kwa askari wetu na zoezi hili ni endelevu, Iwapo kutakuwa na uhitaji zaidi wa huduma hii katika msimu wa sikukuu n.k tutaona namna ya kufanya,Hata hivyo tutaangalia pia uwezekano wa sekta nyingine kupatiwa huduma hii.,” 

“Tumeanza na wenzetu wa Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro na lengo kubwa ni kuhakikisha tunarahisisha mawasiliano na kufanya utendaji kazi wao kuwa rahisi zaidi.,mafanikio tutakayo yapata ndio yatasababisha tuangalie namna ya kuingia pia katika mikoa mingine,” ameongeza Tenga.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Kilimanjaro akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Abbas Kayanda.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Abbas Kayanda




0 Comments:

Post a Comment