Afisa Uhusiano wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi kuhusu maboresho yaliyofanyika tangu mwaka 2019 hadi sasa |
Uwekezaji wa bilioni 429.1 kwa ajili ya uboreshaji
wa bandari ya Tanga umeanza kuzaa matunda baada ya mkandarasi kukabidhi ujenzi
wa wa gati wenye urefu wa mita 200 ambao utaruhusu bandari hiyo kongwe kuhudumia
meli zisizozidi mita 200 gatini kwa wakati mmoja.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliamua kutenga kiasi hicho cha fedha ili kutekeleza mradi mkubwa na wa kimkakati katika bandari ya Tanga ambao unatekelezwa kwa awamu mbili.
Nchi
jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimeanza
kutumia bandari ya Tanga kupitishia mizigo yake kutokana na maboresho ya
bandari hiyo yanayoendelea ya upanuzi wa bandari hiyo, huku nchi nyingi zaidi
zikitarajiwa kutumia bandari hiyo.
Rwanda imeanza kutumia bandari hiyo kupitishia malighafi inayotumika kutengenezea saruji huku nchi ya Burundi ikipitisha mzigo wa mafuta kupitia bandari hiyo.
Mnamo mwanzoni mwa Agosti mwaka huu mkandarasi
ambaye ni kampuni ya China Harbour Engineering (CHEC) Limited alikabidhi
kipande cha urefu wa mita 200 hivyo kufanya uboreshaji wa bandari hiyo kufikia asilimia 61.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi Afisa Uhusiano wa Bandari ya Tanga
Peter Milanzi amesema mradi huo uliwekwa katika awamu mbili za utekelezaji
ambapo awamu ya kwanza ilijikita katika uchimbaji wa kina cha maji kwenye
mlango wa kuingilia meli na shemu ya
kugeuzia meli kutoka mita tatu hadi mita 13.
“Aidha licha ya uchimbaji huo, ununuzi wa mitambo ya
bandari (operational equipment) kwa gharama ya shilingi 172.3 bilioni
ulifanyika,” amesema.
Awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi umegharimu
shilingi 256.8 bilioni na utadumu kwa miezi 22 ulioanza Septemba 5, 2020 na
unatarajiwa kumalizika Novemba 28, 2022.
“Awamu ya pili unahusisha ujenzi wa gati mbili zenye
urefu wa mita 450 na kuongeza kuchimba kina cha maji kutoka mita tatu hadi 13
wakati wa maji kupwa
Bandari
ya Tanga ni ya namna gani?
Bandari ya Tanga ni bandari kongwe iliyojengwa
katika Pwani ya Afrika Mashariki na kuanza kufanya kazi mwaka 1891 wakati wa
utawala wa Wajerumani katika ardhi ya Afrika Mashariki.
Bandari ya Tanga ni ya pili kwa ukubwa katika
kuhudumia shehena baada ya bandari ya Dar es Salaam. Bandari ya Tanga ina uwezo wa kuhudumia
shehena ya jumla ya tani 750,000 kwa mwaka ikijumuisha mzigo mchanganyiko,
shehena ya mafuta pamoja na shehena ya makasha kwa mwaka
Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imeweza kuvuka lengo
kwa kuhudumia jumla ya Tabi 870,000, hata hivyo hayo ni matokeo ya awali mara
baaada ya uwekezaji mkubwa wa uboreshaji wa bandari ya Tanga tangu mwaka 2019.
Tangu kujengwa kwake, bandari ya Tanga ilikuwa
inahudumia shehena katika kina kirefu cha maji eneo la umbali wa mita 1700 kutoka
gatini kwasababu ya changamoto ya kina kifupi cha maji eneo la gati ambapo kina
cha maji kilikuwa mita tatu hali iliyofanya meli zishindwe kufika kwenye gati.
Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliamua kutenga kiasi cha shilingi
429.1 bilioni ili kutekeleza mradi mkubwa na wa kimkakati katika bandari ya Tanga ambao unatekelezwa
kwa awamu mbili.
TPA
imejipanga vipi na bandari kavu ya Arumeru?
Kuhusu
ujenzi wa Bandari kavu katika eneo la Malula wilayani Arumeru, ujumbe huo wa
bandari ya Tanga umesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
imetenga bajeti ya fedha ya kufanya upembuzi yakinifu katika mwaka huu wa fedha
2022/23.
Ujumbe
wa kueleza uboreshaji uliofanyika katika bandari ya Tanga uliongozwa na Afisa Uhusiano Peter Milanzi, Afisa Masoko
Mkuu Rose Tandiko na Mhandisi wa Bandari hiyo,Hamis Kipalo.
Mikoa
ya Arusha na Kilimanjaro imekuwa wanufaika na ziara hiyo ya taarifa ya maboresho
ya bandari ya Tanga tangu mwaka 2019.
Afisa Masoko Mkuu wa Bandari ya Tanga Rose Tandiko akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matunda yaliyoanza kupatikana baada ya uwekezaji wa shilingi 429.1 bilioni bandari hapo. Mhandisi wa Bandari ya Tanga Hamisi Kapilo
Hecton Chuwa, mwandishi wa Daily News akiuliza swali kwa ujumbe wa TPA Bandari ya Tanga uliofika mjini Moshi kuzungumza na waandishi wa habari. |
Bahati M. Nyakiraria, Mwenyekiti wa Kilimanjaro Press Club (MECKI) akizungumza na ujumbe wa Bandari ya Tanga
0 Comments:
Post a Comment