Mwandishi wa vitabu Salman Rushdie, ambaye amekuwa mafichoni baada kuamuliwa kuuawa na hukumu ya sheria ya dini ya Kiislamu Fatwa ya Iran, anapumulia mashine hospitalini na anaweza kupoteza jicho moja baada ya kushambuliwa jana jijini New York, Marekani.
Mwandishi huyo wa Uingereza wa kitabu cha "aya za shetani"
ambacho kilizusha ghadhabu miongoni mwa baadhi ya nchi za Kiislamu walioamini
kuwa ni kufuru, ilibidi asafirishwe kwa ndege hadi hospitali kwa ajili ya
upasuaji wa dharura kufuatia shambulio hilo.
Mshambuliaji alipanda kwenye jukwaa ghafla na kumchoma visu shingoni na
tumboni kabla ya watu waliokuwa ukumbini kukimbilia jukwaani na kumdhibiti
mshambuliaji.
Kitabu chake cha "aya za shetani alichokitoa mwaka 1988 kilichukuliwa na baadhi ya Waislamu kama dharau kwa dini hiyo na Mtume Mohammed.
Kitabu cha ‘Aya za Shetani’ kikoje?
The Satanic Verses ni riwaya
iliyotungwa mnamo mwaka 1988 na mwandishi mwenye asili ya India raia wa
Uingereza Salman Rushdie. Kitabu hicho
kilitungwa na kuonyesha maisha ya Mtume wa Dini ya Kiislam Muhammad
(S.A.W).
Rushdie alionyesha wasifu kwa
kutumia aya za Koran akiwajumuisha miungu watatu wa Makka; Allāt, Al-Uzza, na
Manāt. Aidha upande mwingine wa riwaya hiyo ilitumia taarifa za wanahistoria wa
kale al-Waqidi na al-Tabari.
Nchini Uingereza kilipokea
tuzo mbalimbali ikiwamo ya mwaka 1988 Whitbread baada ya kushindwa kutwaa tuzo
ya Booker ya mwaka 1988 licha ya kufika fainali ikipitwa na ile ya Peter
Carey's Oscar na Lucinda.
Waislamu wanaichukulia riwaya
hiyo kuwa inakufuru dini ya Uislamu na Mtume Muhammad SAW.
Nchini India kilipigwa
marufuku kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kauli za chuki dhidi ya Uislamu.
0 Comments:
Post a Comment