Rais wa Kolombia, Gustavo Francisco Petro Urrego |
Rais wa kwanza wa Colombia mwenye siasa za mrengo wa kushoto Seneta Gustavo Petro, ameapishwa rasmi mnamo Agosti 7, 2022 kuliongoza taifa hilo la Amerika ya Kusini.
Petro, ambaye ni mwanachama wa zamani wa kundi la waasi la
M-19 alishinda uchaguzi wa Urais mnamo mwezi Juni kwa kuvibwaga vyama vya
kihafidhina ambavyo vilipoteza ushawishi kwa wapiga kura.
Mara baada ya kuapishwa, Petro, ameapa kupambana na ukosefu
wa usawa na kuleta mabadiliko makubwa katika taifa hilo lililokumbwa na vita ya
muda mrefu baina ya serikali na vikundi vya waasi.
Petro ni sehemu ya kundi linalozidi kushamiri la wanasiasa wa
mrengo wa kushoto ambao wamekuwa wakishinda uchaguzi katika kanda ya ya Amerika
ya Kusini tangu kuzuka kwa janga la Corona na kuwashinda marais waliokuwa
madarakani ambao wameshindwa kushughulikia athari mbaya za kiuchumi.
GUSTAVO
FRANCISCO PETRO URREGO
Jina lake kamili ni Gustavo Francisco Petro Urrego, mzaliwa
wa Ciénaga de Oro, nchini Kolombia. Alizaliwa mnamo Aprili 19, 1960. Huyu ni
mpiganaji wa zamani wa msituni pia msomi wa masuala ya uchumi na siasa.
Katika uchaguzi uliompa kukalia kiti hicho alimpiku Rodolfo
Hernández Suárez katika mzunguko wa pili wa uchaguzi wa Rais wa taifa hilo la
AMerika ya Kusini mnamo Juni 19, 2022.
Gustavo Francisco Petro Urrego anakuwa Rais wa kwanza kutoka mrengo wa kushoto
kuliongoza taifa hilo.
Akiwa na umri wa miaka 17, alijiunga na jeshi la ukombozi la
msituni la 19th of April Movement, (M19) na baadaye kuunda kuunda Chama cha Kidemokrasia cha Colombia
Humana.
Mnamo mwaka 2011 Gustavo Francisco Petro Urrego alichaguliwa
kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Bogota. Katika uchaguzi wa Rais wa mwaka 2018 Gustavo
Francisco Petro Urrego alishika nafasi ya pili akiwa na zaidi ya asilimia 25 ya
kura mnamo May 27, 2018 na kasha alipoteza katika mzunguko wa pili wa uchaguzi
huo mnamo Juni 17.
0 Comments:
Post a Comment