Rais mteule wa Kenya William Ruto ameshinda uchaguzi ambao ulikuwa na ushindani mkali katika historia ya Kenya.
William Ruto alimshinda mpinzani wake aliyekuwa waziri mkuu
Raila Odinga ambaye alikuwa anawania urais kwa mara ya tano.
Ruto
alishinda kwa asilimia 50.49 ya kura huku Odinga akiachwa kwa asilimia mbili
tu.
Uchaguzi huo hata hivyo ulifanyika wakati ambapo taifa hilo lenye uchumi mkubwa Afrika mashariki linakabiliwa na gharama kubwa ya maisha na ukosefu wa ajira, masuala ambayo wagombea wote wakuu walikuwa wameahidi kuyaangazia.
William
Ruto, ni miongoni mwa wanasiasa wengi wakubwa nchini Kenya walioweka wazi nia
zao za kuingia Ikulu ya Kenya, kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, kurithi
mikoba ya aliyekuwa 'swahiba wake', Uhuru Kenyatta.
Mwanasiasa huyu tajiri ambaye amekuwa na ndoto za kuwa Rais wa Kenya, amekuwa akikutana na vikwazo lukuki vya kisiasa, ikiwemo kuzuiwa kwa sababu ama kuzuiwa kwa makusudi kufanya shughuli kadhaa za kisiasa na binafsi kutokana na msukumo wa kisiasa.
Ni miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini humo, walioweka wazi nia zao za kuingia Ikulu ya Kenya, kupitia uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022, kurithi mikoba ya 'swahiba wake', Uhuru Kenyatta.
0 Comments:
Post a Comment