Wapiga kampeni wa wagombea wakuu kwenye uchaguzi huo William
Ruto na Raila Odinga wanatumia mitandao kusambaza taarifa za shutuma dhidi ya
mahasimu wao kwamba wanashiriki kwenye visa vya udanganyifu.
Mashirika ya kiraia nchini Kenya yameonya kwamba taarifa hizo potofu zinahatarisha demokrasia na yameyataka majukwaa ya mitandao ya kijamii kuchukua hatua.
Wakenya watapiga kura ya kumchagua Rais, wabunge na viongozi
wengine kesho Jumanne Agosti 9.
Mshindi katika uchaguzi huo atamrithi Rais Uhuru Kenyatta
anayemaliza muda wake.
Wachambuzi wanasema ushindani ni mkali kati ya wagombea
wawili wakuu na kwamba kwa mara ya kwanza Kenya inaweza kuingia katika duru ya
pili ya uchaguzi.
0 Comments:
Post a Comment