Kasi ya
mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yamewafikiwa wakulima wa kahawa mkoani
Kilimanjaro kwa kuunganishwa na matumizi ya mtandao na simu kwa upataji na
utoaji wa taarifa mbalimbali kuhusu zao hilo kupitia ‘Farming Solution App’.
Akizungumza
katika semina hiyo ya siku moja mjini Moshi na watalaamu na maafisa ugani Meneja
Mradi wa Solidaridad Mary Mkonyi alisema “Kama sekta tumepata changamoto kubwa za
taarifa sahihi za uzalishaji, taarifa sahihi za biashara, taarifa sahihi za
masoko katika ngazi ya taifa, kama sekta kiongozi tukasema tunataka sasa taarifa
sahihi za mkulima, biashara ya kahawa ambapo itasaidia sisi kama wadau wajue ni
kwa kiasi gani wanaweza kuwekeza nchini.”
Pia Mkonyi
aliongeza kuwa baada ya mradi huo kufanya vizuri katika bara la Amerika Kusini
wameona sasa ni zamu ya wakulima wa kahawa mkoani Kilimanjaro. “Bado
tunashughulika na wakulima 10,000 lakini program hii itakapokuwa tayari
tutachukua wakulima 1,000 ili kuona namna unavyofanya kazi na changamoto zake kisha
nchi nzima,” aliongeza Mkonyi.
Meneja Mradi wa
Solidaridad Mary Mkonyi akiwa kwenye mahojiano na Jaizmelanews
Aidha Magese alisema program hiyo inaweza kufanya kazi kwenye mazingira yasiyo na intaneti kisha baadaye mkulima akamalizia kwa kutumia intaneti.
“Utafiti wa
mwaka 2018 wa ‘The Mobile Economy, GSM Association’
ulionyesha kwa mwaka 2017 watu wanaotumia mtandao ni asilimia 21, aidha utafiti
huo ulionyesha hadi ifikapo mwaka 2025 idadi ya watu wanaotumia mtandao
litafikia asilimia 40. Pia utafiti huo ulionyesha kuwa mwaka 2017 asilimia 44
ya watu walikuwa wanatumia simu na kwamba ifikapo mwaka 2025 itafikia asilimia
52,” aliongeza Magese.
“Inamsaidia
mkulima kujifanyia tathmini yeye
mwenyewe na kujipatia mpangokazi wa shamba lake
hivyo michango yao itaweza kusaidia nini iweze kuboreshwanini kiweze
kuondolewa na nini kiweze kuwekwa, imegusa kila upande,” alisema afisa huyo.
Afisa Mradi wa
Solidaridad Erick Mlimba akitoa maelekezo kuhusu application kwa maafisa ugani
na wataalamu wa zao la kahawa.
Afisa
Maendeleo Bodi ya Kahawa Tanzania Kanda ya
Kaskazini Godfrey France alisema, “Ni program ambayo ni nzuri, vijana
wengi wanakaa katika masuala ya kiteknolojia na itakuwa inawahamasisha kukipenda
kilimo, Haitamlazimisha masaa yote kuwa shambani anaweza akawa anaishi mjini na ikampa notification
na akaelekeza mtu aliyepo shambani na akafanya kile alichokuwa akikifiri.”
Gazeti la Tanzanite ukurasa wa 8, Machi 27, 2019. |
Story by:
Kija Elias, Jabir Johnson
0 Comments:
Post a Comment