Mei 29,
1827 alizaliwa mtu aliyefahamika kwa jina la John Macadam katika kitongoji cha
NorthBank jijini Glasgow nchini Scotland. Macadam alizaliwa katika familia ya
mfanyabiashara na mmiliki wa kiwanda cha nguo na uchapishaji katika eneo la
East Ayrshire huko Kilmarnock.
Matunda ya Macademia yakiwa kwenye mti wake |
Kwa
mwonekane mtoto huyo kadri alivyokuwa akikua alionekana umbo lake halisi kuwa
ni mrefu kwa kimo, nywele ndefu za rangi nyekundu, kidevu kikiwa kimesheheni
ndevu na sauti nzito. Katika maisha yake yote alikuwa akihimiza umakini.
Matunda za Macademia |
Septemba 2, 1865 alifariki dunia akiwa amekaa miaka 10 katika ardhi hiyo. Macadam alikuwa msomi, mwanasiasa na mkemia hivyo alikuwa na ushawishi mkubwa ndani na nje ya Ulaya.
Macadam
alikuwa na rafiki yake raia wa Ujerumani Dkt. Ferdinand Mueller (1825-1896)
ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Royal Botanic Gardens jijini Melbourne nchini
Australia.
Dkt. Mueller ndiye aliyegundua mmea wa Macademia ambao kwa lugha ya Kiswahili unafahamika kwa jina la Karanga Miti. Mwaka 1857 aligundua hivyo kwa heshima aliamua kuupa jina kwa heshima ya rafiki yake.
Dkt. Mueller ndiye aliyegundua mmea wa Macademia ambao kwa lugha ya Kiswahili unafahamika kwa jina la Karanga Miti. Mwaka 1857 aligundua hivyo kwa heshima aliamua kuupa jina kwa heshima ya rafiki yake.
Dkt. John
Macadam kutokana na ushawishi wake kwenye taasisi yao nchini humo. Kwa ujumla
wake mmea huu uligunduliwa na matajiri wa mashamba barani Ulaya ambao baadaye
walikuja kusambaa duniani na kila walipoenda walifanikiwa kuupanda.
Hivyo
Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo ambayo yalikutwa na neema hiyo ya wahamiaji
hawa kutokana walipofika walianza kumiliki maeneo makubwa kwa ajili ya ardhi na
kuanza kulima kahawa ambapo waliendelea kupanda miti hiyo kama kivuli.
KWANINI
MACADEMIA KILIMANJARO?
Zamani
ilionekana kahawa ndio zao pekee lililo ghali ambalo linaweza kuleta faida
kubwa lakini katika tafiti mbalimbali zinaonyesha makademia inaweza kubadili
maisha ya wakulima zaidi ya ilivyo kahawa.
Wawekezaji
wazawa wameliona hilo na kuamua kuanza kubadilika taratibu ili kukabiliana na
soko na maisha. Mwekezaji wa Tudeley Estates Limited Jensen Natai alisema,
Mimea ya Macademia katika Tudeley Estates LImited mkoani Kilimanjaro |
“Tumeanza majaribio ya kuona kama linaweza kuleta faida ikilinganishwa na kahawa lakini kwa maelezo ya awali ni zao ambalo lina protini kubwa kuliko hata ya korosho na karanga pia utunzaji wake ni mwepesi kuliko hata wa kahawa.”
Macademia
ni mmea ambao unaanza kuzaa baada ya miaka mitano kisha uvunaji wake utadumu
kwa miaka hadi 30. Natai aliongeza kuwa Macademia katika majaribio yao
wamepanda miti 1,000 ambayo ikishakomaa soko lake kubwa ni barani Ulaya.
“Soko
lake haliyumbi kama ilivyo kahawa pia urahisi wake ni kwamba linaweza
kuchanganyikana na kahawa, linazuia upepo mkali,” alisema Natai. Pia Natai
aliongeza kuwa nchi za Afrika Kusini na Zimbabwe ni zao muhimu na hutoa ajira
sio chini ya 200.
0 Comments:
Post a Comment