BIBLIA inasema kwamba ngamia
walikuwa kati ya wanyama wa kufugwa ambao Farao alimpa Ibrahimu.
Mzee Dahir Jama Yusuf akiwa na mtoto wake Ahmed kwenye zizi la Ngamia Machi 20, 2019. |
Wasomi
wamebishana kuhusu usahihi wa kihistoria wa habari hiyo kuhusu ngamia kwa
sababu wengi wao wanaamini kwamba wanyama hao walianza tu kufugwa katika sehemu
nyingi karibu mwaka wa 1200 K.K., miaka mingi baada ya siku za Ibrahimu.
Kwa
hiyo, inaweza kuonekana kwamba maandiko yoyote ya Biblia yaliyotaja ngamia si
sahihi kwa sababu ngamia hawakutumiwa hivyo katika vipindi vinavyotajwa katika
masimulizi hayo ya Biblia.
Hata hivyo, wasomi wengine wanadai kwamba ingawa
ngamia walianza kufugwa kwa wingi karibu mwisho wa miaka elfu mbili ya kwanza
K.K., hilo halimaanishi kwamba ngamia hawakutumiwa kabla ya hapo. Katika kitabu
cha Mwanzo 12:16 Biblia inaandika, “Farao alimtendea Abramu vema kwa sababu ya
Sarai, naye akapata kondoo, ng’ombe, punda madume na majike, watumishi wa kiume
na wa kike, na ngamia.”
Katika Tarjuma ya Quran Tukufu kwa Kiswahili Surat Hajj
aya ya 27 inasomeka hivi, “Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu
ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.”
Huo ni
uthibitisho kuhusu Ngamia kwenye vitabu vya dini ya Kikristo na Uislamu. Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa na wikipedia zinasema, Ngamia wamefugwa na
binadamu tangu miaka 5,000–6,000 iliyopita.
Leo hii mifugo hao ni takriban
milioni 19 na idadi kubwa, yaani milioni 14, wako Afrika, milioni 7 pekee
nchini Somalia na milioni 3.3 nchini Sudan.
Katika miaka ya nyuma Wamasai wa
Kenya na pia Tanzania wameanza kufuga ngamia baada ya kuona ya kwamba ng'ombe
wao walikufa wakati wa ukame lakini ngamia waliendelea kuishi na kutoa maziwa.
Katika makala haya tutaangazia Jamii ya Ki-Maasai katika maeneo ya Hai na
Simanjiro nchini Tanzania ilivyovutiwa na ufugaji wa ngamia.
Mzee Dahir akiwa mbele ya ngamia wake anayefahamika kwa jina la Soran. |
DAHIR JAMA YUSUF NI NANI?
Huyu ni mtanzania mwenye asili ya
Kisomali aliyezaliwa mwaka 1932. Dahir Jama Yusuf alizaliwa katika kijiji cha
Bomang’ombe, Hai mkoani Kilimanjaro.
Baada ya miaka mingi ya kuishi katika ardhi ya Bomang’ombe alifanikiwa kuoa mke aliyemzalia watoto 11. Mkewe alifariki miaka mitatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 60. Katika watoto aliowazaa wa kiume wapo sita na wa kike watano.
Kifungua mimba ni mtoto wa kike aliyemzaa mwaka 1969. Aidha mziwanda ni watoto mapacha aliowazaa mwaka 1985, wote wa kiume. Kwa sasa Mzee Dahir anaishi katika kijiji cha Mtakuja kilichopo mpakani mwa Hai na Simanjiro katika kata ya KIA wilayani Hai.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 40 kutoka mji mdogo wa Bomang’ombe kwenye barabara ya Arusha-Moshi.
KILICHOMSABABISHA DAHIR KUFUGA
NGAMIA

Mzee Dahir Jama Yusuf akikamua
maziwa na Meneja wa ngamia hao Farul.
|
Mzee huyo wa miaka 87 alikuwa
mfugaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo kwa muda mrefu huku akiwa na kundi kubwa la
wanyama hao zaidi ya 100 hali iliyomfanya ahame katika ilivyo jadi ya wafugaji
kwa ajili ya kutafuta malisho.
Lakini baadaye anasema, “ Nilijifikiria moyoni namna ninavyopata tabu ya kuwalisha, nikabadili mawazo na kuanza kufuga ngamia.”
Pia mzee Dahir anaongeza kuwa ufugaji wa ngamia ni rafiki wa mazingira kutokana na kwamba wanyama hao hawali mimea ya kupandwa isipokuwa ya asili tu ikiwamo miti ya minyaa.
“Hawaleti mmomonyoko wa mazingira kama unavyoona katika zizi hakuna mmomonyoko wa udongo.” Dahir anasema hiyo inatokana na kwamba ngamia hawana kwato hivyo hawachimbi ardhi kama wanyama wengine wenye kwato.
ILIKUWAJE ALIPOINGIA KATIKA JAMII YA WAMAASAI?

Dahir alianza kufuga ngamia saba
aliowachukua nchini Kenya kwa kiasi cha Dola za Kimarekani 3,500 wakati huo,
ambayo kwa mmoja mmoja ilikuwa ni kiasi cha dola za Kimarekani 500. Pamoja na
gharama nyingine ilifika dola za kimarekani 5,000.
Aidha Mzee Dahir anasema wakati anawachukua kutoka Kenya aliwasafiri kwa mguu kwa takribani majuma mawili. Lakini sasa ana ngamia 80 na wote akiwa amewapa majina. Kinachostaajabisha kwa wanyama hao kila mmoja ikiitwa kwa jina lake inaelewa na kuitikia wito wa sauti ile.
Miongoni mwa majina ya ngamia wake ni Shar, Soran Sikhagh, Hira na Kuze. Miaka hiyo ya mwishoni mwa karne ya 20 wakati akiingia katika kijiji cha Mtakuja alikutana na mtu mmoja anaitwa Emmanuel Simeli wa jamii ya Ki-Maasai. Simeli ambaye sasa ana umri wa miaka 54 anasema,
“Wakati Mzee Dahir anaingia kijijini hapa, mimi nilikuwa mwenyekiti wa kitongoji; alinipa taarifa za kuhamia mahali hapa na tumeendelea kushirikiana hadi leo.”
USHUHUDA WA WAMAASAI KUHUSU NGAMIA

Dahir Jama Yusuf akisalimiana na
Emmanuel Simeli ambaye alikuwa mtu wa kwanza kumpokea Dahir kijiji hapo.
|
Simeli anasema, “Watu wa jamii
yangu walipokuwa wanaona wanyama hao walikuwa wanakimbia, lakini baadaye
tuliendelea kuelemishwa kuhusu ngamia na sasa wamewazoea na wengine wameanza
kufuga.”
Hata hivyo Simeli anasema miaka miwili ijayo ataanza kufuga mara baada ya kuona faida zake kwani hawana athari yoyote kwa mifugo mingine, na kwamba ni wanyama wapole. Farul ni kijana mwenye umri wa miaka 29 ambaye aliachana na kuchunga mifugo ya jamii ya Ki-Maasai na kuanza kuchunga ngamia wa mzee Dahir anasema,
“Nilianza kuchunga ngamia nikiwa na miaka 10 hadi sasa nimekuwa meneja wa mifugo ya mzee huyu kwa muda wote nimejifunza namna ya kufuga ngamia.” Kijana huyo alianza kufanya kazi na Dahir wakati huo akiwa na ngamia 20.
Farul ambaye alipewa ngamia mmoja na Mzee Dahir ambaye baadaye alimzalia ngamia wengine watano. Aidha kijana huyo mwenye watoto wawili nafurahi kufuga ngamia kuliko ng’ombe na mbuzi kutokana namna wanavyoweza kuvumilia mazingira na gharama ya kuwatunza ni ndogo huku faida zake zikiwa lukuki.
“Imesaidia sana familia yangu kujenga, kusomesha vilevile suala la kuhamahama kumeondoka kabisa, hata Wamasai wenzangu wameanza kuelewa na kufurahia wanyama hawa,” anaongeza Farul.
MAJIRANI WANAMCHUKULIAJE DAHIR?

Kijana Farul aliyeanza kufanya kazi
kwa Mzee Dahir Jama Yusuf tangu akiwa na miaka 10 akizungumza na mwandishi wa
makala haya.
|
Jamii ya Ki-Maasai inamwona Mzee
Dahir kama mtu ambaye ana mawazo chanya kuhusu maisha yao. “Dahir ni baba yetu
nje ya kutusaidia kujua wanyama hawa lakini amekuwa msaada wa masuala mengi ya
kijamii,” anasema Simeli.
Kwa upande wake Dickson Jackson ambaye ni Mwalimu katika Shule ya Msingi Kibaoni iliyopo upande wa Simanjiro anasema, “Mimi ni mwenyeji wa Musoma, Mara nilikuja mwaka 2014 katika kazi ya ualimu; ilikuwa mara ya kwanza kuwaona ngamia uso kwa uso aisee nilishtuka nilianza kukimbia baada ya kuwaona lakini baadaye niliwazoea.”
Aidha Dickson (32) anaongeza kuwa wamekuwa wakienda na wanafunzi ambao wengi ni wa jamii ya Ki-Maasai kujifunza namna ya kuwafuga wanyama hao.
Makala haya na:
Jabir Johnson;

Mwalimu Dickson Jackson wa Shule ya
Msingi Kibaoni, Simanjiro katika mahojiano na mwandishi wa makala haya.
|
Watoto wa Ngamia wa Mzee Dahir Jama Yusuf wakipelekwa malishoni |
Mwandishi wa makala haya Jabir
Johnson katika mojawapo ya zizi la ngamia wa Mzee Dahir Jama Yusuf.
|
Dahir Jama Yusuf akiwa majirani
zake walikwenda kumtembelea Machi 20, 2019.
|
Picha na: Kija Elias
nilikuwa naomba namba ya simu ya mzee huyu au mwandishi wa makala haya ili niweze kununua ngamia na kuanza kufuga
ReplyDelete