Pombe haramu ya Gongo katika hatua za awali |
Wednesday, August 31, 2016
16 kortini kwa kukutwa na gongo
NA MWANDISHI WETU
Wakisomewa mashtaka na Karani Blanka Shayo mbele ya Hakimu Mkazi
Matrona Luanda ilidaiwa Marijani Muhidin (29), Amos Yakob (30), Amina Ally
(47), Hidaya Abdul (33), Monica Milanzi (49), John Kibuko (26), Sophia Josephy
(40), Said Shabani (26), Hugo Saimoni (51), David Wilfredy (26), Shukuru
Mwagama (42), Said Kinyozi (47), Kennedy Umcha (35), Ndoma John (28), Adam Mohamed
(48) na Boniface Nestroy (31) walitenda kosa hilo Agosti 30 mwaka huu saa 11:30
jioni katika mtaa wa Pemba, Kariakoo jijini hapa.
Aidha ilidaiwa askari wa Jeshi la Polisi Na. 1669 Koplo Thomas
aliwakuta washtakiwa wakiwa na lita 15 za pombe hiyo kinyume na Kifungu cha
Sheria Na. 30 (16) cha Kanuni ya Adhabu.
Kesi itatajwa tena Septemba 12 mwaka huu huku fungu la dhamana Sh. 200,000
lilikuwa wazi kwa kila mshtakiwa.
Tuesday, August 30, 2016
Kondakta kortini kwa kutukana Mwalimu
NA JABIR JOHNSON
Mwalimu akifundisha darasani (Picha ya Mtandao) |
KONDAKTA wa daladala mkazi wa Vingunguti Kiwalani Nuhu Omary (32),
jijini Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Ilala kwa kosa la
kuwatukana walimu.
Akisomewa mashtaka na Karani Blanka Shayo mbele ya Hakimu Matrona Luanda ilidaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 19 mwaka huu saa 8:30 mchana katika maeneo ya Mnazimmoja kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 89(1)(a) sura ya 16 ya Kanuni ya Adhabu.
Aidha ilidaiwa mshtakiwa alimtukana Mwalimu Asia Abdallah na walimu wenzake waliokuwa katika gari hilo kuwa “Hawana Kazi Wanajiuza Mchana Kutwa”.
Hakimu alisema fungu la dhamana la Sh. 100,000 lipo wazi kwa mshtakiwa na
mdhamini wa kuaminika huku kesi ikitarajiriwa kusikilizwa tena Septemba 8 mwaka
huu.
Wizi wa madini wawafikisha kortini
ILALA, DAR ES SALAAM
Madini aina ya Natural Opal |
WAKAZI watatu wa Buguruni jijini Dar es Salaam akiwamo mganga wa
kienyeji wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kujipatia madini yenye
thamani ya Sh. Milioni 500 kwa udanganyifu.
Mwendesha Mashtaka Sylivia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce
Luhwago alidai Salum Joseph (52) ambaye ni mganga wa kienyeji, Zahoro Hamis
(41) na Sofia Michael kwa pamoja walitenda kosa hilo maeneo ya Buguruni Juni 24
mwaka huu kinyume na sheria za nchi.
Aidha Mitanto alidai washtakiwa walijipatia madini aina ya Opal (karati
92.14) yenye thamani ya Shi. Milioni 500 kwa udanganyifu wa kutumainiwa mali ya Jesse Kahembe aliyewatuma wakauze.
Upelelezi wa shitaka hilo haujakamilika hadi Septemba 12 mwaka huu
itakapotajwa tena, huku Hakimu akiwataka washtakiwa kutimiza masharti ya
dhamana ya Sh. Milioni 75 kila mmoja au hati ya makazi yenye thamani hiyo na
wadhamini wa kuaminika.
Matusi yampandisha kizimbani
NA MWANDISHI WETU
MKAZI wa Sikukuu
jijini Dar es Salaam Athuman Iddi (24) amepandishwa katika mahakama ya mwanzo Ilala
kwa kosa la kumtukana matusi ya nguoni Askari wa Jeshi la Polisi.
Akisomewa mashtaka
na karani Blanka Shayo mbele ya Hakimu Mkazi Matrona Luanda ilidaiwa mshtakiwa
alitenda kosa hilo Agosti 29 mwaka huu saa 5:49 usiku kinyume na Kifungu cha
Sheria Na. 89(16) cha kanuni ya adhabu.
Aidha ilidaiwa
mahakamni hapo mshtakiwa alitenda kosa hilo katika mtaa wa Kongo kwa askari
aliyekuwa lindo katika Tawi la NMB aliyefahamika kwa jina la Sajenti Kambona D.4061
alipomtukana, “Wasenge na hamnifanyi lolote”.
Hakimu alisema
fungu la dhamana lipo wazi kwa mshtakiwa kwa Sh. 400,000 na kwamba kesi hiyo
itatajwa tena Septemba 8 mwaka huu.
Katika shauri
lingine mkazi wa Zakheim Mbagala Ramadhani Omary (35), alipandishwa kortini kwa
kumtukana Zawadi Abdallah matusi ya nguoni.
Ilidaiwa
mahakamani hapo mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 26 mwaka huu saa 11 jioni
maeneo Jangwani, “Kuma la mamaake, msenge unafirwa” kinyume na sheria za nchi.
Hakimu alisema
fungu la dhamana la Sh. 100,000 lipo wazi na mdhamini mmoja wa kuaminika na
kesi itatajwa tena Septemba 8 mwaka huu.
Monday, August 29, 2016
Fundi seremala kizimbani kwa wizi
NA DIANA JOACHIM, TUDARCO
FUNDI seremala aliyefahamika kwa jina la Mrisho Iddi (29) mkazi wa
Mchikichini amefikishwa mahakama ya mwanzo ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa
kosa la kuiba pochi iliyokuwa na dola 3000.
Akisomewa mashtaka na karani Blanka Shayo mbele ya Hakimu Matrona
Luanda ilidaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na sheria za nchi, Agosti
26 mwaka huu katika Mtaa wa Kongo, Kariakoo.
Aidha ilidaiwa kuwa mshtakiwa aliiba pochi iliyokuwa na risiti za bidhaa,
vitambulisho na dola 3000 (sawa na Sh. Milioni 6 mali ya Alli Bonomali .
Hakimu alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kwa ahadi ya Sh. Milioni
10 na wadhamini watatu wa kuaminika na aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 6
mwaka huu.
Katika shauri lingine Omary Twaha (23) na Jeremia Molel (32) wote
wakazi wa jijini hapa waliiba Sh. Milioni 2 zilizokuwa dukani mali ya Boniface
Gervas.
Washtakiwa walikana mashtaka hayo na kesi kuahirisha hadi Septemba 7
mwaka huku washtakiwa wakitakiwa kutoa Sh. Milioni 3 na wadhamini wawili.
Kortini kwa kukutwa na Heroine
ILALA, DAR ES SALAAM
MKAZI wa Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam Mbaraka Ndambwe
(22) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Ilala kwa kukutwa na
dawa za kulevya aina ya heroine.
Mwendesha mashtaka Chesensi Gavyole mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule
alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 2 mwaka huu Buguruni kwa Mnyamani
kinyume na sheria za nchi.
Pia ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio alikuwa katika nyumba ya Salma Ramadhani wakati alipokamatwa
akiwa na gramu 1.92 ya dawa hizo.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa unajiandaa kuleta mashahidi watano na
vielelezo viwili kuhusu kesi inayomkabili mshtakiwa.
Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 7 mwaka huu itakapotajwa
tena.
Friday, August 26, 2016
Kortini kwa wizi kontena la Mil. 160
NA JABIR JOHNSON
WATU
watatu wamepandishwa kortini katika mahakama ya wilaya ya Ilala jijini hapa
wakikabiliwa na makosa ya kula njama na kujipatia mali kwa udanganyifu ikiwamo
wizi wa kontena lenye thamani ya Sh. Milioni 160
Wakisomewa
mashtaka na Mwendesha Mashtaka Sylivia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce
Luhwago mshtakiwa Abdallah Ndule mkazi wa Mbezi Louis (47) na Hassan Selemani
mkazi wa Buguruni (49) ilidaiwa washtakiwa wakiwa na Hamis Mtitu (ambaye
hakutokea mahakamani hapo) walitenda kosa hilo Mei 16, 2015 maeneo Ticts
Bandarini.
Aidha
Mitanto alidai walitenda kosa la kula njama kinyume na Kifungu cha Sheria Na.
384 cha Kanuni ya Adhabu kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na walitenda
kosa la wizi wa kontena Na. MSK 435766 lenye thamani ya Sh. 160,125,433 kinyume
na Kifungu cha Sheria Na. 258 na 265(16) mali ya Nyota Tanzania Ltd.
Baada
ya kusomewa mashtaka yao Hakimu wa mahakama hiyo aliwapa masharti ili waweze
kuachiliwa kwa dhamana kuweka Sh. Milioni 20
au Hati za Makazi zenye thamani ya Sh. Milioni 20, washtakiwa
walishindwa na kurudishwa rumande hadi Agosti 30 mwaka huu itakapotajwa tena.
Kizimbani kwa kuvuruga ibada
ILALA, DAR ES SALAAM
WATU 10 wamepandishwa kizimbani kwa kuvuruga ibada ya waumini wa Kanisa
la Moravian Parishi ya Kitunda jijini hapa.
Wakisomewa mashtaka na Mwendesha Mashtaka Sylivia Mitanto mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago ilidaiwa
washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 14 mwaka huu.
Ilidaiwa Joachim Mwaseba (45), Obadia Mwatonoka (28), Obedi Mbotwa
(28), Matthew Mwasiposya (62), Kennedy Nsangafuru (21), Geoffrey Kibona (25),
Godfrey Gambi (35), Edom Kasengile (39), Boniface Disoni (35) na Martin Mwiba
(35) walitenda kosa hilo kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 126 na 35 CAP 16 R.E
2002 cha Kanuni ya Adhabu.
Washtakiwa wote walikana kuhusika na tukio hilo hivyo kuachiliwa kwa
dhamana
Awali upande wa utetezi chini ya Wakili Msomi Hezron Mwankenja uliiomba
mahakama kuipeleka kesi hiyo hadi Novemba 24 mwaka huu kutokana na wakili huyo
kupata udhuru ambapo Hakimu Luhwago aliridhia ombi hilo.
Thursday, August 25, 2016
Wizi wa Sh. Milioni 13 wamtupa jela miaka 4
NA DIANA JOACHIM, TUDARCO
MKAZI wa Lumo, Ilala jijini hapa Ally Juma (25) ametupwa jela miaka minne baada ya kukutwa na kosa la wizi wa Sh. 13,500,000 mali ya Come and Call Co. Ltd
MKAZI wa Lumo, Ilala jijini hapa Ally Juma (25) ametupwa jela miaka minne baada ya kukutwa na kosa la wizi wa Sh. 13,500,000 mali ya Come and Call Co. Ltd
Akisomewa mashtaka na Mwendesha Mashtaka Florida Wenceslaus mbele ya Hakimu
Mkazi Juma Hassan ilidaiwa Machi 3, 2014 mshtakiwa akiwa na Charles Malima
walivamia kampuni hilo na kuiba kiasi hicho cha fedha.
Aidha mwendesha mashtaka alidai mshtakiwa aliwatishia kwa bastola Ivan
Marinde na Agnes Pima ili kujipatia mali hiyo kinyume na Kifungu cha Sheria Na.
258 na 265 cha Kanuni ya Adhabu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walijipatia mali
hiyo kwa uvamizi wa kutumia silaha kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 287A cha
Kanuni ya Adhabu.
Hakimu alisema ushahidi wa kuvamia kwa kutumia silaha
haukuthibitika hivyo mshtakiwa wa pili Charles
Marinde kuachiwa huru.
Pia mshtakiwa wa kwanza Ally hakuwepo mahakamani hapo kutokana na
kuendelea kutumikia kifungo cha miezi sita kwa kutaka kumpaka kinyesi Hakimu wa
kesi hiyo.
Wednesday, August 24, 2016
Wembe wampeleka kortini, sahani zamtupa jela miezi minane
NA JEMA MAKAMBA
KIJANA
aliyefahamika kwa jina la Chande Rashid (20) amepandishwa kortini katika
Mahakama ya Mwanzo Ilala jijini Dar es Salaam kwa kosa la wizi na kudhuru
mwili.
Akisomewa mashtaka
na karani Lucy Lutabazi mbele ya Hakimu Asha Mpunga ilidaiwa mshtakiwa alitenda
kosa Agosti 8 mwaka huu saa 4 usiku kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 241(16)
cha kanuni ya adhabu maeneo ya Uhonda na Raha.
Ilidaiwa mshtakiwa
ambaye kazi yake ni kubeba mizigo walipishana kauli na Mohamed Mfaume ndipo
alipochukua wembe na kumchana pua.
Hakimu ameahirisha
kesi hadi Septemba 7 mwaka huu itakapotajwa tena.
Katika shauri
lingine Sharif Fadhil (19) mkazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam ametupwa jela
miezi minane kwa wizi sahani na kuharibu mali za Noel Aloyce.
Ilidaiwa Juni 16
mwaka huu katika mtaa wa Aggrey mshtakiwa alitenda kosa kinyume na Kifungu cha
Sheria Na. 265(16) na 336(16) akitumia kisu.
Hakimu alimtaka
mshtakiwa atupwe jela na akishatoka atapaswa kulipa thamani ya mali ya mshtaki.
Kortini kwa ubakaji mtoto miaka 5
ILALA, DAR ES SALAAM
MKAZI
wa Kitunda jijini Dar es Salaam Damian Leonard (18) amepandishwa kizimbani
katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la ubakaji.
Akisomewa
makosa na Mwendesha Mashtaka Sylivia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce
Luhwago ilidaiwa Mei 27 mwaka huu Kitunda Machimbo wilaya hapa mshtakiwa
alimbaka mtoto wa miaka mitano.
Aidha
ilidaiwa mahakamani hapo mshtakiwa alishtakiwa na Kifungu cha Sheria Na. 130
(1)(2)(e) na 131(1) cha kanuni ya adhabu CAP 16 R.E 2002.
Mshtakiwa
alikosa wadhamini Hakimu aliahirisha kesi hadi Septemba 6 mwaka huu
itakapotajwa teja.
Katika
shauri lingine Mgeni Mohamed mwenye miaka 18 mkazi Bombom alipandishwa kortini
katika mahakama hiyo kwa kukutwa na kete
60 za dawa za kulevya aina ya bangi zenye gramu 27.73
Mwendesha
Mashtaka Chesensi Gavyole alidai mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule mshtakiwa
alitenda kosa hilo kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 15(1)(a) na 15(2), Juni 24
mwaka huu maeneo ya Kiwalani CCM.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi Septemba 6 mwaka huu itakapotajwa tena.
Monday, August 22, 2016
Kortini kwa kuchomoa Sh.200,000/-
NA MAGRETH MTAFI
MKAZI wa Magomeni Thadei Agostino(35) amefikishwa mahakama ya mwanzo
Ilala kwa kukabiliwa na mashtaka ya kumchomolea Seif Mohamed kiasi cha shilingi
200,000.
Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkazi ya mahakama hiyo, Asha Mpunga ,Karani wa kesi hiyo Lucy
Lutabazi alidai mshtakiwa alifanya kosa hilo Agosti 20 saa tatu usiku maeneo ,
Kariakoo Dar es Salaam.
Ilidaiwa mshtakiwa alifanya kosa hilo kwa makusudi huku akijua kuwa ni
kosa kisheria, baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana kosa hilo.
Hakimu mpunga alisema dhamana iko wazi kwa kufuata masharti, ambapo
wadhamini watasaini shilingi 300,000, mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya
dhamana na alirudishwa rumande hadi Septemba Mosi mwaka huu kesi hiyo
itakapotajwa tena.
Katika hatua nyingine washtakiwa Bernad stanley(18) na Chacha
Chacha(34) walifikishwa katika mahakama hiyo kwa kosa la wizi wa fedha Sh. 60,000
mali ya Wiliam Mlenda.
Ilidaiwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo Agosti 21 maeneo ya
kariakoo Dar es Salaam.
Washtakiwa walikana kosa kosa hilo mshtakiwa namba moja Bernard Stanley
alirudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana na Chacha ametoka
kwa dhamana ambapo watarudi mahakamani hapo Semptemba mosi kesi hiyo
itakapotajwa tena.
Jela miaka 3 kwa Wizi
ILALA, DAR ES SALAAM
MKAZI wa Unguja Migombani Said Rashid Said (26) amehukumiwa kwenda jela
miaka mitatu na mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam baada ya kukutwa na
hatia ya wizi wa gari mali ya Mohamed
Ibrahim Ismail.
Mwendesha mashtaka mahakamani hapo Florida Wenceslaus alidai mshtakiwa
alitenda kosa hilo kati ya Aprili 7 na 19 mwaka 2012 alikula njama na
udanganyifu ili kujipatia gari aina ya Suzuki Escudo lenye usajili wa T 708 BZS
lililokuwa likisafiriwa kutoka Zanzibar kwenda Kilimanjaro kupitia Dar es
Salaam.
Wenceslaus alidai gari hilo awali lilikuwa Zanzibar chini ya mmiliki wa
kwanza Maliki Said Ramadhani likiwa na usajili wa Z 326 DQ na kuuzwa kwa
Mohamed kwa Sh. Milioni 14.
Wakili wa mshitakiwa Ludovick Nickson aliiomba mahakama kumpunguzia
kifungo mshtakiwa kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kifamilia kwani ana
mke, watoto na wazazi wanaomtegemea na kusisitiza ingefaa apewe kifungo cha
nje.
Awali Mwendesha Mashtaka aliiomba mahakama impe adhabu kali mshtakiwa
kwani alidhamiria kufanya kosa hilo na
kwamba amemtia hasara mlalamikaji kutokana
na kesi hiyo kuchukua muda mrefu.
Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja alisema
mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuhusu ushahidi wa watu watano uliotolewa
kuhusu mshtakiwa kwamba alikwenda
kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 258, 265 cha Kanuni ya Adhabu CAP 16 R.E 2002.
Kiyoja aliongeza mshtakiwa anapaswa kutumikia jela miaka mitatu na gari
T 708 BZS litatakiwa kukabidhiwa kwa mlalamikaji.
Saturday, August 20, 2016
Abaka mwanafunzi darasa la pili Bagamoyo
BAGAMOYO, PWANI
Binti aliyebakwa na mtuhumiwa Umbuje |
Uchunguzi umebaini mtuhumiwa alilitenda kosa hilo Julai 16 mwaka huu saa
nane mchana nyumbani kwake mtaa wa Mingoi kata ya Mapinga wilayani hapa baada
ya mtoto huyo kutumwa kuchukua ‘Ice Cream’ ndani.
Aidha baada ya mtuhumiwa kutenda kitendo hicho alimtishia mtoto huyo
kwamba angemnyonga kama angetoa siri za kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama.
Akizungumza mtoto huyo alisema, “Mimi hapa nilitoka
shule baada ya kula chakula dada alinituma nichukue Ice Cream ndani ndipo
alipokuja…alinichukua juu, akaniziba mdomo na kuniweka kwenye kochi akanibaka.”
Mtoto huyo aliongeza kuwa mtuhumiwa ambaye mtaani anajulikana kama Baba
Mukhsin,
“Hakuvua suruali, wala shati katoa tuu m****** wake, kisha nikavaa sketi yangu nikaondoka lakini damu kidogo ilinitoka,…nilikaa kama wiki hivi…aliyenigundua ni mwalimu wa afya na kutunza mazingira.”
Pia mtoto huyo alisisitiza licha ya mwalimu huyo kumgundua na kumtaka
aseme kuhusu hali hiyo lakini hakusema akihofia vitisho vya mwanajeshi huyo na
kwamba aliweka bayana baada ya askari polisi wa kike kumhoji.
Mwalimu aliyegundua hali ya binti huyo Kandida Asenga alisema, “Tulimuona mtoto huyo
akishindwa kabisa kukaa tukamuuliza akasema nina mchubuko, tukahisi ana tatizo
jingine, ndipo tulipoamua kumchukua na kumpeleka katika Zahanati ya Mtambani
ambako nesi akatupa majibu kwamba amebakwa…tukaenda polisi.”
Daktari wa Zahanati ya Mtambani wilayani hapa Baraka Mushi
alithibitisha kumpokea mtoto huyo Julai 21 mwaka huu na kubaini kwamba
alitendewa unyama huo.
Mama wa binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Zainabu Mtungwe (31)
alisema, “Dada yake alinipigia simu, huyu mtoto nilimwacha na dada yake
nilimkabidhi kwake kwani alikuwa anafanya kazi kwa mama Mukhsin kwa mazingira
ya shule…kutokana na hali yangu haikuwa vizuri nikarudi Kusini (Mtwara), na
nilitaka kumhamisha anifuate lakini wakanishauri nimwache hadi oktoba… nimekuja
jana (Agosti 10 mwaka huu)….hayo uliyoyasikia ni hayohayo …na upelelezi wa Polisi unaendelea.”
Mjomba wa binti huyo Hamis Abdallah Omari ‘Subiri’ mwenye miaka 55
aliyesafiri kutoka Mtwara hadi wilayani hapa alisema, “Natokea Chungutwa, Masasi
mkoani Mtwara, kilichonileta ni taarifa ambayo dada yangu…kwamba binti yetu
amebakwa na mwanajeshi Baba Mukhsin. Nilipofika nilienda kituo cha Polisi
Mapinga lakini wakawa wananizungusha ikabidi niende kwa Mwalimu shuleni
anakosoma nikapata kila kitu.”
Kwa upande wake Umbuje alisema, “Kwa sasa nafanya kazi kwenye Ofisi ya
Makamu wa Rais…Jambo hilo sio la kweli hata Jeshi la Polisi liliniita jana
(juzi),nami niliripoti… yaani halina ukweli wowote…hivi kweli mtu mzima na
akili zake anaweza kufanya hivyo?”
Umbuje aliongeza, “Polisi wanaendelea na uchunguzi wao,…kwa kweli
wananichafua…halina ukweli wowote…ndio mimi, ndio Baba Mukhsin.”
Aidha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventure Mushongi alisema, “Sina taarifa
hizo kwa sasa nipo huku Mkata nikirudi nitazifuatilia taarifa hizo kutoka kwa
wenzangu…”
Friday, August 19, 2016
Ang’atwa na bosi akidai Sh. 250,000/-
Ilala, Dar es Salaam
MFANYABIASHARA aliyefahamika kwa jina la Kalunde Waijuba mwenye miaka
42 mkazi wa Kisota, Kigamboni jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala akituhumiwa kufanya shambulio la kudhuru mwili.
Akisoma mashtaka Karani Lucy Lutabazi alisema mtuhumiwa alitenda kosa
hilo Agosti 10 mwaka huu saa 9:40 alasiri katika mtaa wa Mkunguni jijini hapa.
Ilidaiwa na mbele ya Hakimu Mkazi Asha Mpunga kuwa mtuhumiwa alitenda
kosa hilo wakati mlalamikaji Bi. Upendo alipokwenda kudai Sh. 250,000/-.
“Mtuhumiwa alimvamia mlalamikaji na kumpiga ngumi kumi za kifua,
alimpiga mgongoni, mdomo mateke ya tumboni kisha kumkanyaga, pia alimng’ata
meno bega na kumsukumiza chini huku akijua
kufanya hivyo ni kukiuka kifungu cha
sheria Na. 241(16) cha kanuni ya adhabu,” alidai Mwendesha Mashtaka.
Aidha Hakimu Mkazi alimtaka mlalamikaji kupata dhamana ya Sh. 800,000/-
kutoka kwa wadhamini wawili kisha aliahirisha kesi hadi Agosti 31 mwaka huu
itakapotajwa tena.
Katika shauri lingine kijana aliyefahamika kwa jina la Said Omary mwenye miaka
19 mkazi wa Kibondeni mjini Zanzibar amepandishwa mahakamani kwa wizi wa waya
wenye thamani ya Sh. 10,000.
Akisoma Mwendesha Mashtaka alisema Agosti 13 mwaka huu saa 3:20 usiku maeneo Upanga jijini hapa kwenye Ofisi za Stamico aliiba
waya huo kinyume na kifungu cha sheria Na. 265 (16) cha kanuni ya adhabu.
Mtuhumiwa amekubali kosa amerudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini
mpaka Agosti 31 mwaka huu itakapotajwa tena.