Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Wednesday, December 28, 2016

Dk. Guydon Makulila na salamu za Mwaka Mpya 2017

ZIMEBAKI siku chache kumaliza majuma 52 ya mwaka 2016. Katika mwaka huu kuna mengi yametokea ya kuudhi, kuhuzunisha na kufurahisha. Licha ya changamoto zote bado kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitambua kuwa hayo yote ni maisha.
Dk. Guydon Makulila

Kwani maisha ni mchanganyiko wa vipindi vyote vya kila siku katika maisha ya binadamu. Inapokuwa siku zote ni furaha tu hayo sio maisha, ikiwa ni kulia tu bila kingine hayo sio maisha.
Jaizmelaleo imepata bahati ya kuzungumza na Dk. Guydon Makulila ambaye ni mtaalamu wa mtaalam wa kutoa dawa za usingizi katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya kuhusu masuala mbalimbali.
Dk. Makulila (kushoto) akiwa na wahandisi kutoka Kasmedics Ltd baada ya kufunga mashine ijulikanayo kwa jina la Universal Anaestjeaia (UAM), katika kuhakikisha wagonjwa wa upasuaji wanapata huduma bora na ya usalama.
Miongoni mwa mambo aliyoyasema ni kuhusu matarajio yake mwaka 2017 katika medani yake ya utabibu.
“Matarajio yangu kwa mwaka 2017 ni kuongeza ufanisi katika kazi yangu ili wagonjwa wote ninaowahudumia wapate kurudi katika hali yao ya kawaida,” alisema Dk. Makulila
Aidha Dk. Makulila alifunga kwa kuiasa jamii ya Watanzania ambao baadhi yao wamekuwa na tabia ya kujinunulia dawa pasipo kupimwa.
“Pia naiasa jamii kuwa na hali ya kuwahi katika vituo vya tiba ili kupata matibabu ya uhakika na sio kujitibia wenyewe kama ilivyo kwa sasa wananchi wengi wanaojinunulia dawa katika maduka ya madawa pasipo kupimwa,” alihitimisha Dk. Makulila.
Kwa ufupi Dk. Makulila ni baba wa watoto watatu (Kefa, Samweli na Guydon) na mke mmoja mwenye uzoefu wa kimataifa katika fani ya udaktari ambapo amekuwa akichukua kozi na mazoezi mbalimbali ya kuongeza ufanisi wake ndani na nje ya nchi.
Familia ya Dk. Makulila



Thursday, December 22, 2016

Happy Birthday Brayan Kuzenza

NA MWANDISHI WETU
Brayan Kuzenza
 Brian Kuzenza amesheherekea miaka mitatu (3) ya kuzaliwa kwake.
Hafla hiyo ilifanyika katika nyumba ya bibi yake Magdalene Mdai katika kitongoji cha Mpakani, Kibondeni-Mbagala jijini Dar es Salaam. Ndugu, jamaa, marafiki walihudhuria hafla ya mtoto huyo. Mama wa mtoto Vaileth Mdai alisema tukio hilo ni muhimu kwa maisha ya mwanaye.
Hata hivyo washiriki wa hafla hiyo walimtakia maisha marefu yenye baraka tele na uongozi wa Mwenyezi Mungu katika siku za usoni. Brian alizaliwa Desemba 22, 2013 Ismani Health Centre, Iringa.
Brian akikata keki huku akishuhudiwa na ndugu, jamaa na marafiki

Brian Kuzenza (kushoto) akimlisha keki bibi yake, Magdalena Mdai katika hafla iliyofanyika Mpakani, KibondeMaji-Mbagala jijini Dar es Salaam










Brian (kushoto), akiwa na mama yake na Yassir baada ya keki kuleta kwenye hafla hiyo.



Mariamu Ramadhani Mbiaji akiwasilisha keki ya Brian akiwa na mdogo wake Beatrice muda mfupi baada ya kuanza hafla hiyo.



Marafiki wa Brian hawakuwa nyuma katika kumpongeza Brian



Mariamu Ramadhani Mbiaji akiwa na Brian muda mfupi kabla ya kuanza hafla hiyo.

Brian  akiwa na mama yake muda mfupi baada ya keki kuletwa  kwenye hafla hiyo.


Tuesday, December 20, 2016

‘Rushwa ya ngono sasa basi’

NA JEMAH MAKAMBA
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Chalinze Anthony Nyange (aliyesimama) akizungumza katika semina hiyo

JAMII imetakiwa kuungana na taasisi zisizo za kiserikali katika vita dhidi ya rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi ili kuiweka nchi katika nafasi nzuri kimaendeleo.
Akizungumza katika semina ya uwezeshaji iliyofanyika Miono wilayani Chalinze, Pwani hivi karibuni Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo Anthony Nyange alisema rushwa ya ngono imesababisha madhara makubwa katika jamii.
“Rushwa ya Ngono imekuwa sugu nchini kutokana ugumu uliopo katika kumgundua mhusika, bila nguvu ya jamii pamoja na NGO’s hizi vita hii itakuwa ngumu kuikabili na itawatafuna watoto wetu hususani wa kike,” alisema Nyange.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa na na Shirika la Maendeleo ya Wajasiriamali Miono (SHIMAWAMI) kwa msaada wa Women Fund Tanzania (WFT), Nyange aliweka bayana kuwa taasisi zinazoendesha harakati mbalimbali za kimaendeleo ni muhimu kwani zinaikumbusha serikali ulazima wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Nyange alisisitiza kuwa umaridadi umekuwa ukitumiwa na wengi kutenda maovu kutokana na uvivu miongoni mwa wanawake, tamaa, ukosefu wa sifa kwenye ajira na uwezo wa kifedha.

Hata hivyo Nyange aliwakumbusha washiriki akali wa 65 wa SHIMAWAMI kuwa utafiti  umeonyesha wanawake na wasichana wengi wamekuwa wakikosa sifa katika maeneo ya kazi lakini wameendelea na kazi kutokana na mahusiano ya kimapenzi na mabosi wao.








Sunday, November 20, 2016

Guninita atoa rai Chadema

NA MWANDISHI WETU
John Guninita
 MAKATIBU wa Wilaya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wametakiwa kujenga utaratibu wa kuwaita makatibu wakuu wa kata katika wilaya zao na kuwapa taarifa za mapato na matumizi ili kurahisisha utendaji wa chama bila manung’uniko.
Katika mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa wilaya hiyo Bernard Mwakyembe walihudhuria Mbunge wa Viti Maalum jimbo la Temeke Lucy Magereri, Afisa Kanda ya Pwani kwa tiketi ya chama hicho Christopher Mbusule Shiru
Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo Chang’ombe jijini Dar es Salaam kiongozi huyo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema mapato na matumizi katika chama ni sehemu nyeti ambayo isipowekewa utaratibu mzuri huibua migogoro isiyo na sababu.
Aidha Guninita alisisitiza serikali ya Rais John Magufuli (JPM), imejaa woga, kiburi na majivuno yasiyo na msingi wowote katika maendeleo ya nchi hii.
“Mimi ni mwanasiasa wa siku nyingi…viburi, majibu ya hovyo hovyo, hiyo ndiyo CCM ya sasa. Rais ni kama mpiga ngoma anapiga mwenyewe na kutaka kucheza mwenyewe… Haiwezekani,” alisema Guninita.
Pia aliongeza tatizo kubwa la watanzania namba moja ni maji na kwamba Rais anaogopa kukosolewa juu ya hilo.
“Rais mzuri ni yule anayewaruhusu wananchi wake wamkosoe, sio yule anayefanya tathmini kwa mwaka mmoja…hatujaona mabadiliko kwa Magufuli,” alisema Guninita.
Kwa upande wake Magereri alisema Operesheni Amsha Chama inakuja na itaendeshwa nchi nzima kuelekea 2020 na kuongeza kadi mpya za kielektroniki kwa wanachama zitaanza kupatikana mwaka ujao.
Aidha Afisa wa Kanda ya Pwani aliwataka wanachama wasitishike na vitisho vya serikali iliyopo sasa isipokuwa sauti ya pamoja itatwatoa katika konga hilo.
Pia aliwataka wanasheria wa chama kupita katika kata na kuwaeleza na kutolea ufafanuzi wa katiba ya chama chao ili kuongeza na kukuza uelewa wa mwongozo huo hali itakayoondoa sintofahamu.
Kata 13 za wilaya ya Temeke zilihudhuria mkutano huo hivyo kutimiza akidi kwa mujibu wa Sura ya sita (6.2), ya katiba ya chama hicho 
Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bernard Mwakyembe (katikati) akipiga makofi pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya hiyo uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mwenezi wa Wilaya hiyo Edson Joel, kulia ni mgeni rasmi John Guninita. (Picha na Mpigapicha wetu





Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lucy Magereri akizungumza jambo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam.




Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lucy Magereri akizungumza jambo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Tuesday, October 25, 2016

Kizimbani kwa wizi wa magodoro Aga Khan

NA JABIR JOHNSON
WATU wawili wamepandishwa kortini katika mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka kwa kosa la wizi wa vitu mbalimbali vya Hospitali ya Aga Khan yakiwamo magodoro 20.
Wakisomewa mashtaka yao jana na Mwendesha Mashtaka Grace Mwanga mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo ilidaiwa washtakiwa Jimmy Rupia (47) na James Makoye (37) walitenda makosa mawili eneo la Aga Khan Julai 20 mwaka huu.
Mwendesha mashtaka alidai kosa la kwanza lilikuwa ni kuvunja ghala la vifaa vya hospitali wakiwa na nia ya kuiba kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 296 (a) na kosa la pili ni kuiba magodoro 20, mahema matatu na mashine ya kubembea kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 258 na 265.
Aliongeza kuwa mali zote zilizoibwa zilikuwa na jumla ya thamani ya Sh. 10,900,000 mali ya hospitali hiyo.
Washtakiwa wote wawili walikana mashtaka yao na kutakiwa kutimiza masharti ya dhamana kwa kutoa ahadi ya Sh. 3,000,000 na wadhamini wawili wanaotambulika; hata hivyo walikosa wadhamini na kurudishwa rumande.

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 7 mwaka huu.

Kizimbani kwa kubaka

ILALA, DAR ES SALAAM
MKAZI wa Majohe Plaza jijini Dar es Salaam Ally Ramadhani (23) amepandishwa kizimbani kwa kosa la kumbaka msichana wa miaka 17.
Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Flora Mjaya, mwendesha mashtaka Ashura Mnzava alidai Mei 5 mwaka huu eneo la Kinyerezi mshtakiwa alitenda kosa hilo huku akijua ni kinyume cha sheria.
Mnzava aliongeza mshtakiwa alikiuka Kifungu cha Sheria Na. 130(1)(2)(e) na 131(1) sura ya 16 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo.
Hakimu alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi endapo atakuwa na wadhamini wawili wa kuaminika na ahadi ya Sh. 3,000,000; hata hivyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Kesi itatajwa tena Novemba 7 mwaka huu.

Monday, October 24, 2016

Dk. Mashinji Oktoba 23


Alichokisema Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Vincent Mashinji baada ya uchaguzi wa meya wa Kinondoni, Oktoba 23, 2016 kuhusu kufungua kesi mahakamani.

“Chadema hakitakuwa chama cha kulalamika…hatutakuwa walalamishi tena tutakusanya ushahidi…Hii sio Tanzania tulioitarajia. Ilikuwa ni wanasiasa sasa ni zamu ya wanahabari.”

“CHADEMA ilianzisha Operesheni Umoja wa Kupambana Udikteta Tanzania (UKUTA), hatuwezi kukaa kimya tena, Nyerere alikataza Vijana kuwa wanyonge na waoga, hakutaka Taifa la watu waoga, na sisi tunasema mwisho wa uoga umekwisha, tutakwenda Mahakamani kwa sababu kilichotokea kwenye Uchaguzi wa Meya wa Manispaa Kinondoni ni uhuni, kanuni na taratibu zinavunjwa waziwazi.”

 “Wanafahamu kwamba vyombo vya habari vya Kimataifa hawawezi kuvibana. Sisi tunakwenda mahakamani pili ili kuondoa ukakasi huu. Watumishi wa umma hamna amani tena tutapigania Katiba ya Wananchi.”

Hata hivyo Mashinji alieleza tija ya kufungua kesi mahakamani kutokana na kwamba hadi sasa wamefungua kesi nyingi.

“Kesi nyingi tumefanikiwa…unapofungua kesi mahakamani inaonyesha kuwa unaheshimu utawala wa sheria, pili unaweka msingi wa siku zijazo watu watakuja kujua wenzetu kumbe walifanya hivi; tatu unapokuwa unatafuta tafsiri ya mahakama unakuwa huru zaidi katika maamuzi yako binafsi na mwisho ni kwa tija ya wananchi.”

Sunday, October 23, 2016

Sita kortini kwa unyang’anyi

NA MWANDISHI WETU
WATU sita wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Mbele ya Hakimu Mkazi John Msafiri, Mwendesha Mashtaka Sylivia Mitanto alidai Ramadhani Athumani (18), Jabil Muhando (17), Khalifan Humba (16), Nurdin Muhando (17), Abdul Omary (15) na Hamad Mohamed (15) walitenda makosa mawili ya unyanganyi wa kutumia silaha Septemba 13 mwaka huu eneo la Vingunguti kwa Simba.
Mitanto aliongeza washtakiwa hao walii simu ta kiganjani aina ya Tecno M3 yenye thamani ya Sh. 130,000; Nguo za Mazoezi zenye thamani ya Sh. 60,000; mkanda mweusi wenye thamani ya Sh. 150,000 na fedha taslimu  Sh. 30,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh. 370,000 mali ya Laika Mboya.
Katika kosa la pili washtakiwa walimwibia Tabu Juma simu aina ya Samsung yenye thamani ya Sh. 350,000 na katika makosa yote kabla na baada ya kuiba waliwatishia kwa panga ili kujipatia mali hizo.
Washtakiwa walikana mashtaka yao huku wakishindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Kesi itatajwa tena Novemba 2 mwaka huu.

Friday, October 21, 2016

Dereva wa daladala jela miaka 7

ILALA, DAR ES SALAAM
MAHAKAMA ya Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu dereva wa daladala mkazi wa Ubungo wa External Mohamed Amir Ramadhani kwa wizi wa Sh. 6,700,000.
Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja alisema ushahidi wa mahakama umethibitisha bila shaka yoyote kuwa mnamo Mei 5, 2015 eneo la Gongo la Mboto aliiba begi lililokuwa na fedha taslimu milioni sita na laki saba.
Kiyoja aliongeza kuwa Mohamed alifanya wizi huo kwa kuvunja kioo cha gari Na. T768 CJX aina ya Toyota Harrier mali ya Ally Ngaboli kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 258 na 265 cha Kanuni ya Adhabu
Kiyoja alisema shahidi wa kwanza akiwa Gongo la Mboto eneo la Majumbasita alipaki gari lake ili kununua matunda aliporudi alikuta wamevunja kioo.
Hakimu alisema mashahidi wengine waliiambia mahakama kuwa walishuhudia wizi huo na kumsaidia shahidi namba moja kumkamata mwizi kisha kumfikisha kituo cha polisi kwa hatua zaidi.
Awali mwendesha mashtaka Florida Wenceslaus aliiomba mahakama kuwa mshtakiwa apewe adhabu kali ili iwe fundisho kutokana na kutokuwa na historia ya makosa ya jinai.
Akijitetea Mohamed aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa ni mgonjwa wa kifafa, familia yake inamtegemea wakiwamo watoto anaowasomesha na kuwalipia ada pia baba yake ni mzee na mama yake ni mgonjwa wa shinikizo la damu na kisukari.
Hata hivyo kujitetea kwake hakumzuia Hakimu kumtupa jela miaka saba.

Thursday, October 20, 2016

‘Scorpion’ afunguliwa upya mashtaka, abadilishiwa hakimu

NA JABIR JOHNSON
Salum Njewete 'Scorpion' akitolewa nje ya ukumbi wa mahakama ya Wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam jana chini ya ulinzi mkali baada ya kusomewa mashtaka upya.


MSHTAKIWA wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha Salum Njwete (34) ‘Scorpion’  amefutiwa shtaka lake la awali na Mahakama ya Wilaya Ilala, jijini Dar es Salaam jana kisha kesi yake kuanza upya.
Hata hivyo kuanza kwa shtaka lake jipya kumeenda sanjari na kubadilishwa hakimu wa kuisikiliza kesi hiyo.
Mwendesha Mashtaka Munde Kalombola mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sachore aliiomba mahakamani kuwa upande wa mashtaka hawezi kuendelea kusikiliza kesi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha Sheria Na. 91(1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Hakimu aliridhia ombi la mwendesha mashtaka kufuta shtaka lililokuwa likimkabili Scorpion.
Shtaka jipya ambalo Scorpion anashtakiwa nalo ni unyang’anyi wa kutumia silaha alilolitenda Septemba 6 mwaka huu Buguruni Shell kisha kumchoma na kisu mlalamikaji Said Ally Mrisho machoni, mabegani na tumboni.
Awali Mwendesha Mashtaka Chesensi Gavyole mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alimpora mlalamikaji ambaye hakuwepo mahakamani hapo vitu vya thamani na fedha taslimu vyote vikiwa na jumla ya Sh. 476,000.
Mshtakiwa alikana kuhusika na kosa hilo.
Hakimu alisema kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria Na. 148(5)(a)(i) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mshtakiwa hawezi kupata dhamana hivyo atarudishwa mahabusu.
Ikumbukwe Septemba 23 mwaka huu, Scorpion alipandishwa mahakamani hapo na kufunguliwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha chini ya kifungu cha Sheria Na. 287A cha makosa ya jinai.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Scorpion aliyejipatia umaarufu ‘Mtoboa Macho’ mnamo Septemba 6 mwaka huu maeneo ya Buguruni Shell jijini hapa alimvamia na kumpora mali na fedha taslimu muathirika Said Ally Mrisho kisha kumchoma na kisu katika macho, mabegani na tumboni huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Kesi hiyo ilikuwa chini ya Hakimu Mkazi Adelf Sanchore na Mwendesha Mashtaka Munde Kalombola ambao wameisimamia hadi Oktoba 19 mwaka huu.

HALI ILIVYOKUWA MAHAKAMANI
Umati wa watu walikusanyika tangu asubuhi kusubiri kusikilizwa kwa kesi hiyo ambapo Karandinga la Magereza lilitinga mahakama hapo saa 2:09.
Scorpion alishuka kutoka kwenye karandinga hilo saa 2:19 asubuhi akiwa katika kanzu nyeupe na barghashia yenye rangi nyeupe, njano na bluu.
Kilichowastaajabisha watazamaji  wakati anashuka alikuwa akitabasamu chini ya ulinzi mkali.
Baadhi ya watazamaji walifura kwa hasira, wengine wakiendeleza minong’ono ya kulaani kitendo hicho.
Saa 3:10 asubuhi kesi hiyo ilitua mezani Hakimu Mkazi Adelf Sachore  chini ya Mwendesha Mashtaka Munde Kalombola.
Ilitumia dakika tano tu kusikilizwa hadi kufutwa kwake.
Jambo la kushangaza lilikuwa pale wakati mwendesha mashtaka alipokuwa akitamka Kifungu cha Sheria Na. 91(1),  wingu lenye manyunyu ya mvua lilishuka kwa ghafla kisha umati wa watu uliokuwa madirisha kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo kutafuta mahali pa kujisitiri.
Hata hivyo alipomaliza kusoma na Hakimu Sachore kuridhia kufutwa kwa kesi hiyo manyunyu hayo yalikata ghafla na miale ya jua ikaendelea kupenyeza katika miili ya watu.
Baada ya kesi hiyo kufutwa Scorpion alirudishwa mahabusu kisha majira ya saa 6:19 mchana kukiwa na jua kali alipandishwa mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule chini ya Mwendesha Mashtaka Chesensi Gavyole kusomewa mashtaka mapya.
Kabla ya kusomewa mashtaka hayo Scorpion alifunguliwa pingu alizofungwa mikononi mwake na Askari Polisi huku umati mkubwa ukifuatilia kwa karibu.
Ilimchukua dakika nne tu hakimu kuisikiliza kesi hiyo, kisha Scorpion akaondolewa mbele ya korti na kurudishwa mahabusu.

Wednesday, October 19, 2016

‘Panya Road’ afufuka mochwari

TEMEKE, DAR ES SALAAM 
MKAZI wa Buza wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Isaack Ernest (16), miongoni mwa wahalifu wa kundi la ‘Panya Road’ amefufuka katika Chumba cha Kuhifadhi Maiti cha Hospitali ya Temeke siku chache baada ya kufikishwa hapo kama maiti.
Tukio hilo la aina yake lililotokea siku chache baada ya kijana huyo kufikishwa hospitalini hapo kutokana na kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kuhusika matukio ya kuiba, kujeruhi na kuharibu mali.
Oktoba 15 mwaka huu katika maeneo ya Sabasaba, Mbagala vijana sita walikamatwa na kushambuliwa na wananchi kwa tuhuma za kupora watu waliokuwa wakipita maeneo hayo.
Kikundi hicho cha vijana kilichojitambulisha kwa jina la Taifa Jipya kilianza kufanya uhalifu huo baada ya kumalizika kwa Tamasha la Kuinua Vipaji vya Muziki liliandaliwa na Clouds FM katika viwanja vya Zakheim jijini hapa.
Katika tukio hilo mkazi wa Yombo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nuruakim Kelvin Nyambocha (14), aliuawa kwa kuchomwa moto huku watano wakijeruhiwa vibaya kutokana na kipigo hicho.
Aidha miongoni mwao mkazi wa Kilungule Seleman Hamis (16), alifariki dunia akiwa katika chumba cha upasuaji mdogo katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke huku mkazi wa Buza kwa Lugenge ambaye ni fundi gereji Faraji Suleiman (19) alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi ambako yupo hadi sasa.
Akisimulia mkasa huo jana jijini hapa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe Isaack (miongoni mwa waliopokea kichapo na kudhaniwa kuwa amekufa kisha kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Temeke) akiwa mikononi mwa polisi jinsi alivyoshawishiwa kujiunga na ‘Panya Road’ hadi kukutwa na masahibu hayo
anasimulia kuhusu namna ‘Panya Road’ walivyomshawishi kujiunga nao.
“Mimi nakaa Buza, Jumamosi tulikuwa Zakheim kulikuwa na shoo tulikwenda na wenzangu wakati wa kuondoka, wakaniambia kama kula tunakula mimi nikawaambiaje, kula mi sijiwezi kama kula kuleni,” alisema Isaack kuongeza
“Wakaanza kuniambia kuwa mimi nina under fear (ninaogopa), na wakasema na tukila hatukugei mali nikwaambia kama kula kuleni mi sijiwezi…mi nikapita njia nyingine na wenyewe kivyao, kila walipopita walikuwa wanaiba.”
Pia kijana huyo mwanafunzi wa kidato cha tatu katika sekondari ya Lumo jijini hapa anaendelea kusema, “Walivyopita njia nyingine mmoja wakamwitia kelele za mwizi, akapigwa asa mi nikawa nipo ng’ambo nyingine, nikamwona mwingine wengine wakavuka ng’ambo nilikuwapo mimi na kutangulia wengine wakaangukia bondeni, sasa nikaonekana mimi wakaniitia kelele za mwizi kustuka nikajikuta nipo mochwari.”
Isaack anahitimisha kwa kusema, “Mpaka dakika hii nipo hapa…sitarudia vitendo vya wizi kwani nilishawakataa na kwasababu mimi bado mwanafunzi…bado napenda maisha yangu.”
Kwa upande wake mzazi wa Isaack ambaye ni mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Buza anasema hakuwahi kumuona kijana wake akijihusisha na masuala ya wizi kwani katika mtaa wao wamekuwa wakishirikiana na Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

JESHI LA POLISI
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Temeke Gilles Muroto alisema kijana alizindukia mochwari yupo mikononi mwao na baada ya mahojiano ya muda mrefu amewasaidia kujua mtandao wa kundi lao.
“Kijana huyu ametusaidia kuwapata vijana wengine kumi na tunao tunatarajia kuwapandisha mahakamani kujibu mashtaka yao,” alisema Muroto.
Aidha Muroto alisema katika msako walioufanya wamewakamata vijana 16 wakiwa na mapanga na bendera ya kundi lao iliyochorwa na kuandikwa ‘Taifa Jipya…Makali yanaendelea…”
Hata hivyo kamishna huyo alisema wamewaita wazazi wa watoto hao na wamefika katika makao makuu ya Kipolisi Temeke jana ambao watapandishwa mahakamani muda wowote wiki hii kutokana na kukiuka sheria ya watoto ya mwaka 2009 kifungu cha saba hadi tisa.

Aidha Muroto alisema kifungu cha 14 cha sheria hiyo kinatoa adhabu kwa mzazi atakayeshindwa kutekeleza hayo atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atapewa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela au faini ya Sh. Milioni 5.

Imeandikwa katika Gazeti la Tanzania Daima ISSN 0856 9762 Toleo Na. 4337 Jumatano Oktoba 19, 2016 Uk. 2

‘Scorpion’ kupandishwa korti leo

NA MWANDISHI WETU
Salum Njewete
MSHTAKIWA wa unyang’anyi wa kutumia silaha Salum Njwete (34) maarufu Scorpion anatarajiwa kupandishwa tena katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo.
Scorpion anapandishwa kortini kwa mara ya tatu baada ya kesi yake kuahirishwa Oktoba 7 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka  kuiambia mahakama upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa serikali Munde Kalombola mbele ya Hakimu Adelf Sachore kuwa Septemba 6 mwaka huu katika maeneo ya Buguruni Shell jijini Dar es Salaam mshtakiwa alimvamia na kumchoma visu kwenye macho, tumboni na mabegani Said Mrisho kinyume na Kifungu cha Sheria Na.287A sura ya 16 ya makosa ya jinai.
Mwendesha mashtaka alidai mshtakiwa alimpora mkufu wa fedha gramu 38 wenye thamani ya Sh. 60,000; kidani cha mkononi chenye thamani ya Sh. 85,000 na fedha taslimu Sh. 331,000.

Kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya kwanza Septemba 23 mwaka huu.

Imeandikwa katika Gazeti la Tanzania Daima ISSN 0856 9762 Toleo Na. 4337 Jumatano Oktoba 19, 2016 Uk. 6

Tuesday, October 18, 2016

Jela miaka 30 kwa kubaka mlemavu

ILALA, DAR ES SALAAM
MAHAKAMA ya Wilaya Ilala jijini hapa imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Pugu Bangulo Mathayo Mtanga (20) kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 14.
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Florah Haule alisema kesi hiyo ilifika mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 21, 2015 na mshtakiwa alitenda kosa hilo Mei 28, 2015 eneo la Bangulo kwa msichana huyo ambaye ni bubu na kiziwi.
Aidha Hakimu aliongeza kusema ushahidi wa maandishi aliokiri katika mahojiano yake na Polisi baada ya kukamatwa, mashahidi wanne na PF3 viliithibitishia mahakama pasipo shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa.
Awali Mwendesha Mashtaka Chesensi Gavyole alidai mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa hana rekodi ya makosa ya jinai  hivyo adhabu kali itolewe kwa kitendo alichokifanya.
Aidha Agosti 11 mwaka huu mshtakiwa alidai katika utetezi wake kuwa mama wa mlalamikaji ni jirani yake na kwamba muathirika aliwahi kumkuta chumbani kwake na akamuuliza alichokifuata kuwa ametumwa na mama yake hela, akamtaka aondoke na iwe mwisho.
Mshtakiwa aliongeza haikuishia hapo baada ya majuma mawili muathirika alimkuta tena chumbani alipomwamuru atoke alianza kulia na siku moja iliyofuata akiwa kazini alifuatwa na polisi na kuambiwa kuwa amebaka.

Akiwa kituo cha polisi aliambiwa atoe laki tano ili kumaliza kesi hiyo lakini hakuwa nayo wakamtaka laki mbili lakini nayo hakuwa nayo hadi kufikia anahukumiwa hakuweza kutoa chochote.

Monday, October 17, 2016

Shahidi wa tukio la wizi Tabata Bima asimulia

ILALA, DAR ES SALAAM
SHAHIDI namba moja wa tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha lililotokea Tabata Bima jijini Dar es Salaam Antimi Kimati ameiambia Mahakama ya Wilaya ya Ilala kuwa alimwona mtuhumiwa namba moja Amir Mohamed ‘Songambele’ akiwa na bunduki siku ya tukio.
Kesi hiyo ilifika mahakamani hapo Aprili 21 mwaka huu na kufunguliwa jalada CC. 88/2016
Washtakiwa wanne Songambele (52), Juma Kassim Mwishehe (50), Hassan Seleman Said  (45) na Denis Charles Chacha (32) walipandishwa kortini kujibu mashtaka yanayowakabili.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja ilianza kwa Mwendesha Mashtaka Florida Wenceslaus kuiomba mahakama kuanza kusikiliza ushahidi wa unyang’anyi wa vocha zenye thamani ya laki  tatu (300,000) na fedha taslimu milioni mbili na laki nane (2,800,000) mali ya Matola Asenga katika tukio lililotokea Januari 31 mwaka huu.
Pia Mwendesha Mashtaka aliiomba mahakama kupokea vithibitisho ambavyo ni vitambulisho na maandishi ya awali ya kukiri kwao kutenda tukio hilo walipohojiwa na polisi.
Baada ya kuapa kuwa atasema kweli kuhusu tukio hilo, Hakimu alimtaka shahidi huyo kuanza kutoa ushahidi wake.
Shahidi huyo aliiambia mahakama kuwa wakati tukio lilipokuwa likitokea alikuwa ni mfanyakazi wa Grocery iitwayo Container Pub iliyopo Tabata Bima.
Akiwa na wenzake katika kontena akiendelea kupanga vinywaji kwenye friji ghafla alisikia mlio wa risasi, alipoangalia nje, watu wote walikuwa chini ya ulinzi mmoja tu akiwa amesimama na bunduki.
Antimi alidai kwasababu taa zilikuwa zikiwaka aliiona sura ya aliyeshika bunduki, alipoinua uso wake walitazamana uso kwa uso ndipo aliponyooshewa mtutu wa bunduki na kupiga risasi aliyoikwepa na kuishia kutoboa TV.
Alipodondoka Antimi alidai alitembelea magoti na kupita kwa kutumia mlango wa nyuma ambako alijificha.
Hata hivyo Machi 7 mwaka huu, aliitwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata ili kuwatambua watuhumiwa wa ujambazi kama kuna miongoni mwao aliyehusika na tukio la Januari 31 mwaka huu, ndipo alipomtambua mtuhumiwa namba moja wa kesi hiyo ya unyang’anyi.

Kesi hiyo itasikilizwa tena Oktoba 31 mwaka huu ambapo inatarajiwa kuendelea kusikiliza ushahidi.

Thursday, October 13, 2016

Dk. Didas Masaburi is no more

CHANIKA, DAR ES SALAAM

Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi amefikwa na umauti jana majira ya saa tatu na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake, Dk. Makongoro Mahanga ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za msiba huo na kwamba leo watatoa taarifa rasmi na taratibu nyingine.
“Taarifa za kifo cha Dk. Masaburi ni za kweli ingawa sijaenda hospitali, ninafanya mawasiliano na familia lakini taarifa kamili kuhusu msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye tutamteua usiku huu, na kesho (leo) tutaeleza kiundani,” Alisema Dk. Mahanga jana usiku.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (CCM) alisema kifo cha mwanasiasa huyo ni pigo kwa chama pamoja na wakazi wa Dar es Salaam.
“…alikuwa Muhimbili kwa siku kama tano pale ICU…tunamuombea mwenzetu ambaye ametangulia mbele ya haki,” liliandika gazeti la Mtanzania ISSN 0856 5679 Toleo Na. 8334 Uk. 3
Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Aidha asubuhi ya leo Ikulu ya Rais John Magufuli imetuma salamu za rambirambi kwa wafiwa.
Masaburi atakumbukwa kauli tata kwani Agosti 6, 2011 aliingia kwenye malumbano na wabunge wa jiji la Dar es Salaam ambao walimtaka ajiuzulu wadhifa wake wa Umeya kutokana na kukiuka taratibu katika uuzwaji wa Shirika la Usafir Dar es Salaam (UDA)

Kutokana na hali hiyo Dk. Masaburi kama wengi walivyokuwa wakimfahamu alijibu mapigo dhidi ya wabunge hao ambapo alisema baadhi yao wanashindwa kufikiria kwa kutumia vichwa na badala yake wanafikiri kwa kutumia ‘makalio’.