Friday, October 21, 2016

Dereva wa daladala jela miaka 7

ILALA, DAR ES SALAAM
MAHAKAMA ya Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu dereva wa daladala mkazi wa Ubungo wa External Mohamed Amir Ramadhani kwa wizi wa Sh. 6,700,000.
Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja alisema ushahidi wa mahakama umethibitisha bila shaka yoyote kuwa mnamo Mei 5, 2015 eneo la Gongo la Mboto aliiba begi lililokuwa na fedha taslimu milioni sita na laki saba.
Kiyoja aliongeza kuwa Mohamed alifanya wizi huo kwa kuvunja kioo cha gari Na. T768 CJX aina ya Toyota Harrier mali ya Ally Ngaboli kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 258 na 265 cha Kanuni ya Adhabu
Kiyoja alisema shahidi wa kwanza akiwa Gongo la Mboto eneo la Majumbasita alipaki gari lake ili kununua matunda aliporudi alikuta wamevunja kioo.
Hakimu alisema mashahidi wengine waliiambia mahakama kuwa walishuhudia wizi huo na kumsaidia shahidi namba moja kumkamata mwizi kisha kumfikisha kituo cha polisi kwa hatua zaidi.
Awali mwendesha mashtaka Florida Wenceslaus aliiomba mahakama kuwa mshtakiwa apewe adhabu kali ili iwe fundisho kutokana na kutokuwa na historia ya makosa ya jinai.
Akijitetea Mohamed aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa ni mgonjwa wa kifafa, familia yake inamtegemea wakiwamo watoto anaowasomesha na kuwalipia ada pia baba yake ni mzee na mama yake ni mgonjwa wa shinikizo la damu na kisukari.
Hata hivyo kujitetea kwake hakumzuia Hakimu kumtupa jela miaka saba.

1 comment:

  1. Great and I have a super supply: Whole House Remodel Cost for home renovation

    ReplyDelete