Chumba cha tatu cha Bweni la Makka katika shule ya Kaloleni Islamic Smeinary baada ya kuzimwa kwa moto. Picha na Jabir Johnson/JAIZMELA correspondent
Zaidi ya wanafunzi 50 wa kike, Shule ya Sekondari ya Kaloleni Islamic ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kuungua na moto baada ya bwenì walilokuwa wakiishi kulipuka moto leo saa saba mchana.
Taarifa za wafanyakazi na majirani
wa karibu na shule hiyo ndio waliofanikisha ujio wa haraka wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji ambalo lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto
katika bweni hilo la wasichana lenye vyumba 20.
Wakiwa katika huzuni kuu kutokana
na viaa vyao kuungua moto, Wanafunzi wa kike shuleni hapo walipata fursa ya
kuzungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo ambapo lamic
Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa
ni wanafunzi wa chumba cha tatu ndani ya bweni kilicholipuka moto kuwa na vifaa
vinavyolipuka.
Akizungumza na vyombo vya habari
katika eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jeremiah
Mkomagi amesema hakuna majeruhi yaliyojitokeza licha ya vifaa vya wanafunzi
yakiwamo madaftari, magodoro.
“Majira ya saa 7 na dakika 17
mchana tulipata taarifa za tukio la moto katika shule hii kutoka kwa mtu
aliyejitambulisha kwa jina la Urio, kikosi kilichokuwepo zamu kilifika na
kusaidiana na wafanyakazi na majirani kuzima moto,” alisema Mkomagi.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo
Mohammed Hussein Migeto amesema wakati tukio la moto linajitokeza alikuwa nje
ya shule na alirudi haraka na kuchukua hatua stahiki kuhakikisha wanafunzi wapo
salama licha ya wawili miongoni mwao kupata mshtuko na kukimbizwa hospitalini.
“Wanafunzi wawili walipata mshtuko
baada ya kusikia kelele za moto kutokana kwa wanafunzi wenzao wakati wakiwa
msikitini,…” aliongeza Mwalimu Migeto.
Hii ni mara ya pili kwa shule hiyo
ya Kiislamu kupatwa na janga la moto; Moto katika shule unaweza kuwa na athari
kubwa kwa jamii nzima; Jamii inaweza kukosa huduma muhimu za elimu kwa
wanafunzi ambao wanashindwa kurudi shule kwa sababu ya uharibifu unaojitokeza
wakati wa majanga ya moto.