Chama Cha Soka Manispaa
ya Moshi (MMFA) mkoani Kilimanjaro kimepokea kwa shangwe kuu marekebisho
yanayoendelea ya Uwanja wa Soka wa Railway.
Hatua ya kufanya
marekebisho ya uwanja vya soka wa Railway yanatoa taswira kadhaa muhimu kuhusu
maendeleo ya michezo, usimamizi wa miundombinu, na mwelekeo wa kijamii na
kiuchumi katika mji.
Akizungumza uwanjani
hapo Katibu wa MMFA Mwalimu Japhet Mpande amesema marekebisho yanaonyesha
dhamira ya Manispaa ya Moshi kuboresha mazingira ya michezo kwa vijana na
wakazi wake.
Mwalimu Mpande amesema yote
yanaonesha kuwa Moshi inajitahidi kufikia viwango bora vya michezo na kuvutia
mashindano ya kitaifa, pia inaweza kusaidia vijana wengi kujiingiza katika
michezo kitaaluma au kupata ajira kupitia michezo.
………
Aidha Mwalimu Mpande
ameongeza kuwa marekebisho ya viwanja mara nyingi huambatana na mpangilio mzuri
wa mazingira ambapo yataongeza mvuto wa Manispaa ya Moshi kama sehemu inayojali
mazingira na ustawi wa jamii.
Kwa upande wao wakazi
wa Njoro uliopo uwanja wa Railway wamepokea kwa furaha na kutoa pongezi lukuki
kwa Meya wa Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Kidumo ambaye ni Diwani wa Kata ya
Njoro.
Aidha wakazi hao
wameapa kuulinda uwanja huo ikiwamo tabia mbaya za udokozi, pia watu kukatisha
uwanjani ili uendelee kuwa lulu kwa kata ya Njoro na Manispaa ya Moshi kwa ujumla.
…………….
Gharama za ukarabati
huo bado hazijawekwa wazi mpaka utakapokamilika na taarifa rasmi kutolewa.
Viwanja bora vinaweza
kuleta fursa za biashara ndogondogo (mfano wauzaji wa vyakula, vinywaji, mavazi
ya michezo) na kuongeza mapato ya halmashauri kupitia kodi na matumizi ya
viwanja kwa shughuli mbalimbali.
Uwanja wa Railway
unafanyiwa marekebisho ikiwa ni takribani miongo minne kupita licha ya kwamba
umekuwa ukitumiwa katika mashindano mbalimbali ikiwamo Zuberi Cup.
0 Comments:
Post a Comment