Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amewataka wananchi kutambua kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) sio Chama kinachosubiri kuzungumza na wananchi wakati wa Uchaguzi.
Komredi Makonda amesema CCM Iko katika ziara ya mikoa 20 huku mkoa wa Kilimanjaro ukiwa wa Nne katika kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi na kuwaeleza wananchi kazi ambazo zimefanywa na Serikali ya Awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha akiwa wilayani Same katika ziara yake akitokea mkoa wa Tanga, Komredi Makonda amewaonya Watendaji Wazembe , Wababishaji na wale wanaonyanyasa wananchi, kuwa watawashughulikia kikamilifu kwa kuwatambua kwa majina yao.
Komredi Makonda amesema watendaji wa serikali katika idara muhimu kama Afya, Maji, Ardhi na Umeme watashughulikiwa ipasavyo kwa majina wao.
Pia Mbunge wa Same Magharibi Dkt. David Mathayo amesema anamshukuru Rais Samia kwa jinsi alivyowasaidia wananchi wa Kata ya Hedaru kutatua changamoto ya Kituo cha afya.
Hata hivyo Dkt. Mathayo ameomba mji wa Hedaru upandishwe hadhi ya kuwa mji mdogo kutokana na idadi ya watu inavyozidi kuongezeka kwa idadi ya watu siku baada ya siku.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wa rais mkoa umepata Sh bl 821 kwa zaidi ya miaka 25 mkoa haujawahi kupata fedha hizo.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Komredi Paul Makonda akiwa Same, mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya siku mbili kati ya mikoa 20 nchini Tanzania. |
0 Comments:
Post a Comment