LOGO ni
nembo. ni kitu cha muhimu sana katika biashara yako, watu wengi hawajui maana
ya kuwa na logo. Logo ni utambulisho wa brand yako au ni utambulisho wa kile
unachokifanya.
Nembo au
logo ni picha ya msingi ya bidhaa na kampuni yako. Utambulisho wa biashara,
kampuni yako au bidhaa unaonyeshwa kupitia nembo yako, ambayo ni pamoja na jina
la kampuni yako. Hivyo, nembo ni moja kati ya mambo makuu ambayo yanafanya
biashara yako kukumbukwa na kutambulika. mfano hapo chini nimekuwekea baadhi ya
logo, pamoja sijaandika ni logo za kampuni gani lakini umesha fahamu ni za
kampuni gani.
Logo ni
utambulisho wa biashara yako yaani mtu hata kama hakufahamu wewe anakua kesha
fahamu biashara yako kwa kuwa logo inauza au inafanya mauzo bila wewe kuwepo. Mfano
kuna watu wanatumia logo ya mtu maarufu kuuza bidhaa zake na wewe unaponunua
unanunua kwa sababu unanunua bidhaa inayofahamika, mfano vifaa vya yamaha bei
yake ni kubwa tofauti na vifaa vingine kutokana na umaarufu wake. Logo yako
ikiwa maarufu hata kama utaondoka duniani bado watoto wako wataendelea kuuza
bidhaa kwa kutumia logo yako.
Logo inaweza
kuwa maarufu kuliko wewe mwenyewe.
0 Comments:
Post a Comment