Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Monday, August 29, 2022

Ngumi kufufuliwa upya Kilimanjaro

 

Chama cha mchezo wa ngumi, Kanda ya Kaskazini (KBA),umepania kuurejesha mchezo huo baada ya kipindi kirefu kupotea  kutokana na vijana wengi kutokujitokeza kushiriki pambano hilo.

Katibu wa mchezo wa Ngumi mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Taifa wa maandalizi Ngumi Frank Francis, amesema hayo jana wakati wa uzinduzi wa mchezo wa ngumi  uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mawenzi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro

Amesema kutokana changamoto mbalimbali za kiutendaji kutoka kwa baadhi ya viongozi wa mchezo huo, zilipelekea kupoteza ya sifa yake Kitaifa na Kimataifa na kudidimiza maendeleo yake hapa nchini.

Francia ametumia fursa hiyo ya kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki mchezo huo wa ngumi ambapo kwa sasa chama hicho kimeamua kurejesha heshima ya mikoa hiyo ya Kanda ya Kaskazini.

“Ngumi ni miongoni mwa michezo ambayo imeitangaza na kuipa heshima nchi yetu ya Tanzania duniani, kutokana na mabondia wake kuonyesha uwezo mkubwa na kushinda katika mapambano mbalimbali ya Kimataifa,”amesema.

Amesema mchezo wa ngumi Kanda ya Kaskazini kwa kipindi kirefu ulipotea baada ya vijana wengi kutojitokeza kushiriki pambano hilo na hivyo wameamua kufufua na kuinua mchezo wa ngumi katika Kanda ya Kaskazini ili vijana wengi waweze kushiriki mchezo huo.

Aidha ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau wa mchezo wa ngumi kuwasaidia vijana walioonesha nia ya kucheza mchezo huo kupata viwanja vya kufanyia mazoezi ya ngumi sanjari na kuwapatia vifaa vya mchezo huo.

Naye Bondia mstaafu mkoa wa Kilimanjaro Emmanuel Mushi amesema wameandaa pambano hilo la ngumi kimkoa ili kukuza vipaji vilivyopo ili kuwasaidia vijana waweze kupata ajira

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa Chama cha Ngumi Mkoa wa Kilimanjaro (KBA), Malonga Kitika amesema ukosefu wa viwanja vya mchezo wa ngumi pamoja na upungufu wa vifaa vya mchezo huo, umekuwa chanzo kikubwa cha vijana wengi kurudi nyuma kushiriki mchezo wa ngumi na kutoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kuwapatia maeneo yao ili waweze kufanyia mazoezi ya mchezo huo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bomang’ombe Wilaya ya Hai Evod Njau, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo, amewashauri madiwani kuhakikisha kila kata wanayoiongoza kuhamasisha vijana chini ya umri mdogo kuanza kushiriki mchezo wa ngumi ili taifa liweze kupata wachezaji bora ambao wataweza kushindana na kuweza kuleta medani za mchezo huo.

Mchezo wa ngumi ni miongoni mwa michezo inayofahamika na kupendwa na watu wengi duniani, kama ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa miguu, mchezo huu umekuwa ni chanzo cha ajira na hivyo kujipatia umaarufu mkubwa ambapo vijana wengi wanajiunga kwa lengo la kujipatia kipato.

Mchezo wa ngumi nchini Tanzania ulianza kufahamika katika miaka ya 1950 ambapo miaka ya 1970 mabondia wake walianza kufahamika katika mashindando mbalimbali ya Kimataifa.

Medali ya kwanza ya Kimataifa ililetwa na Titus Simba mwaka 1974 katika michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika nchini Uingereza na mwaka 1998 bondia mwingine Michael Yombayomba aliiletea Tanzania medali nyingine katika mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika nchini Malaysia.








Tuesday, August 16, 2022

Uwekezaji wa bilioni 429.1 kuboresha Bandari ya Tanga waanza kuzaa matunda

 

Afisa Uhusiano wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi kuhusu maboresho yaliyofanyika tangu mwaka 2019 hadi sasa


Uwekezaji wa bilioni 429.1 kwa ajili ya uboreshaji wa bandari ya Tanga umeanza kuzaa matunda baada ya mkandarasi kukabidhi ujenzi wa wa gati wenye urefu wa mita 200 ambao utaruhusu bandari hiyo kongwe kuhudumia meli zisizozidi mita 200 gatini kwa wakati mmoja.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania  (TPA) iliamua kutenga kiasi hicho cha fedha ili kutekeleza mradi mkubwa na wa kimkakati  katika bandari ya Tanga ambao unatekelezwa kwa awamu mbili. 

Nchi jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimeanza kutumia bandari ya Tanga kupitishia mizigo yake kutokana na maboresho ya bandari hiyo yanayoendelea ya upanuzi wa bandari hiyo, huku nchi nyingi zaidi zikitarajiwa kutumia bandari hiyo.

Rwanda imeanza kutumia bandari hiyo kupitishia malighafi inayotumika kutengenezea saruji huku nchi ya Burundi ikipitisha mzigo wa mafuta kupitia bandari hiyo. 

Mnamo mwanzoni mwa Agosti mwaka huu mkandarasi ambaye ni kampuni ya China Harbour Engineering (CHEC) Limited alikabidhi kipande cha urefu wa mita 200 hivyo kufanya uboreshaji wa bandari hiyo  kufikia asilimia 61.

 

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Moshi Afisa Uhusiano wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi amesema mradi huo uliwekwa katika awamu mbili za utekelezaji ambapo awamu ya kwanza ilijikita katika uchimbaji wa kina cha maji kwenye mlango wa kuingilia meli  na shemu ya kugeuzia meli kutoka mita tatu hadi mita 13.

“Aidha licha ya uchimbaji huo, ununuzi wa mitambo ya bandari (operational equipment) kwa gharama ya shilingi 172.3 bilioni ulifanyika,” amesema.

 

Awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi umegharimu shilingi 256.8 bilioni na utadumu kwa miezi 22 ulioanza Septemba 5, 2020 na unatarajiwa kumalizika Novemba 28, 2022.

 

“Awamu ya pili unahusisha ujenzi wa gati mbili zenye urefu wa mita 450 na kuongeza kuchimba kina cha maji kutoka mita tatu hadi 13 wakati wa maji kupwa

 

Bandari ya Tanga ni ya namna gani?

 

Bandari ya Tanga ni bandari kongwe iliyojengwa katika Pwani ya Afrika Mashariki na kuanza kufanya kazi mwaka 1891 wakati wa utawala wa Wajerumani katika ardhi ya Afrika Mashariki.

 

Bandari ya Tanga ni ya pili kwa ukubwa katika kuhudumia shehena baada ya bandari ya Dar es Salaam.  Bandari ya Tanga ina uwezo wa kuhudumia shehena ya jumla ya tani 750,000 kwa mwaka ikijumuisha mzigo mchanganyiko, shehena ya mafuta pamoja na shehena ya makasha kwa mwaka

 

Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imeweza kuvuka lengo kwa kuhudumia jumla ya Tabi 870,000, hata hivyo hayo ni matokeo ya awali mara baaada ya uwekezaji mkubwa wa uboreshaji wa bandari ya Tanga tangu mwaka 2019.

 

Tangu kujengwa kwake, bandari ya Tanga ilikuwa inahudumia shehena katika kina kirefu cha maji eneo la umbali wa mita 1700 kutoka gatini kwasababu ya changamoto ya kina kifupi cha maji eneo la gati ambapo kina cha maji kilikuwa mita tatu hali iliyofanya meli zishindwe kufika kwenye gati.

 

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania  (TPA) iliamua kutenga kiasi cha shilingi 429.1 bilioni ili kutekeleza mradi mkubwa na wa kimkakati  katika bandari ya Tanga ambao unatekelezwa kwa awamu mbili.  

 

TPA imejipanga vipi na bandari kavu ya Arumeru?

 

Kuhusu ujenzi wa Bandari kavu katika eneo la Malula wilayani Arumeru, ujumbe huo wa bandari ya Tanga umesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetenga bajeti ya fedha ya kufanya upembuzi yakinifu katika mwaka huu wa fedha 2022/23.

 

Ujumbe wa kueleza uboreshaji uliofanyika katika bandari ya Tanga uliongozwa  na Afisa Uhusiano Peter Milanzi, Afisa Masoko Mkuu Rose Tandiko na Mhandisi wa Bandari hiyo,Hamis Kipalo.

 

Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro imekuwa wanufaika na ziara hiyo ya taarifa ya maboresho ya bandari ya Tanga tangu mwaka 2019.

 

Afisa Masoko Mkuu wa Bandari ya Tanga Rose Tandiko akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matunda yaliyoanza kupatikana baada ya uwekezaji wa shilingi 429.1 bilioni bandari hapo.

Mhandisi wa Bandari ya Tanga Hamisi Kapilo

Hecton Chuwa, mwandishi wa Daily News akiuliza swali kwa ujumbe wa TPA Bandari ya Tanga uliofika mjini Moshi kuzungumza na waandishi wa habari.


Bahati M. Nyakiraria, Mwenyekiti wa Kilimanjaro Press Club (MECKI) akizungumza na ujumbe wa Bandari ya Tanga 

William Ruto, Rais Mteule wa Kenya, amshinda Odinga kwa asilimia mbili


Rais mteule wa Kenya William Ruto ameshinda uchaguzi ambao ulikuwa na ushindani mkali katika historia ya Kenya.

William Ruto alimshinda mpinzani wake aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga ambaye alikuwa anawania urais kwa mara ya tano.

Ruto alishinda kwa asilimia 50.49 ya kura huku Odinga akiachwa kwa asilimia mbili tu.

 

Uchaguzi huo hata hivyo ulifanyika wakati ambapo taifa hilo lenye uchumi mkubwa Afrika mashariki linakabiliwa na gharama kubwa ya maisha na ukosefu wa ajira, masuala ambayo wagombea wote wakuu walikuwa wameahidi kuyaangazia. 

William Ruto, ni miongoni mwa wanasiasa wengi wakubwa nchini Kenya walioweka wazi nia zao za kuingia Ikulu ya Kenya, kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, kurithi mikoba ya aliyekuwa 'swahiba wake', Uhuru Kenyatta.

 

Mwanasiasa huyu tajiri ambaye amekuwa na ndoto za kuwa Rais wa Kenya, amekuwa akikutana na vikwazo lukuki vya kisiasa, ikiwemo kuzuiwa kwa sababu ama kuzuiwa kwa makusudi kufanya shughuli kadhaa za kisiasa na binafsi kutokana na msukumo wa kisiasa. 

Ni miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini humo, walioweka wazi nia zao za kuingia Ikulu ya Kenya, kupitia uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022, kurithi mikoba ya 'swahiba wake', Uhuru Kenyatta.



 

Saturday, August 13, 2022

Chongolo atimiza ahadi ya mabati 70 Kaloleni Moshi

 

Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi Ibrahimu Mjanakheri na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kaloleni Joshua Kojo katika kukabidhi mabati 70 kwenye kata ya Kaloleni, Manispaa ya Moshi kwa niaba ya Katibu wa CCM Taifa Daniel Chongolo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametimiza ahadi yake ya mabati 70 aliyoitoa, alipotembelea ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Kaloleni Manispaa ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro, wakati wa ziara yake ya kukagua, kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 pamoja na kuhimiza uhai wa chama ngazi za Mashina na Kata.

Akikabidhi mabati hayo kwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kaloleni Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi Ibrahimu Mjanakheri, alisema Katibu Mkuu Chongolo ametimiza ahadi yake ambayo aliiitoa hivi karibuni wakati alipotembelea ofisi hiyo na kuahidi kuchangia mabati 70.

“Nimekuja hapa leo kukabidhi ahadi ya Katibu mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo, aliyoahidi hivi karibuni wakati wa ziara yake ya kukagua, kutembelea na kuangalia uhai wa chama katika Manispaa yetu ya Moshi, naomba kuwakabidhi mabati 70 ikiwa ni ahadi ya Katibu Mkuu wetu wa chama taifa,”alisema Mjanakheri.

Akipokea mabati hayo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kaloleni Joshua Kojo, alimshukuru Katibu Mkuu wa CCM taifa  kwa kuwakabidhi ahadi ya mabati 70 hayo aliyoyatoa wakati alipotembelea  ujenzi wa  ofisi ya chama.

“Tunamshukuru sana Katibu mkuu kwa kutimiza ahadi yake kwa muda mfupi na leo hii ametukabidhi, wako baadhi ya watu wamekuwa wakitoa ahadi zao, lakini unapowafuatili wamekuwa hawako tayari kutoa ahadi hizo, lakini Katibu Mkuu Chongolo  ameweza kutukabidhi leo kupitia kwa Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi,”alisema..

Naye Diwani wa Kata ya Kaloleni Nasibu Mariki, alisema, walikuwa wanashindwa  kufanya mikutano yao ya chama ya  siri kutokana na kata hiyo kutokuwa na ofisi hivyo kukamilika kwa ofisi hiyo, itasaidia kuendesha mikutano ya chama wakiwa huru.

Akizungumza kwa niaba ya Makatibu Kata wa Kata za Manispaa ya Moshi, Katibu wa CCM Kata ya Rau Abdallah Mtwenge, alimpongeze Katibu wa CCM wa Manispaa ya Moshi mjini Ibrahimu Mjanakheri kwa kuja na mikakati ya kuhakikisha kila Kata inakuwa na jengo la ofisi ya chama.

“Tangu Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi aje Moshi, amekuwa akipambana kuhakikisha kila kata ambayo haina ofisi ya chama inakuwa na ofisi, kwani zipo kata nyingi zilikuwa zimeungana lakini baada ya kugawanywa zikawa hazina ofisi, baada ya kuja na kuiona changamoto hiyo akaja na wazo la kuanzisha ujenzi wa ofisi za chama kila kata ili kuweza kuimarisha chama.

Aliongeza “Mkakati huu unapaswa kupongezwa na kila mwanachama wa CCM huku akizishauri wilaya zingine ambazo hazina ofisi za chama kuiga utaratibu ambao umeanzishwa na Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi,”alisema Mtwenge.




Mwandishi wa ‘Aya za Shetani’ Salman Rushdie achomwa kisu New York

 

Mwandishi wa vitabu Salman Rushdie, ambaye amekuwa mafichoni baada kuamuliwa kuuawa na hukumu ya sheria ya dini ya Kiislamu Fatwa ya Iran, anapumulia mashine hospitalini na anaweza kupoteza jicho moja baada ya kushambuliwa jana jijini New York, Marekani.

Mwandishi huyo wa Uingereza wa kitabu cha "aya za shetani" ambacho kilizusha ghadhabu miongoni mwa baadhi ya nchi za Kiislamu walioamini kuwa ni kufuru, ilibidi asafirishwe kwa ndege hadi hospitali kwa ajili ya upasuaji wa dharura kufuatia shambulio hilo.

Mshambuliaji alipanda kwenye jukwaa ghafla na kumchoma visu shingoni na tumboni kabla ya watu waliokuwa ukumbini kukimbilia jukwaani na kumdhibiti mshambuliaji.

Kitabu chake cha "aya za shetani alichokitoa mwaka 1988 kilichukuliwa na baadhi ya Waislamu kama dharau kwa dini hiyo na Mtume Mohammed.

 

Kitabu cha ‘Aya za Shetani’ kikoje?

The Satanic Verses ni riwaya iliyotungwa mnamo mwaka 1988 na mwandishi mwenye asili ya India raia wa Uingereza Salman Rushdie. Kitabu hicho  kilitungwa na kuonyesha maisha ya Mtume wa Dini ya Kiislam Muhammad (S.A.W).

Rushdie alionyesha wasifu kwa kutumia aya za Koran akiwajumuisha miungu watatu wa Makka; Allāt, Al-Uzza, na Manāt. Aidha upande mwingine wa riwaya hiyo ilitumia taarifa za wanahistoria wa kale al-Waqidi na al-Tabari.

Nchini Uingereza kilipokea tuzo mbalimbali ikiwamo ya mwaka 1988 Whitbread baada ya kushindwa kutwaa tuzo ya Booker ya mwaka 1988 licha ya kufika fainali ikipitwa na ile ya Peter Carey's Oscar na Lucinda.

Waislamu wanaichukulia riwaya hiyo kuwa inakufuru dini ya Uislamu na Mtume Muhammad SAW.

Nchini India kilipigwa marufuku kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kauli za chuki dhidi ya Uislamu.

Katibu Mkuu CCM Taifa aipongeza halmashauri ya Mwanga

Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kwa kushika nafasi ya Nne na kufanikisha kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato na matumizi, utoaji wa mikopo ya asililimia 10%, ujibuji wa hoja za CAG, usimamizi wa matumizi ya fedha za marejesho na matumizi ya tovuti.

Katibu Mkuu wa (CCM), Taifa Daniel Chongolo, aliyasema hayo hivi karibuni  wilayani humo, wakati akizungumza na viongozi wa chama na serikali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za chama hicho wilayani humo.

Chongolo ameipongeza Halmashauri ya Mwanga chini ya Mkurugenzi  mtendaji Mwajuma Nasombe, kwa kuweka rekodi ambayo haijawahi kutokea na kuwa halmashauri  ya  Nne Kitaifa, baada ya tathmini ya jumla iliyofanywa na TAMISEMI ya kupimwa utendaji kazi wa Wakurugenzi kwa vigezo vitano  ikiwemo ya ukusanyaji wa mapato na matumizi, mikopo ya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Niipongeze halmashauri ya Mwanga chini ya Mkurugenzi mtendaji Mwajuma Nasombe, kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi ya halmashauri kwa kipindi cha robo ya nne ya Mwaka 2021/2022 na kuzielekeza fedha hizi kwenye miradi ya maendeleo,” alisema Chongolo.

 Alisema ili kufanikisha maswala ya maendeleo ni lazima viongozi wote waondoe ubinafsi na kwamba urafiki ndani ya kazi ndiyo msingi wa maendeleo.

Chongolo aliendelea kusema kuwa changamoto kubwa miongoni mwa watumishi wengi wa Serikali ni kukosa umoja miongoni mwao, huku wengine wakihangaika kuchunguza makosa ya mtu mmoja mmoja jambo ambalo alisema huchangia migogoro kazini.

 Aliongeza “Hali ya tulikotoka tunaijua, hapa tulipofikia hakuna mtu anaempongeza Mkurugenzi kwa kazi nzuri aliyoifanya  kila mmoja anakwenda kivyake, tujenge tabia ya kupongezana pindi mtu anapofanya kazi nzuri kama hii,” alisistiza Chongolo.

Aidha Chongolo alitoa wito kwa madiwani wa halmashauri hiyo kuonyesha njia kwa kupongeza juhudi zinazofanywa na mkurugenzi na timu yake na kwamba penye kasosro wasisite kukosoa.

“Ni vyema mtu akifanya vizuri mkampongeza na si hayo tu kama ikitokea amekosea jambo, msiache kumkosoa na kutoa ushauri maana hakuna aliekamilika kwa asilimia 100 wala hakuna Malaika hapa”, alisema na kuongeza kila mtu ana madhaifu yake.

 Alisisitiza,  “Rais Samia  kila mara anatoa maelekezo  kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinahudumia wananchi kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo, hivyo ni majukumu yenu madiwani kusimamia watendaji wa halmashauri ili kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa”.

Kauli ya Chongolo juu ya mafanikio ya halmashauri ya Mwanga, inakuja siku chache baada ya Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa kutangaza mafanikio yaliyopatikana baada ya halamashauri za wilaya, manispaa na majiji kuvuka malengo ya makusanyo nchini ambayo nayo yalivuka lengo. 

Kwa mujibu wa Waziri Bashungwa kipindi cha Julai mwaka jana  na Juni mwaka  huu, tathmini ya ufanisi wa utendaji wa halmashauri ni alama 80 kati ya 100, tathmini hii imezingatia ukusanyaji wa mapato na matumizi mapato ya ndani.

 

Wednesday, August 10, 2022

Benedict Haule ailisha Moshi Veterans Club

 

Harusi ni jambo linalopendeza kwa kila mmoja pindi inapotokea anafanya hivyo katika maisha yake hapa ulimwenguni.

 Pia ndugu, jamaa na marafiki hufurahia pindi inapotokea mpendwa wao anafikia hatua ya kufunga pingu za maisha.

Benedict Haule ni miongoni mwa wachezaji waliofanikiwa kufunga pingu za maisha mnamo Julai 2022.

Moshi Veterans walipokea keki ya upendo kutoka kwa Benedict Haule.

Nao Moshi Veterans waliamua kuikata hadharani kusherehekea furahi hiyo chini ya Kocha Issa Rugaza.

Benedict Haule alisajiliwa na Azam FC na msimu wa 2022/23 atahudumu na Singida Big Stars zote za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL)