Nyama ikiwa katika machinjio |
Wednesday, June 28, 2017
Machinjio ya punda yafunguliwa Kenya
Machinjio ya tatu punda nchini Kenya imefunguliwa katika eneo la
Nakwaalele mjini Lodwar,katika kaunti ya Turkana. Machinjio hiyo ya kampuni ya
Zilzha kutoka China itasindika
nyama ya punda pamoja na ngozi kwa ajili ya usafirishaji hadi China na nchi
nyingine za mashariki ya mbali.
Kufunguliwa kwa machinjio hiyo utaleta ushindani wa machinjio nyingine
mbili za Maraigushu,mjini Naivasha
katika kaunti ya Nakuru,na ile iliyopo Mogotio katika kaunti ya Baringo.
Shu Jing Long,mmojawapo wa wachina wanaoendesha kichinjio cha Zilzha
cha Turkana amesema machinjio hicho itatoa ajira kwa wenyeji zaidi ya 200.
Aidha Long amesema hamu yao hasa ipo katika
ngozi ya punda ambayo ina soko kubwa nchini China .
Afisa wa Afya kutoka Wizara ya Mifugo nchini Kenya Dkt Jonathan Tanui msimamizi
wa shughuli za uchinjaji katika machinjio cha Zilzha amesema machinjio hiyo
imefikia viwango vinavyotakiwa na kuongeza kuwa wanyama hao kabla ya kuchinjwa
ni lazima wapimwe ili kuhakikisha kuwa ni salama kwa kuliwa.
Punda mmoja anauzwa katika ya shilingi 8,000 hadi 10,000 za Kenya .
Sunday, June 25, 2017
Dereva bodaboda agongwa na gari afariki dunia
Mwili wa dereva bodaboda ambao haukutambulika mara moja ukiwa umelazwa pembezoni mwa barabara mita chache kutoka kituo cha Mabasi yaendayo kwa haraka cha Morocco jijini Dar es Salaam Juni 25, 2017 |
Dereva wa bodaboda
ambaye hajafahamika jina lake na mahali anapotoka amefariki dunia baada ya kugongwa
na gari maeneo ya Kinondoni Kanisani jijini Dar es Salaam mita 200 kutoka kituo
cha mabasi yaendayo kwa haraka cha Morocco .
Mashuhuda wa tukio hilo walisema ajali hiyo ilitokea saa 1:30 usiku wa
Jumapili ya Juni 25 mwaka huu wakati dereva huyo akiwa na wenzake watatu wakiwa
katika pikipiki iliyosajiliwa kwa Na. MC 861 AHE alipogongwa na gari ambalo
lilikimbia baada ya tukio hilo .
Aidha mashuhuda hao
walisema aliokuwa amewapakiza wametokomea kusikojulikana kutokana na sheria
kukataza kupakiza ‘mshikaki’ yaani watu zaidi ya wawili.
Dereva wa bodaboda
hiyo anakadiriwa kuwa na kati ya miaka 23-30 ilishuhudiwa dimbwi la damu
barabarani hapo kutokana na kupasuka kichwa.
Jeshi la Polisi mkoa
wa Kinondoni lilifika yapata dakika tano baadaye baada ya raia wema kutoa
taarifa kuhusu tukio hilo .
Baada ya kuandika maelezo waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka
hospitalini kuuhifadhi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Hata hivyo Maofisa wa
Jeshi hilo
walisikika wakiwataka madereva wa bodaboda kuvaa kofia za kujikinga pamoja na abiria
wao ili kupunguza madhara zaidi inapotokea ajali.
Gari la Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni PT 4012 likiwa katika eneo la ajali Juni 25, 2017 |
Mashuhuda wa tukio hilo katika eneo la ajali Juni 25, 2017 |
Ofisa wa Jeshi la Polisi akichukua maelezo kutoka kwa mashuhuda wa tukio la ajali maeneo ya Kinondoni Kanisani Juni 25, 2017 |
Wasamaria wema wakisaidia kuupakia mwili wa marehemu katika gari la Polisi, Kinondoni Juni 25, 2017 |
Monday, June 19, 2017
SAA yaisaidia familia ya Mzee Sixtus Mhagama
Wanachama wa Chama cha Washehereshaji Tanzania (SAA) katika picha ya pamoja na familia ya Mzee Sixtus Mhagama Juni 19, 2017 maeneo ya Boko inapoishi familia hiyo inayougua ugonjwa wa ajabu. |
Wanachama wa SAA katika kuwatia moyo familia ya Mzee Sixtus Mhagama. |
Mzee Sixtus Mhagama akipokea fedha taslimu kutoka kwa wanachama wa SAA. |
Mtoto wa kwanza wa Mzee Sixtus Mhagama, Schola ambaye hajaathirika na ugonjwa huo akiwashukuru SAA kwa msaada walioutoa. |
Schola akiwa na mama yake ambaye kwa sasa haoni kutokana na matatizo yaliyomkuta. |
Chama cha Washereheshaji Tanzania (SAA) kimetoa msaada wa shilingi
milioni mbili zikiwamo fedha taslimu shilingi milioni 1.3 jana kwa familia moja
inayougua ugonjwa wa ajabu uliothibitishwa na madaktari kuwa haiwezekani
kutibika.
Familia hiyo watu sita ya Mzee Sixtus Mhagama ya kijiji cha Litoho
kutoka Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma
iliyohamia jijini Dar es Salaam imepatwa na ugonjwa wa ajabu unaowafanya watoto
wao kila wanapofikisha miaka mitano huanza kupata ulemavu.
Katika ushuhuda wake wakati akikabidhiwa msaada huo vikiwamo vitu
mbalimbali kama nguo, mafuta, sukari Mzee Mhagama amesema walitoka kijijini
kwao Litoho mwaka 2006 na kuja Dar es Salaam katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kwa ajili ya matibabu kutokana na hospitali zote mkoani humo kukosa
suluhisho la watoto wao.
Aidha Mzee Mhagama amesema miongoni mwa watoto hao mmojawapo
alishafiriki dunia huku wengine wakiendelea kukumbwa na ugonjwa huo ambao
unawafanya wote magamba pindi wanapokuwa katika maeneo ya baridi na maumivu
makali na mifupa yao
kushindwa kuimarika hali inayosababisha ulemavu.
Akipokea msaada huo Mzee Mhagama ameishukuru jamii kwa kumjali kwani
hata nyumba anayoishi huko Boko jijini Dar es Salaam amepewa na msamaria mwema
ili aweze kujisitiri katika hali ngumu ambapo mkewe pia amepatwa na ugonjwa huo
ambao umemfanya ashindwe kuona.
Hata hivyo amesema changamoto bado ni kubwa kwani anapaswa kwenda kila
siku Muhimbii na watoto wake ili waweze kufanyiwa mazoezi lakini kuna wakati
anashindwa kutokana na ukosefu wa fedha za kuwasafirisha wagonjwa hao.
Kwa upande wake wakati akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa SAA Emmanuel
Urembo amesema wamekuwa wakisaidia jamii kwa mwaka mara moja lakini safari hii
waliiona familia hiyo inayopata mateso makubwa japokuwa ni kiasi kidogo lakini
wanaamini msaada huo utaweza kuwafariji.
Tuesday, June 13, 2017
Korea Kaskazini yamwachilia Otto Warmbier
Otto Warmbier |
Korea Kaskazini imemwachilia huru mwanafunzi Mmarekani Otto
Warmbier ambaye alikuwa amefungwa jela katika taifa hilo
la bara Asia . Warmbier, 22, alihukumiwa
kufungwa jela miaka 15 na kazi ngumu Machi 2016 baada ya kupatikana na hatia ya
kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwenye hoteli moja. Tillerson amesema
Bw Warmbier sasa yuko njiani kurejea Marekani ambapo ataungana tena na jamaa
zake Cincinnati , Ohio . Gazeti la Washington Post limemnukuu babake
Fred akisema mwanawe wa kiume amesafirishwa kama
mgonjwa kwa sababu hana fahamu. Gazeti hilo
linasema wazazi wa Warmbier waliambiwa mwana wao wa kiume alianza kuugua
ugonjwa wa botulism, ugonjwa nadra ambao humfanya mtu kupooza, muda mfupi baada
ya kesi yake kumalizika miezi 15 iliyopita. Otto Warmbier, mwanafunzi aliyekuwa
amehitimu na shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Virginia ,
alikuwa amezuru Korea
Kaskazini kama mtalii akiwa na shirika la Young Pioneer Tours alipokamatwa 2
Januari 2016.
Rais Magufuli awafunda wakuu wa mikoa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na wakuu wa mikoa yote katika Ikulu jijini Dar es Salaam Juni 13, 2017. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mpango
wa ujenzi wa viwanda katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi kuongeza
thamani ya mazao yao na kuzalisha ajira.
Magufuli ametoa agizo hilo jana Ikulu Jijini Dar es Salaam
alipokutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara, kuwa kila Mkuu wa Mkoa anapaswa kufanyia kazi
fursa za uanzishaji wa viwanda katika eneo lake na kuhakikisha anashawishi
wawekezaji kuzitumia fursa hizo kama inavyofanyika katika Mkoa wa Pwani.
Aidha Magufuli amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuongeza juhudi za
utatuzi wa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa
kuwanyang’anya hati za umiliki wa mashamba makubwa ambayo yanashikiliwa na watu
pasipo kuyaendeleza.
Hata hivyo amewatahadharisha Wakuu wa Mikoa hao dhidi ya
watu wanaofanya njama za kujimilikisha maeneo makubwa ya ardhi na kusababisha
wakulima na wafugaji kukosa maeneo ya kilimo na malisho na ametaka wote watakaobainika
kufanya njama hizo wafichuliwe na kunyang’anywa maeneo hayo.
Ndugai atishia kuwaongezea adhabu Mdee na Bulaya
Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai |
Spika wa Bunge Job Ndugai amewapa onyo
tena wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya akisema kuwa wanapaswa kutambua kuwa
Bunge bado lina uwezo wa kuwaita na kuwahoji na kuwapa adhabu kali zaidi ya
hiyo walionayo sasa.
Onyo hilo linakuja ikiwa ni siku moja baada ya
spika huyo kusifiwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa anafanya vizuri kuwadhibiti
wabunge waropokaji bungeni na kumtaka aendelee na kasi hiyo.
Ndugai amesema kuwa ameamua kutoa onyo
hilo kufuatia wabunge hao kufanya malumbano na
bunge huku wengine wakitumia maneno ambayo sio mazuri hivyo amewashauri kuwa
wamewavumilia kwa mengi lakini kama bado huko
waliko wanaendelea na tabia hizo wanaweza kuwaita na kuwapa adhabu kali zaidi
ya hiyo waliyonayo sasa.
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya
Bunge imewaadhibu wabunge kutohudhuria vikao vyote vya Bunge linaloendelea hadi
Bunge la Bajeti 2018/2019 baada ya kuwakuta na hatia ya kudharau mamlaka ya
Spika wa Bunge.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ester Bulaya na Halima Mdee |
Monday, June 12, 2017
Acacia yamjibu JPM
Mgodi wa North Mara |
Kampuni ya Madini ya Acacia imeona matokeo ya
kushtua ikiwa ni saa chache baada ya Kamati ya Pili ya Rais iliyoundwa na Rais
John Pombe Magufuli kuwasilisha ripoti ambayo imeangazia nyanja za historia ya
kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.
Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi Machi mwaka huu na
Rais John Magufuli iliyojikita kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na usafirishaji wa
mchanga wenye madini imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi yake nchini Canada , Acacia
ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi kusajiliwa nchini, hivyo
imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.
Katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni
kutoka Ikulu, Rais Magufuli amesema Tanzania
imepoteza takriban shilingi trilioni 188 katika kipindi cha miaka 19 kati ya
mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba .
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Acacia
imesema kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha
matokeo yao na
yaliyokutwa na kamati, kwani kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10
kuliko thamani halisi ya makanikia.
Tume hiyo imetoa mapendekezo imefanya ikiwamo ya
Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba
mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo
wa marufuku ya kuuza nje tuhuma ambazo imekanusha vikali.
Aidha Acacia imesema imekuwa ikifanya biashara kwa
kufuata utaratibu na sheria za Tanzania
na kuongeza kuwa tangu kuanza kwa uchimbaji wa madini wamekuwa wakilipa
mirahaba yote inayotakiwa kulipwa na kukaguliwa kila mwaka kwa viwango vya
Kimataifa.
Hata hivyo Acacia imekaribisha mazungumzo na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgodi wa Bulyahulu |
Tanzania yapoteza Trilioni 188 makanikia dhahabu na shaba
Tanzania imepoteza takriban shilingi trilioni 188 katika kipindi cha
miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya
dhahabu na shaba.
Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi Machi mwaka huu na Rais John Magufuli iliyojikita
kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na
usafirishaji wa mchanga wenye madini imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi
yake nchini Canada, Acacia ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi
kusajiliwa nchini, hivyo imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.
Katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni kutoka Ikulu, Rais
Magufuli amemtaka Waziri wa Sheria Profesa Paramagamba Kabudi kupitia mikataba
yote ya madini.
Ripoti iliyopita ilisababisha Waziri wa nishati na madini Prof.
Sospeter Muhongo kusimamishwa kazi.
Tuesday, June 6, 2017
Mama Mghwira rasmi mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, ala kiapo Ikulu
Mama Anna Mghwira Juni 6, 2017 katika Ikulu jijini Dar es Salaam |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amemwapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mama Anna Mghwira akila kiapo cha Uadilifu wa Viongozi |
Mghwira amekula kiapo cha Uadilifu wa Viongozi
mbele ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Kiapo hicho kinafuatia
uteuzi alioufanya Rais Magufuli kwa Mwenyekiti huyo wa chama cha ACT –
Wazalendo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mapema mwezi huu. Kutokana na uteuzi
huo Mama Mghwira alilazimika kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama chake
pamoja na kujivua uanachama. Mara baada ya kiapo hicho, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira alipanda gari lake la kazini na kuelekea Mkoani
Kilimanjaro kuanza kazi rasmi. Mama Anna Mghwira anachukua nafasi ya Said Meck
Sadiq ambaye aliomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Dk John Magufuli. Mkoa wa
Kilimanjaro umepata kuongozwa na wakuu wa mkoa watatu katika kipindi cha miaka
miwili, Leonidas Gama ambaye ni mbunge wa Songea Mjini, Said Meck Sadick na
Anna Elisha Mghwira. Kabla ya hapo Mkuu huyo mpya wa mkoa alikuwa Mgombea wa
Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Uteuzi wa kushika wadhifa huo umeacha maswali lukuki miongoni mwa wafuatiliaji
wa masuala ya kisiasa kitaifa na kimataifa.
Sudan yataka kuwa msuluhishi mgogoro wa Qatar
Muonekano wa Qatar kutoka mbali |
Monday, June 5, 2017
Cisco Mtiro is no more
Cisco Mtiro enzi za uhai wake |
Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro amefariki.Taarifa ya familia
imesema Mtiro amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa
anapatiwa matibabu. Aidha msiba upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B. Enzi za
uhai wake aliwahi kugombea ubunge wa Temeke akipambana vikali na Agustino
Mrema. Mwaka 2009 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania
katika nchi za Malaysia , Ufilipino , Cambodia ,
Singapore na Laos .