Mkuu wa Wilaya ya Hai Lazaro Twange akizungumza na waandishi wa Habari Ofisi kwake, katika mji wa Mdogo wa Bomang'ombe.(Picha na; JAIZMELA) |
Mkuu Wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lazaro Jakob Twange amewataka wanasiasa watakaonza kampeni kuelekea uchaguzi Wa serikali za mitaa kuhakikisha wanaendesha siasa zao kwa mujibu Wa Sheria na kanuni za uchaguzi zilizowekwa.
Akizungumza na vyombo vya Habari Twange alisema shughuli za kuelekea uchaguzi Wa serikali za mitaa na zoezi la kuchukua fomu zinaendelea na anawahakikishia wananchi kuwa vyombo vya usalama vipo hivyo Kila mmoja aliejiandikisha ajiandae na itakapofika mwezi novemba 27 wakapige kura .
"Hakuna atakayekuwa tishio kwa mwenzake uchaguzi utakuwa huru,Wa amani na Wa haki hivyo wananchi washiriki uchaguzi kwa hisia na namna wanavyotaka na kwa upande Wa wanasiasa Wa vyama vyote wakati kampeni zinapoanza wafanye kampeni zao kwa amani na utulivu na vyombo vya ulinzi vipo na vitawalinda kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo"alisema Mkuu wa Wilaya ya Hai.
Aliongeza kwa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwachagua viongozi wanaowataka Wa vijiji,vitongoji na mitaa huku akibainisha kuwa kabla ya hapo kutakuwa na siku kadhaa za kampeni hivyo wajitokeze kusikiliza Sera za wagombea ili waweze kuchagua viongozi sahihi.
"Hai hakuna hekaheka zozote za uvunjifu wa amani,na ninawashukuru wananchi na wadau wote Wa uchaguzi kwa namna wanavyoendesha zao kwa amani na utulivu na ninawaomba waendelee hivyohivyo kudumisha amani hadi siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi kwisha". alisema Twange.
Credit to: Elizabeth R. Mkumbo/JAIZMELA
0 Comments:
Post a Comment