Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la mto Pangani Segule Segule ameonya na kuwataka wananchi kuacha shughuli za kibinadamu zinazoharibu Kingo za mto Rau Moshi Mkoani Kilimanjaro kwani shughuli hizo ndio chanzo Cha mafuriko kuvamia makazi na kuharibu mashamba ya watu.Mkurugenzi wa Bodi ya Maji, Bonde la Mto Pangani Segule Segule (kushoto) akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Mji Mpya Abuu Shayo. (Picha na JAIZMELA)
Amezungumza hayo wakati akikagua Zoezi la udabuaji maji na kutanua Kingo za maji , kuongeza kina n bdp.a kunyoosha Kona hatarishi zilizopelekea mafuriko kuvamia makazi ya watu wa majengo na msaranga katika kipindi cha mvua zilizonyesha mwezi April 2024.
Segule amewaomba wadau mbalimbali Wa Maendeleo kuungana na Bonde la maji mto Pangani kwa kushirikiana kikamilifu katika zoezi hilo la udabuaji maji na kutengeneza Kingo za mto Rau ili pindi mvua zinaponyesha mafuriko yasivamie makazi ya watu na kuleta maafa.
Sambamba na hayo diwani Wa kata ya msaranga Charles Lyimo ametoa shukrani za dhati kwa uongozi Wa Bonde la maji mto Pangani kwa kuona na kuanza zoezi Hilo litakalosaidia kwa kiwango kikubwa wananchi kuondokana na adha za mafuriko pia kuwataka wananchi kupanda miti na kuacha kufanya shughuli zao Ndani ya mita 60 ya mto huo.
Naye Diwani Wa kata ya mji Mpya Manispaa ya Moshi Abuu Mohammed Shayo amesema mwezi Aprili Kata hiyo ilipata adha kubwa ya mafuriko iliyopelekea watu kupoteza Maisha ,makazi na uharibifu mkubwa Kiasi kwamba baadhi ya wakazi walipoteza matumaini ya kuendelea kuishi katika kata hiyo na kukimbia makazi yao .
Ameongeza kuwa ni jukumu la Kila mwananchi anaeishi pembezoni mwa mto huo kutunza mazingira kwa kupanda miti na kuacha kutupa taka hovyo.
Mvua zilizonyesha mwezi April 2024 Mkoani Kilimanjaro zilisababisha mto Rau kujaa maji na mafuriko kuvamiaa makazi ya watu yaliyopelekea maafa makubwa ya vifo vya watu kadhaaa ,uharibifu kaya zaidi ya 690 na kusababisha jumla ya watu 2400 kuathirika na mafuriko hayo hususani kwa wakazi Wa Mji Mpya na Msaranga Manispaa ya Moshi .
Credit to: Elizabeth R. Mkumbo/JAIZMELA
0 Comments:
Post a Comment