Serikali nchini imewataka wazazi na walezi kutowaficha watu wenye ulemavu na wanatakiwa kuwatoa na kuwatambulisha kwa serikali ili waweze kupata huduma muhimu na stahiki .
Waziri Mkuu nchini Mhe.Kasim Majaliwa Majaliwa ameyasema hayo Mkoani Kilimanjaro wakati akifunga Maadhimisho ya wiki ya fimbo nyeupe ambayo huadhimishwa Kila mwaka mwezi October na Chama Cha watu wasioona ( TLB).
Amesema kwa mwaka Wa fedha 2023/2024 serikali imeendelea kuboresha mazingira fikivu kwa watu wenye ulemavu hususani Miundombinu ya elimu ili kuongeza Idadi ya wanafunzi walemavu kwa kuongeza na kuhakikisha Kila mlemavu asieona anapata vifaa saidizi .
Ameongeza kwa kuzitaka taasisi zinapojenga majengo ya shule,hospitali na ofisi kuzingatia na kusimamia maelekezo ya serikali kwa kujenga miundombinu rafiki na fikivu itakayowawezesha watu wenye ulemavu kuingia kwenye majengo hayo na kupata huduma.
Awali mkuu Wa mkoa Nurdin Babu amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa pesa nyingi kwa mkoa Wa Kilimanjaro ili kuboresha miundombinu mbalimbali ya Maendeleo yenye kuzingatia pia mahitaji ya watu wenye ulemavu.
Naye kaimu katibu mkuu wa Chama hicho Lomitu Loata ameishukuru serikali kwa kuendelea kutambua na kuendelea kuwaunga mkono ,kusimamia na , kuhakikisha watu wasioona wanapata haki na mahitaji Muhimu.
Credit to: Elizabeth R. Mkumbo/ JAIZMELA
0 Comments:
Post a Comment