Chuo cha Viwanda vya Misitu Tanzania (FITI) kinaendelea kufanya kazi ya kutoa mafunzo ya kiufundi na kitaaluma katika sekta ya misitu, huku kikijitahidi kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kuboresha ujuzi wa wafanyakazi.
Tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1976 FITI, kimekuwa imekuwa ikitoa mafunzo kwa wanachama wa sekta ya misitu na mbao. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, chuo hicho kimepanua program zake na sasa kinatoa vyeti na diploma katika Teknolojia ya Sekta ya Misitu.
Mkuu wa Chuo cha FITI, Dkt. Zacharia Lupala amesema, “Tunaweka juhudi kubwa katika kuboresha vifaa na mafunzo tunayotoa ili kuwajengea uwezo wanafunzi wetu. Lengo letu ni kuhakikisha wanapata ujuzi wa kisasa unaokidhi mahitaji ya tasnia.”
FITI ina maeneo ya mafunzo yenye vifaa vya kisasa na inashirikiana na wadau wa sekta ya misitu ili kuimarisha ubora wa mafunzo.
Wanafunzi wa FITI wamesema wanafurahia mafunzo wanayopata na wanatumaini kuwa wataweza kutumia ujuzi wao katika kujiajiri au kupata kazi katika sekta mbalimbali zinazohusiana na misitu.
Chuo kinaendelea kuwa chimbuko muhimu la wataalamu katika sekta ya misitu nchini Tanzania, na kinatarajia kuimarisha nafasi yake kama kiongozi katika utoaji wa mafunzo ya viwanda vya misitu.
Mbali na hilo kuelekea mahafali ya 27 mnamo Novemba 1, 2024 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Cecilia Moses ameweka bayana kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas atakuwa mgeni rasmi mbele ya wahitimu 300.
Chuo cha Viwanda na Misitu (FITI) ni taasisi ya umma inayofanya kazi chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii. FITI ilianzishwa mwezi Novemba mwaka 1976 kwa msaada wa kifedha kutoka serikali ya Sweden.
Mwanzoni, lengo kuu la taasisi ilikuwa kuwaelekeza wafanyakazi wa kati wanaohitajika katika uendeshaji wa sekta ya miti inayomilikiwa na serikali, inayojulikana kama Tanzania Wood Industries Corporation (TWICO). Mwishoni mwa kipindi cha ufadhili wa Sweden mwaka 1980, FITI ilifanikiwa kupata msaada wa kifedha kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Finland (FINNIDA) kwa kipindi cha mwaka 1980 hadi 1988.
Kuanzia mwaka 1988 hadi sasa, FITI inaendeshwa na serikali ya Tanzania na lengo lake kuu ni kutoa mafunzo maalum ya kiufundi katika sekta ya misitu na huduma katika sekta ya miti.
Hadi sasa FITI imeendelea kuzalisha wahitimu wengi katika ngazi za astashahada na Stashada.
0 Comments:
Post a Comment