Tanzania huadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka.
Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini. Pamoja na hayo hufanyika gwaride maalum kwa ajili ya mashujaa wetu.
Mashujaa hao walipambana kwa hali na mali kwa ajili ya kuitetea Nchi ya Tanzania wakiwa katika maeneo mbalimbali.Walijizatiti na kujitoa kwa uzalendo mkubwa kwa kuweka rehani Maisha yao kwa ajili ya Tanzania.
Uongozi na menejimenti ya Wilaya ya Serengeti tunaungana na Watanzania wote kuwakumbuka na kuwaombea kheri kutokana na kujali na kudumisha Misingi ya Amani.
Misingi mizuri na imara iliyojengwa wasisi wa Taifa letu baba wa Taifa ,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere Na Sheikh Abeid Amani Karume, imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa Amani na Utulivu,huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote wa Ndani au Nje.
Amani iliyojengwa na imewafanya wageni, wakimbizi na watalii kuiona Tanzania kuwa kivutio na kimbilio.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu katika siku ya Mashujaa |
Vijana nchini wametakiwa kujitafakari kabla ya kufanya lolote katika kutunza Amani na utulivu wa nchi badala ya kuwa na mihemko ambayo italeta ghasia zitakazorudisha maendeleo nyuma.
Akizungumza katika siku ya Mashujaa Mkuu wa mkoa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema mambo yamebadilika ambapo baadhi wamekuwa wakifanya mambo ambayo hayampendezi Mwenyezi Mungu kutokana na kushindwa kutafakari kwa undani kuhusu madhara yake katika siku za usoni.
“Mambo yamebadilikayamekuwa mabaya watu hawana huruma tena wanafanya mambo ambayo hayampendezi Mungu, Watu wengine wanaweza fikiria tu amani tuliyonayo imekuja hivi hivi, hapana na hasa kwa vijana wa sasa, vijana wa sasa wakiona mambo yanakwenda wanasema hiyo ni haki yetu, haki yenu ipiii?”, amesema Nurdin Babu
Babu ameongeza kuwa wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya Mashujaa amewataka kuheshimu mchango wa mashujaa hao ambao waliangalia zaidi maslahi ya taifa kuliko kufanya mambo ya hovyo na kwamba serikali haitaacha kuwachukulia hatua watakaokiuka.
“ Niwaombe tuendelee kuilinda kwa mikono miwili na miguu na macho na masikio amani tulionao, lakini niwaambie hao ninyi mnaofanya fanya mchezo na jambo hili kwenye mkoa, niwape salama kuwa tunataka amani na utulivu kwenye nchi na mkoa wetu wa Kilimanjaro,” amesema Nurdin Babu.
Hata hivyo amewataka wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kushikamana pamoja kuendelea kupiga vita dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo hali inaonyesha sio nzuri hususani wanaume ambao wamekuwa wakipigwa na wenzi wao na kukaa kimya.
“Niviombe vyombo vinavyohusika tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba haya mambo yanapungua kwenye mkoa unyanyasaji wa kinjinsia, kina mama wanapigwa sana, kina baba nao wanapigwa lakini huwa hawasemi, watoto wanafanyiwa vitendo vibaya,” amesisitiza mkuu wa mkoa
Septemba Mosi, 1969 kwa mara ya kwanza, Tanzania iliadhimisha kwa mara ya kwanza Siku ya Mashujaa; miaka michache baadaye ilibadilishwa baada ya ushindi wa Vita vya Kagera dhidi ya nduli Iddi Amini ambapo Julai 25, 1979 majeshi ya Tanzania yalipokelewa mkoani Kagera baada ya ushindi huo na ndipo tarehe ya kuadhimishwa siku ya Mashujaa ilipobadilishwa kutoka Septemba Mosi na kufanyika kila mwaka Julai 25.
0 Comments:
Post a Comment