Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Michael Ngilizu (1967-2023) mnamo Julai 24, 2023 kwa ajili ya Ibada ya kumuaga iliyofanyika nyumbani kwake Kwa Mtei-Mji Mpya. |
Mgambo kata wa anayefahamika kwa jina la Michael Ngilizu (54) ameuawa mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi.
Mauaji hayo yametokea leo majira ya mchana maeneo ya Kwa Mtei katika Kata ya Mji Mpya, Manispaa ya Moshi ambako inadaiwa marehemu alikuwa katika majukumu yake ya kikazi ya kumkamata mtuhumiwa anayefahamika kwa jina la Amdani Mohammed Abdi.
Shuhuda wa tukio hilo Mwanaidi Abdi Omari amesema mtuhumiwa ni mtoto wa dada yake ambaye amekuwa akimsumbua bibi yake kuhusu kumuona baba yake.
“Alianza kumtishia kumwua baba yake wa kambo jana, kwa jitihada tulitafuta msaada tulienda polisi kwenda kuwaambia jamani kuna mtu anamemvamia baba ake mdogo anataka kumwua.,” amesema Mwanaidi Abdi Omari
Wakati mtuhumiwa akitekeleza mauaji hayo inadaiwa kuwa siku ya nyuma yake alikuwa ameingia na vitu vyenye ncha kali na mawe kwa kile ambacho aliwaambia angemwua baba mdogo.
“Anaishi hapa kwa bibi yake, Amdani ni mtoto kibri (ana kiburi) na bibi yake amekuwa akijaribu kuongea naye, jana tulimuona akija na mawe visu ili
ampige baba yake mdogo,” amesema Mwanaidi Abdi Omari
EATV imezungumza na rafiki wa marehemu Seif Abbas namna alivyomfahamu Michael Ngwirizu hadi umauti ulipomkuta.
“Nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kuwa Michael amechomwa kisu amefariki dunia, nilifika eneo la tukio niliona damu zimetapakaa na nlichokiona kingine ni pikipiki ya marehemu,” amesema Seif Abbas
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Kwa Mtei Mary Elirehem Kimei amesema kuondokewa na mgambo mchapakazi ni jambo ambalo limemhuzunisha sana.
“Katika mtaa wangu kumetokea jambo la kushtua, amekuwa mchapakazi, kwa kwa kweli hakuwa mwoga, ni mvumilivu, na shupavu,” amesema Mwenyekiti Kimei.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni dereva wa vyombo vya moto maarufu ‘DEIWAKA’ bado anatafutwa na polisi kwani ametoweka kusikojulikana. Hadi tunaingia studio mama mzazi wa mtuhumiwa, bibi wa mtuhumiwa, baba mdogo wa mtuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Majengo
0 Comments:
Post a Comment