Saturday, January 12, 2019

Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Zanzibar inaadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi kwa sherehe zinazofanyika kwa mara ya kwanza kisiwani Pemba tangu alipoingia madarakani Rais Ali Mohammed Shein.

ILIKUWAJE?
Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. 

Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. 

Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. 

Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi. Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. 

Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. 

Wakati mfalme mpya, Jamshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar. 

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. 

Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu. Na Ilipofika Aprili 26, 1964 liliungana na Tanganyika kutengeneza kile kinachofahamika kwa sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Sasa ni miaka 55 tangu mapinduzi hayo yafanyike. Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Dkt. Ali Mohamed Shein ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo hapo hii leo. Akizungumza na wanahabari. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa pili Mohamed Aboud Mohamed alithibitisha uwepo kiongozi huyo na viongozi wengine wan chi mbalimbali akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli. 

Aidha Dkt. Shein amewasamehe wafungwa 12 walioonyesha nidhamu wakiwa jela.

Kauli mbiu mwaka huu ni “Mapinduzi yetu ni Umoja wetu tuyalinde kwa maendeleo yetu.”




0 Comments:

Post a Comment