Licha ya kuanza mchezo wa kwanza kwa ushindi lakini jana
India ilishindwa kutamba mbele ya wenyeji wa michuano ya soka kwa mataifa ya Asia
Falme za Kiarabu baada ya kupokea
kichapo cha mabao 2-0 (kwa mtungi).
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba
la Zayed Sports City kulishuhudiwa wenyeji hao wakigusa nyavu katika dakika ya 41
ya mchezo pale Khaflan Mubarak alipofumua mkwaju wa nguvu kwa kutumia mguu wake
wa kulia upande wa kulia juu baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ali Ahmed
Mabkhout.
Bao hilo lilikuja baada ya muda wa mashambulizi na kosakosa nyingi
katika lango la India. Bao la pili lilifungwa na Ali Ahmed Mabkhout kwa mguu wa
kulia akipokea pasi ya kiungo Ali Hassan Salmin kisha kuupiga upande wa kushoto
chini na kumwacha mlinda mlango Gurpreet
Singh Sandhu.
Mchezo mwingine wa kundi A
kulishuhudia Bahrain ikishindwa kutamba mbele ya Thailand baada ya kukubali
kichapo cha bao 1-0 mtanange uliochezwa jijini Dubai. Kundi B liliendelea tena
jana kwa Jordan kuizabua Syria kwa mabao 2-0 mjini Al Ain.
Leo hatua ya makundi
itaendelea kwa Australia kuikabili Palestina katika mchezo wa kundi B mtanange
utakaochezwa katika dimba la Rashid jijini Dubai utaanza saa 8:00 mchana
Australia ilianza kampeni zake kwa kichapo hivyo leo itakuwa ikitaka kurudhisha
makali yake.
Kundi C litaingia vitani kuanzia za 10:30 jioni jijini Abu Dhabi
na Al Ain pale Ufilipino ya kocha raia wa Sweden Sven-Goran Eriksson
itakapoikabili China katika mchezo unatarajiwa kuwa mkali. Pia Jamhuri ya
KYRGYZ itapambana vikali Korea Kusini.
0 Comments:
Post a Comment