Wednesday, January 9, 2019

Mahakama yatupilia mbali kesi ya mapitio ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao


Mahakama Kuu kanda ya Mtwara imetupilia mbali kesi ya kutaka mapitio ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao iliyofunguliwa na Baraza la Habari Tanzania MCT, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu 

LHRC na Muungano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC). Katika kesi hiyo washtakiwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu. 

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Wilfread Ndyansobera. Katika maamuzi yake Jaji Ndyansobera amesema kwamba maombi ya wapeleka maombi hayana uzito na kwamba walalamikaji wameshindwa kuthibitisha  jinsi gani Kanuni hizo zitakavyoathiri haki za msingi za walalamikaji katika masuala ya uhuru wa habari na mawasiliano ya mitandaoni.

Jaji wa kesi hiyo amesema mahakama imekubaliana na hoja za  Mawakili wa Serikali kuwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni zimetungwa kwa mujibu wa sheria. Kesi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Septemba 4, 2018.

0 Comments:

Post a Comment