Sunday, January 6, 2019

AFC Asia Cup: India yaanza vema hatua ya makundi

Sunil Chhetri akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao dhid ya Thailand January 6 mwaka huu
Kundi A limeanza kampeni zake za kuwania taji la soka kwa  Mataifa ya Asia mwaka huu huku India ikiizabua Thailand kwa mabao 4-1. Sunil Chhetri mwenye miaka 34 alifunga mara mbili katika ushindi huo. 

Ushindi huo ni wa kwanza mkubwa kwa India baada ya miaka 55 katika mechi za ufunguzi kwenye michuano hiyo. Mabao mengine yalifungwa na Anirudh Thapa na Jeje Lalpekhlua Katika mechi ya Ufunguzi siku ya Jumamosi wenyeji wa mashindano hayo Falme za Kiarabu waligawana pointi na Bahrain kwa sare ya bao 1-1. 

Bao lililofungwa kwa mkwaju wa penati dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo huo na Ahmed Khalil limewafanya wenyeji hao kuiangazia India watakaposhuka dimbani Januari 10. Kundi C linaanza kampeni zake leo kwa China kucheza na Jamhuri ya Kyrgyz mjini Al Ain. Kikosi cha China kinachonolewa na Marcelo Lippi aliywahi kuinoa miamba ya soka Italia na kutwaa taji la Dunia mwaka 2006 kitajiuliza leo. 

Kocha huyo amekuwa na mafanikio makubwa katika soka la Asia kwani mwaka 2013 aliipa taji ligi ya mabingwa klabu ya Guangzhou Evergrande. Lippi amekaririwa akisema wanachotaka ni kuwa na matokeo mazuri ili kuweza kusonga mbele.

0 Comments:

Post a Comment