Inaweza ikawa ngumu kuamini
kilichotokea jijini Abu Dhabi katika mchezo wa fainali ya mataifa ya bara la Asia
lakini ndivyo hali ilivyo pale miamba ya soka ya Asia Japan ilipoangushwa na
Qatar kwenye mchezo ulichezwa kwenye dimba la Mohammed Zayed.
Japan iilishindwa
kutwaa taji hilo kwa mara ya tano baada ya kuzabuliwa kwa mabao 3-1 na hivyo
Qatar kutawazwa mabingwa wapya wa Mataifa ya Asia mwaka huu. Qatar ambao
watakuwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2022 wameweka rekodi waliyoshindwa kuiweka
kwa takribani miaka 63 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo.
Mabao ya Almoez Ali,
Abdelaziz Hatim na Akram Afif yaliamua kipute hicho cha soka Februari Mosi. Pia
zawadi wa ufungaji bora ilikwenda kwa Almoez Ali akifikisha mabao tisa kwenye
mi chuano hiyo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 anayehudumu katika klabu ya
Al Duhail alifunga katika dakika ya 12 ya mchezo bao la tisa baada ya juhudi na
kumwacha mlinda mlango wa Japan Shuichi Gonda akisalia hana msaada.
0 Comments:
Post a Comment