Wednesday, June 27, 2018

China yazindua teknolojia mpya ya Satelaiti

Taifa la China limefanikiwa kurusha chombo hewani katika teknolojia mpya mapema asubuhi ya Juni 27, 2018. 
Teknolojia mpya ya Satelaiti Mbili zilizobebwa katika chombo cha Long March-2C ikizinduliwa Kusini Magharibi mwa China kwenye kituo cha Satelaiti cha Xichang. Uzinduzi huo umefanyika Juni 27, 2018 (Picha na Xinhua).


Uzinduzi huo umefanyika katika mji wa Xichang katika Kituo cha Satelaiti Kusini Magharibi mwa China. Saa 5:30 asubuhi kwa saa za China (sawa na saa 11:30 alfajiri EAT), chombo hicho kilifanikiwa kukaa katika obiti yake. 

Madhumuni ya kupeleka chombo hicho ni kuunganisha mtandao wa satelaiti kwa teknolojia mpya na kutazamwa duniani. Uzinduzi huo ambao taifa hilo limeufanya ni wa 278 katika roketi za Long March.

0 Comments:

Post a Comment